Kumbe Mtikila dikteta!?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Mtikila apata pigo DP

Na Kizitto Noya

CHAMA cha Demokratic (DP) kinachoongozwa na Mchungaji Christopher Mtikila kimepata pigo kwa kuondokewa na viongozi wake waandamizi ngazi ya taifa na mkoa ambao wamejiondoa na kuanzisha chama kipya cha Alliance for Tanzania Farmers (AFP).

Naibu Katibu Mkuu wa DP, Said Soud na Katibu wa Vijana wa Chama hicho Rashid Rai jana waliongoza kundi la wanachama wa DP kusajili chama kipya cha AFP ambacho kimepewa usajili wa muda na kupewa miezi sita kutafuta wanachama 200 kutoka kila mkoa nchini kabla ya kupata usajili wa kudumu.

Wakizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana, viongozi hao walisema kuwa wameamua kukihama DP kutokana na udikteta wanaodai unafanywa na mwenyekiti wake, Mchungaji Mtikila.

Kaimu Mwenyekiti wa AFP, Said Soud alisema kuwa takriban viongozi wote na wanachama wa DP visiwani Zanzibar, wilaya ya Mkuranga na baadhi ya mikoa na wilaya wamekihama chama hicho na kujiunga na chama AFP.

"Idadi ya wanachama wa DP tulioondoka nao ni kubwa, takriban viongozi wote na wanachama wa Zanzibar, Mkuranga na wengi wa kitaifa wameondoka na tupo nao AFP," alisema Soud.

Naye Rai alisema kuwa wameamua kuihama DP baada ya kuona kuwa wamekosa nafasi ya kutekeleza malengo yao kama wanasiasa.

Alidai kuwa DP inaongozwa kidikteta ndio maana hata mfumo wa uongozi wake umejaa watu waliokuwa karibu na mwenyekiti wake hivyo kuashiria kuwa chama hicho kipo kwa maslahi binafsi ya watu.

"AFP imeanzishwa kutetea maslahi ya jamii ya wakulima baada ya kuona kuwa kundi hilo ambalo ni kubwa katika jamii ya Tanzania halina mtetezi. Tutapita kila mkoa, wilaya, kata na vitongoji kuwahamasisha wakulima kujiunga na chama hicho," alisema Rai.

Alitaja dira ya chama hicho kuwa Darubini ya Uchumi Tanzania, Siasa Safi na Uwajibikaji.

Akizungumzia tukio hilo Mchungaji Mtikila alisema viongozi na wanachama wanaodai kukimbia udikteta katika chama chake ni waasi waliofukuzwa.

Alidai kuwa Said Soud alifukuzwa akiwa Naibu Katibu Mkuu baada ya kukabiliwa na tuhuma kadhaa za ubadhirifu wa mali za chama na Rai ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Vijana wa DP alifukuzwa kutokana na tuhuma hizo hizo na kwamba wote walifukuzwa Juni 12 mwaka huu.

Mtikila alisisitiza kuwa hakuna kiongozi mwingine yoyote wala wa mwanachama wa DP aliyekihama chama kama inavyodaiwa na viongozi hawa wawili kwa chama hicho hakina wanachama Zanzibar wala Mkuranga.

Alisema DP bado iko madhubuti na leo inaanza mkutano wake mkuu kumchagua mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Mwekahazina na wakurugenzi wapya wa idara mbalimbali za chama hicho.

source mwananchi
 
Kuna fununu kwamba hawa wote wamekihama chama cha DP kutokana na Mtikila kushupalia kwake kupinga mahakama ya kadhi nchini. Na pia kwamba mengi sana tutasikia kuhusu Mtikila. Mipango ya kuanzisha chama ilianza siku nyingi lakini Mtikila amekuja akawaudhi sana baadhi ya wanachama wake ambao wengi wao ni waislamu kwa kupinga kuanzishwa mahakama ya kadhi.
 
mtikila inaonekana kachanganyikiwa, anashindwa kutofautisha siasa na emotion zake binafsi.

halafu msimamo wa chama si unatolewa na vikao vya chama sasa yy kama mwenyekiti kwa nn hajaitisha kikao ili kauli yake ipate baraka au kuibuka ktk hali ambayo hatowaumiza wafuasi wake wenye tofauti na dini yake??
 
Mtikila is ana Islamophobe na ana conspiracy theories kibao kiasi kwamba hata anapokuwa na point inakuwa vigumu kum-support.

Halafu ana sifa zote za udikteta na umangimeza.
 
Bila Mtikila na DP, TZ itakua hamna siasa tena, maana upande wa pili wa shilingi hautakuwepo zaidi ya CCM. DP and Mtikila wataendelea kuimarika tu.

Walio hama ni walewale tu kina pangu pakavu ambao ni wengi kwenye siasa za TZ.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom