Kumbe Rais wa Muungano akiwa Zanzibar yuko chini kwa Rais wa Zanzibar

KALABASH

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
493
206
Katika kuwasili uwanjani kwenye sherehe za muungano aman stadium zanzibar Rais wa muungano ameingia uwanjani kabla ya Rais wa Zanzibar. Kwa maana hii Rais wa muungano anatangulia uwanjani ili awe tiyari kumkaribisha "mdogo" wake atakapowasili uwanjani. Kwa wenye kuulewa huu muungano nielemisheni.
 
ndo ujue huu muungano ulivyokuwa wa kipuuzi raisi wa Jamhuri ya Muungano ndiye anaetakiwa kuwa mkubwa lakini kwa sababu muungano huu ni wa kipuuzi Zanzibar imebaki kuwa nchi hivyo na raisi wao kuwa mkubwa katika nchi yake kwa kifupi Kikwete ni mualikwa
 
Hapo wanaadimisha mapinduzi ya mwaka 1963, wakati huo zanzibar ilikuwa nchi, na tanganyika ilikuwa nchi.
kwa maana hiyo leo JK amekaribishwa kama mgeni katika sherehe za mapinduzi.
Kinachonikera ni kwamba wazanzibari wanaadimisha sherehe za mapinduzi bila hata kumkumbuka mwanamapinduzi wa Kweli John Gideon Okello.
 
mwenyewe nmeshangaa. Rais wa Muungano anampolea rais wa zanzibar. inakuaje baba mwenye nyumba ushindwe kuingia chumbani kwa mkeo?. inatakiwa baba mwenye nyumba uwe na sauti kwako. Mia
 
Ndio Muungano wetu huo ambao watawala wanaogopa kuujadili ama kuuvunja au kuuboresha wanataka iwe hivyo hivyo na haieleweki kabisa!!hakuna itifaki wala isibati wala unafiki hovyo tuu!!!basi tuwe na Tanganyika pia!!
 
Ni simple logic wakuu.
uhuru sio wa Tanzania bara au muungano bali ni uhuru wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar yupo,sasa inakuwaje Rais wa Muungano ndio awe mwenye shughuli?
Mwenye shughuli ndio anaingia wa mwisho
OTIS
 
Swali dogo tu- kwani shughuli hii ilikuwa ya nani? Rais wa Muungano au Rais wa Zanzibar?
 
Katiba ya Zanzibar inatamka wazi kuwa Zanzibar ni nchi.
Kwa msingi huo mkuu wa Zanzibar ni rais wa Zanzibar,sherehe za mapinduzi ni za nchi ya Zanzibar kwa mujibu wa katiba yao,sasa wewe unashangaa nini.
 
Katika kuwasili uwanjani kwenye sherehe za muungano aman stadium zanzibar Rais wa muungano ameingia uwanjani kabla ya Rais wa Zanzibar. Kwa maana hii Rais wa muungano anatangulia uwanjani ili awe tiyari kumkaribisha "mdogo" wake atakapowasili uwanjani. Kwa wenye kuulewa huu muungano nielemisheni.

Ingekuwa busara rais wa JMT kutokwenda kuepuka mgongano wa kiplotokari.
 
Hapo wanaadimisha mapinduzi ya mwaka 1963, wakati huo zanzibar ilikuwa nchi, na tanganyika ilikuwa nchi.
kwa maana hiyo leo JK amekaribishwa kama mgeni katika sherehe za mapinduzi.
Kinachonikera ni kwamba wazanzibari wanaadimisha sherehe za mapinduzi bila hata kumkumbuka mwanamapinduzi wa Kweli John Gideon Okello.
John Okello alipigana mpaka akamaliza kazi, ndipo Karume akarudishwa na ndege toka daressalaam alikokuwa alikula kuku wa biriani kwa bosi wake na mfadhili mkuu nyerere, Okello aliamriwa kwa bastola akabidhi ofisi kwa Karume, japo Okello alikuwa keshahutubia nchi kuwa Zanzibar imekombolewa.
Rais wa Zanzibar ndie kiongozi wa watu wa Zanzibar, lakini ni Waziri asiyekuwa na Wizara maalum katika Nchi na Taifa la Tanzania, sharti Rais wa Jamhuri aingie mwanzo, lakini kwa kuwapa heshima wananchi wa Zanzibar sio mbaya aonekane ndie mwenye kuongoza sherehe.
 
Katiba ya Zanzibar inatamka wazi kuwa Zanzibar ni nchi.
Kwa msingi huo mkuu wa Zanzibar ni rais wa Zanzibar,sherehe za mapinduzi ni za nchi ya Zanzibar kwa mujibu wa katiba yao,sasa wewe unashangaa nini.

wadau nisaidieni, katiba ya zanzibar ina sema zanzibar ni nchi, je katiba ya muungano yasemaje katika jambo hili?
 
Wakuu Wazanzibari wana nchi yao, bendera yao na ndiyo maana wanataka yao yawe yao peke yao lakini madini ya bara wanataka sehemu yao. Huu ni unafiki wa ajabu kabisa.
 
Jk kaenda kufinya ubwabwa wa sherehe tu......mambo ya sijui kaingia wa mwisho au wa kwanza yeye haihuuuuuuuuuuuuu!!! Mambo yote pilau na kuku.........au pweza!!!!!!!
 
Zanzibar ni Nchi huru, Rais yeyote anayeingia huko yuko chini ya mhe. Rais wa Zanzibar
 
Back
Top Bottom