Kumbe mpenzi wangu ni mke wa mtu?

makoye78

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
672
229
Jamani, kwa takribani miezi saba nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi na dada mmoja mwenye umri wa miaka 35, mwaka mmoja zaidi yangu! Ukweli mimi ni mwanafunzi na dada huyu ni mtumishi ktk idara ya afya hapa Dodoma, hivyo nikiwa na shida ya kifedha huwa ananisaidia sana!
Swala ni kwamba, hivi majuzi ndo kaniambia ya kuwa yeye ni mke wa mtu, lakini hajisikii kuendelea tena na mumewe ambaye wamezaa nae watoto wawili! Sababu ni kwamba bwana yule hana elimu na cha zaidi, anatumia vibaya pesa za biashara yake ambayo mtaji alipewa na mkewe huyo!
Swali, je unanishauri niendelee na huyu mwanamke ama nimuache?
Je nikiendelea naye mwisho wake ni nini?
 
mmmmh, ngoja waje washauri, mie leo na kisirani nisije kuharibia uzi bure.
 
Mweee!!Mke wa mtu sumu.Itafika kipindi hata wewe utatafutiwa mwingine ambaye ataelezwa kuwa unatumia fedha zake vibaya.Shukuru Mungu umeujua ukweli..kimbia haraka na utubu kwa hiyo dhambi(Kumbuka mtenda hutendwa)
 
kuna thread hapa JF ya kaka aliyekatwa mkono kwa kutembea na mke wa mtu. isome halafu utafahamu uamuzi wa kuchukua
 
Yeye anataka mume mwenye elimu gani? Na kama tatizo ni elimu, mwambie ampeleke shule. Kwa wewe huuyo hakufai, maana inavyooneka wewe unachopenda hapo ni pesa yake tu.
 
Mume wa huyo dada atakuja kukusumbua badae, endapo atakua hajakubaliana na swala la mkewe kua na mwanaume mwingine. Achana na mahusiano ya namna hii yatakuletea stress .
 
Mmmh... Achana na huyo mke wa mtu... Uliza wenzio yaliyowakuta..
 
Ulikuwa hujui kuwa ni mke wa mtu ila ameshakuambia live! Swali; unaomba ushauri wa namna ya kumuacha au? Nadhani hapo huitaji ushauri zaidi ya kuachana nae. Labda kama una dhiki ya vijisenti vyake unaweza muomba akawa mfadhili wako! Kila la kheri.
 
Yeye anataka mume mwenye elimu gani? Na kama tatizo ni elimu, mwambie ampeleke shule. Kwa wewe huuyo hakufai, maana inavyooneka wewe unachopenda hapo ni pesa yake tu.

Yeye ni daktari (Doctor of Medicine- MUCHS), anadai mumewe ni form four tu! Mimi ninafanya masters, hivyo anaona mie ninamfaa zaidi! Ila ukweli ni kwamba, baada ya yeye kuniambia juu ya hili la mumuwe, ndo nikaanza kustuka ya kuwa hanipendi bure, bali elimu na sura! Hii ni kutokana na moangezi yake niongeapa nae! Ndo maana naomba ushauri.
 
Mweee!!Mke wa mtu sumu.Itafika kipindi hata wewe utatafutiwa mwingine ambaye ataelezwa kuwa unatumia fedha zake vibaya.Shukuru Mungu umeujua ukweli..kimbia haraka na utubu kwa hiyo dhambi(Kumbuka mtenda hutendwa)

Asante Lilian, kumuacha ni vema! Suala ni kwamba nitumie mbinu ipi kumwacha bila kumfanya akaumia sana?
 
Asante Lilian, kumuacha ni vema! Suala ni kwamba nitumie mbinu ipi kumwacha bila kumfanya akaumia sana?

Njia nzuri kuliko yote ni Kumwambia UKWELI(kuwa yeye ni mke wa mtu na unaheshimu sana hiyo taasisi ambayo Mungu alisema iheshimiwe na watu wote)...
Bora aumie sahizi kidogo kuliko aje kuumia zaidi baadae.Believe me ..ukiendelea na hayo mahusiano utakuja kujuta..
 
mhm hapo patamu...huyo ujue kabisa ukibaki nae basi nawe itafika wakati atakupitia mbavuni na kutoa utamu kwa mwengine na pia ukitaka kumuacha ujue anaweza kuwa mgumu kwa hilo in the sense that kasha invenst kwako both financially na emotionaly so kumbwaga tuu inaweza kuwa ngumu kaka. jiandae kwa vituko
 
Asante Lilian, kumuacha ni vema! Suala ni kwamba nitumie mbinu ipi kumwacha bila kumfanya akaumia sana?

Ni bora ukamuacha hata akiumia atapoa baadae,huwezi jua kama mumewe ameshashtukia au la,na kama amestukia hujui anapanga nini!? be a gentle man na achana na huyo mwanamke haraka,afu you are educated, kuwa makini kaka tusijekupoteza, kuliwa mke INAUMA!!
 
Asante Pombekali!
 
oooh, naomba iendelee kuwa slow tu.

Nikiwa nakusoma huwa najikuta meno yako nje sababu nakunja sana macho kupunguza mwanga.

Hujambo lakini?

i haven't! my internet is slow now, so i can't wait for the menu to change my color.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom