Kumbe Samunge ipo Kenya

Spear_

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,603
486
Najua hiyo heading itakuchanganya ila habari ndo hiyo, watani wetu nilifikiri wangeishia kudanganya dunia kuhusu Kilimanjaro na Serengeti tu... sasa wanadai Samunge ipo South Kenya na ni mwendo wa dakika 45 from Nairobi Airport, wageni wengi wanapitia Kenya kwani wameshaambiwa kutoka KIA (Tanzania) hadi Samunge ni 800Km (hapa wameongea ukweli japo hawajasema ni kwenda na kurudi) Mbunge wa Ngorongoro Hon. Kaika Telele amekuwa mbogo serikali kunyamazia tu bila kukanusha habari hizi....

Ninachojiuliza hivi Serikali yetu ipo wapi....?


Source: gazeti la nipashe
 
Kenya inazidi kupata umaarufu na usishangae wakisema Mzee Mwasapile ni Mkenya....
 
Serikali yetu ipo likizo, na wizara ya utalii ni kama ilifutwa haipo tena. Watu wanahaha na posho tu, ingekuwa vipi Kenya wachukue hata hii mikoa michache ya kaskazini nayo itangaze kuwa ni mali ya Kenya. Hata mzee mseveni aangalie anachotaka upande wake nacho ajisogezee, nchi haina viongozi, yamebaki majina tu.
 
Serikali yetu ipo likizo, na wizara ya utalii ni kama ilifutwa haipo tena. Watu wanahaha na posho tu, ingekuwa vipi Kenya wachukue hata hii mikoa michache ya kaskazini nayo itangaze kuwa ni mali ya Kenya. Hata mzee mseveni aangalie anachotaka upande wake nacho ajisogezee, nchi haina viongozi, yamebaki majina tu.

Watanzania tumezidi uvivu yaani hata Samunge itangazwe na Serikali? lets face the truth we are not creative and uvivu umetuzidi!! lets wake up!! huyo babu wa samunge mwenyewe bado tuna mbeza wakati wenzetu wakenya wanamchukulia serious! angekua kenya kweli ungesikia jinsi tunavyo lalami oh serikali haituwezeshi kwenda kenya oh... blah blah...kutwa kucha!!!
 
Wakenya nawaunga mkono, maana hawajakosea lolote katika matamgazo yao, hawaudanganyi ulimwengu. Wanatangaza huduma wanayoitoa na kujiingizia fedha za kigeni. Hawajasema "mlima Kilimanjaro uko Kenya," bali "njoo Kenya utaona mlima Kilimanjaro." na kweli watakupeleka mahali ambapo utauona. Wanapoongoza watalii kwenda kutembelea mbuga zetu wanaingia kwa vibali na kuwapatia watalii huduma kadiri ya makubaliano; na wanapata faida. Na wakisema "Samunge iko kusini mwa Kenya, kijiografia na kimantiki hawajakosea" Mwenyewe si unaiona kwenye ramani na mipaka unaiona, ila kutokea pande za Kenya huduma ni bora zaidi.
Hili suala halipo kwenye utalii tu, angalia hata bandari. Mara nne mniwafaidishe wakenya nipitishe mizigo yangu Mombasa kuliko usumbufu unaopatikana bandari ya Dar. Tusiwalaumu wakenya ila viongozi wetu waliolala; wakenya hawajatuzuia kutoa huduma wanazozitoa wao.
 
Back
Top Bottom