Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Wachunguzi wa gonjwa sugu la malaria kutoka ifakara health centre wakiongozwa na doctor okumu,wamegundua kuwa soksi chafu zinazonuka uvundo zafaa katika mapambano dhidi ya malaria.Ule uvundo wa soksi ni harufu kutoka mwili wa binadamu hivyo mbu waipatapo harufu hii,kwa haraka huzivamia soksi na kuzengea hapo muda wote wakidhani kuna mwanadamu around.Kwa hiyo unaweza weka soksi chafu zenye uvundo kwenye kona ya chumba chako cha kulala,mbu wote watajaa huko na wewe utalala salama salimini kwa sababu ukali wa harufu ya soksi unazidi hata harufu ya mwili wako,mbu hawatakuwa na habari na wewe,watakuwa busy na soksi usiku kucha.Pia ukitaka kuwaua,ni rahisi tu,wakishajaa eneo la soksi zenye uvundo ni rahisi kuwaangamiza kwa dawa ya kupuliza.Lakini watafiti wanaendelea kutafuta dawa yenye kufanana na harufu ya soksi zenye uvundo(source,BBCSWAHILI).MALARIA HAIKUBALIKI,TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA!