Kumbe polonium 110 ndio chanzo cha mwakyembe na mwandosya

DARKMAN

Senior Member
Aug 23, 2012
122
85
Wazee nimepata taarifa kutoka mbeya ambako waheshimiwa walikuwa wanatoa sadaka ya shukrani kwa mungu kutokana na maswahibu yaliyowakuta. Walikwenda na riport za ugonjwa wao uliokuwa unawasumbua ambazo hizo riport ndizo walizoziwasilisha selikalini, Kifupi ni kwamba waliwaonyesha watu wachache sana hizo ripoti ambapo ni viongozi wa kanisa pekee walioona riport hizo na hakuruhusiwa mtu yoyote kuingia kwenye kile chumba. lengo la kuwaonyesha ripoti hizo ilikuwa ili kuwaongezea imani kuwa bila mungu wao wasingeweza kuwa hai. mtoa taarifa ni mzee wa kanisa ambaye anauelewa kidogo kwenye mambo ya sayansi.

Riport inaonyesha kuwa kilichokuwa kinawasumbua ni Radioactive element inayojulikana kama polonium 210, na wao iliingia kupitia kwenye ngozi ndio maana ilienda kuattack cell za ngozi na kuingia kwenye bone-marrow ya mifupa. Laiti kama wangekuwa wamewekewa kwenye chakula wakaila, results would have been much detrimental, maana ingesababisha organs failure.

Vipimo vyote walivyofanyiwa havikuonyesha kitu, sample zao zilichukuliwa na kupelekwa kwenye maabara ya nuclea ya india ndiko jibu lilikopatikana. unaambiwa kwa conventional toxicological test zilizopo katika mahospitali ya kawaida huwezi kugundua kitu chochote. na unaambiwa hata baada ya kugundua kuwa polonium 210 ndiyo inayowatesa, kama wangekuwa walishwa, ingekuwa kazi sana kui-neutralize kwa sababu neutralizing agents nyingi za radioactive elements ni toxic (sumu) katika mwili wa mwanadamu. Walichofanyiwa kina mwakyembe ni bone-marrow implant

Unaambiwa 1microgram ya polonium 210 inatosha kuwaua watu wazima 5, na inaweza kutengeneza umeme wa 140watts. 1microgram ya polonium 210 ni sawasawa na gramu moja gawanya vipande milioni moja (kwa wasiojua vipimo vya metriki)

Ndio maana yule kamanda alielitangazia taifa kwenye vyombo vya habari kuwa mwakyembe hajapewa sumu DCI KANUMBA (weka manumba) katulia kimya na alijifanya kwenda kumuhoji Mhe Sitta. Sitta alipoenda kumuona Mwakyembe India alikuwa anajua kila kitu kuwa kapewa sumu ndio maana alisema hadharani.

USHAURI KWA WANASIASA HASA HASA WALIOJIPAMBANUA KUWA NI WAPAMBANAJI WA UFISADI, Ukiona umenawa maji sehemu na akaanza kuwashwa nunua JIKI nawia sehemu zote unazohisi umejishika kupunguza makali maana unaweza usifike india. Hii polonium 210 ndio iliyomuua yule ex-KGB spy alipokuwa uhamishoni UK, yeye alikunywa kwenye kahawa.
 
Kama mola hajaamua uondoke duniani then watesi wako watakuwa wanafanya kazi bure kujaribu kukua!
Bse the divine mission has to be accomplished ndo unaweza kufa!
 
Sorry darkman, mkuu hivi Polonium na Uranium ni ipi mbaya zaidi?? na hivi vyote ni viasilia vya nuclear??
kama ni uranium basi tumekwisha vile kuanzia mwakani tutaichimba hapahapa bongo!
 
Nadhani hakuna ukweli hapa. Ni Urusi peke yake ndiyo kwa sasa ina hiyo sumu na handlers wake.

Jiulize: ni Mtanzania gani angeweza kuwawekea hiyo sumu bila kudhurika mwenyewe? Tanzania haina hiyo sumu. Hata Marekani hawana. BBC walitangaza ni Urusi peke yake ndio inao uwezo wa kuwapa watu pollonium powder kwa sasa.
 
Mwakyembe asichekeane nao tena maana aliyemwekea ofisini kwake kwenye sink la kunawia mikono alimtambua kwani asiwaweke hadharani la sivyo wakishika Nchi watammaliza
Hebu hao wazee wa Kanisa waniPM iwapo ntaoata majina ntayaweka
 
haya Mwakyembe na kaka yako Mwandosya Mshukruni sana Mungu wetu atupaye uzima na ulinzi kila kukicha mwenye rehema na aliyejaa neema bado anawapenda na tunawatakia mema zaidi ndani ya nchi yetu.
 
Mwakyembe asichekeane nao tena maana aliyemwekea ofisini kwake kwenye sink la kunawia mikono alimtambua kwani asiwaweke hadharani la sivyo wakishika Nchi watammaliza
Hebu hao wazee wa Kanisa waniPM iwapo ntaoata majina ntayaweka

nimeshafanya hivyo check PM
 
Guys hiyo kitu bado ipo mikononi mwa watu believe me itatumiwa tu tena, tuliambiwa hapaha[a JF nani aliileta na kwa lengo gani. It is about time kuwaamabia wamerakani kuwa hii kitu inaweza kuchukuliwa na magaidi ikawa tishio kwa usalama wa wamarekani. Ni vizuri ikafikishwa CIA nao watajua kuwa kuwa dangerous toxic material is in someone hands in Tanzania and that can pose a danger to Americans, hapo ndio tunaweza kuwa na nafuu.
 
Nadhani hakuna ukweli hapa. Ni Urusi peke yake ndiyo kwa sasa ina hiyo sumu na handlers wake.

Jiulize: ni Mtanzania gani angeweza kuwawekea hiyo sumu bila kudhurika mwenyewe? Tanzania haina hiyo sumu. Hata Marekani hawana. BBC walitangaza ni Urusi peke yake ndio inao uwezo wa kuwapa watu pollonium powder kwa sasa.

Huo unaosema wewe ni uongo, hiyo polonium 210 sio urusi tu ndio inayo, inapatikana kirahisi sana kana unazo centrifuge za ku-enrich radioactive material, kama unaweza google yasser Arafati polonium report utakuta kuna clip ya utube ya aljazeera wanamuhoji prof mmoja wa radiology anaelezea juu ya kuipata hiyo polonium, ni element inayopatikana ardhini kama uranium, sema inakuwa siyo lethal mpaka iwe enriched kwenye centrifuge ndiyo inakuwa na half life kubwa hada miaka 300+, kwa hiyo unataka kuniambia hizo centrifuge wanazo russia peke yao.

Ngoja nikuambie, Polonium kama radioactive element nyingine nyingi ukiacha Uranium hazihuishwi kwa sababu matumizi makubwa ya radioactive element ni kwenye energy na ballistic war head. sasa energy inayokuwa emmitted na uranium ni nyingi kuliko element nyingine na upatikanaji wake ni massive
 
Mkuu kama ni polonium 210 wamepigwa kweli basi uwezekano wa kupona ni mdogo lazima wafe kwa mda mfupi sana,na nikweli ile haina dawa na maranyingi inatumiwa lead katika kuipunguza lakini huwezi kuitumia lead katika mwili wa binadamu manake ni sumu.

Hi polonium handling yake ni too expensive na kuisafirisha hiyo ni ndege inakodishwa kabisa kama ni kutoka urusi mpaka tz,na wanakua wataalamu maalumu na vifaa maalumu na mara nyingi hiyo inakuaga ni deal ya kijasusi katika level ya nchi na nchi kwa hiyo mie bado namashaka na ukweli kuwa waliwekewa polonium 210
 
JamiiForums hakika ni darasa tosha. AHSANTENI!
 
nimefuatilia mjadala huu kwa umakini kwani mimi mwenyewe nilikuwa nataka nijue hasa ni kitu gani kilichokuwa kinamsumbua Dr mwakembe na ndugu yake mwandosya
maoni yangu: ni kwa nini manumba alisema ya kuwa mheshimiwa mwakyembe hajalishwa sumu? ni nani aliyemtuma kufanya hivyo na alifanya hivyo kwa maslahi ya nani?

lakini pia katika nchi ambayo inajipambanua kuwa ina demokrasia wakati watu wake wanauwawa kama wadudu tufahamu nini kutokana na haya yanayoendelea hadi hii leo?

je mbona ripoti iliyowasilishwa serikalini kutoka india kuhusu ugonjwa wake hadi leo hatujaambiwa na serikali ya kuwa ni kitu gani ambacho kilikuwa kinamsumbua mwakyembe?

na kama khali yenyewe ndo kama hii ya kuwa ukijipambanua kuwa mpiganaji dhidi ya ufisadi basi wewe unakuwa ni adui wa mafisadi je ina maana ya kuwa hawa mafisadi wanataka kuhalalisha ya kuwa ni haki yao kula na kufuja raslimali ya umma bila kuhojiwa na mamlaka yeyote na kama ndivyo ilivyo ya nini kuwa na wawakilishi huko bungeni si bora tusiwe na wabunge kwani wao wapo kwa ajili ya kuwasemea wananchi juu ya matatizo yanayowasumbua likiwemo na hili la ufujaji wa mali ya umma

kaka mwakyembe naamini ya kuwa kuna fundisho kubwa sana umelipata na umejua ni jinsi gani serikali yako ilivyo katili hadi kwa watu wake wenyewe.

watanzania tunaomba nikiwemo na mimi binafsi ya kuwa kama serikali wameshindwa kutoa ripoti hadharani basi jitokeze kwenye vyombo vya habari useme ni kitu gani kilichokuwa kinakusumbua kwa kipindi chote huko india nasi tutakuwa nyuma yako kuandamana kupinga tabia hiyo na pia tujue ni kwa nini waliamua kufanya hivyo kana kwamba wao ni mungu
tunashukuru juhudi zao zilishindwa kwa jina la yesu mungu azidi kukuzidishia uzima tele na maisha bora katika utendaji wako serikalini na nje ya serikali
 
I accept correction. Nilichopashwa kusema ni aina ya pollonium iliyomuua Mrusi Uingereza inapatikana Urusi peke yake, na ni mali ya serikali. Ndio ushahidi waliotumia Waingereza kuwalaumu Warusi.

Handling ya hii sumu ni sophisticated kiasi cha kutia wasiwasi kama Tanzania inaweza kuitumia.

Kwa vyovyote vile, kama serikali ya Tanzania ingehusika kuwawekea sumu hawa mawaziri, basi singetegemea waendelee kuweko serikalini. Sidhani kuna ukweli kwenye madai haya.
 
Ni wakati wako Mh:mwakyembe kutujuza yaliyo nyuma ya pazia,usiwalinde sana wauwaji hawa,wataje kwa faida ya taifa ili wote tuwajue ili tusije kuwapa madaraka makubwa wauaji na wezi hawa.
 
Nadhani hakuna ukweli hapa. Ni Urusi peke yake ndiyo kwa sasa ina hiyo sumu na handlers wake.

Jiulize: ni Mtanzania gani angeweza kuwawekea hiyo sumu bila kudhurika mwenyewe? Tanzania haina hiyo sumu. Hata Marekani hawana. BBC walitangaza ni Urusi peke yake ndio inao uwezo wa kuwapa watu pollonium powder kwa sasa.

Chezea system weye,TISS umewasahau eee!.
 
Mkuu kama ni polonium 210 wamepigwa kweli basi uwezekano wa kupona ni mdogo lazima wafe kwa mda mfupi sana,na nikweli ile haina dawa na maranyingi inatumiwa lead katika kuipunguza lakini huwezi kuitumia lead katika mwili wa binadamu manake ni sumu.

Hi polonium handling yake ni too expensive na kuisafirisha hiyo ni ndege inakodishwa kabisa kama ni kutoka urusi mpaka tz,na wanakua wataalamu maalumu na vifaa maalumu na mara nyingi hiyo inakuaga ni deal ya kijasusi katika level ya nchi na nchi kwa hiyo mie bado namashaka na ukweli kuwa waliwekewa polonium 210

Usiidharau TISS,wana uwezo wa kuyafanya yale usio dhania.
 
Back
Top Bottom