...Nakumbuka nilianza mwaka 1980 kwa kutumia kakamera ka shemeji yangu ambapo mdogo wake na mimi tulikaiba na kwenda kupigia picha zetu (mie na mdogo wa shemeji yangu) sehemu mbalimbali. Matokeo yakanivutia na kunifanya niwe na kiu ya kuwa mpiga picha.Miaka mitano baadaye rafiki yangu mmoja alinizawadia Pentax Spotmatic ambayo nilikuwa sijui hata namna ya kuitumia. Bahati wakati huo kulikuwa na masomo ya jioni ya photogrtaphy pale Goethe Institute (jengo la IPS) na mwalimu wangu wa kwanza alikuwa Tom Mwewuka wa us info. services.
Masomo ya vitendo yalinifanya niwe napiga picha mitaani kama mazoezi hatimaye nikajikuta ukumbi wa YMCA ambako disko la ma DJ Kalikali, Neagre J na wengineo lililokuwa juu sana enzi hizo. Wengi hawajui siri hii kwamba picha nilizokuwa napiga zilikuwa ni kwa ajili ya pesa za kusafishia (sio faida) ili kupata mazoezi.
Nilifanikiwa sana kwa hilo kwani nilifaulu vizuri masomo yangu. Baada ya masomo niliendelea pale YMCA na kisha mitaani ambako kila mtu alitaka kupigwa picha na mimi kutokana nadhani na uzuri wa picha zangu. Nakumbuka picha za ajali ya jumba lililobomoka na kuua watu wawili mtaa wa Msimbazi ambapo gazeti la Mfanyakazi walitumia nne hivi. Hizo picha zangu za kwanza gazetini.
Lakini kujikita katika fani ilitokea kwamba siku moja, nakumbuka mwaka 1989, Jah Kimbute na kundi lake la Roots and Culture walifanya onyesho pale YMCA na waliniomba niwapigie picha za kumbukumbu. Mmoja ya wageni waalikwa alikuwa Attilio Tagalile wa Daily News ambaye hakuja na mpiga picha. Akaniomba nimpatie picha moja na nilipompa nakumbuka kwa mara ya kwanza Daily News walitumia picha ya msanii ukurasa wa mbele.
Nahisi walivutiwa jinsi nilivyomtoa Jah Kimbute huku rasta zake zikiwa zimeruka juu na uso kaukunja kwa hisia kali za kuimba. Kuanzia hapo Tagalile akanitia moyo wa kuwa mie ni mtu wa magazeti. Pia mpiga picha mkuu wa Daily News wakati huo hayati Vincent Urio aliyekuwa na studio binafsi pale YMCA iliyoitwa Studio Laura akavutiwa nami na kunichukua.
source; UKIAMBIWA MICHUZI NI MVIVU UTAKUBALI? « BONGO CELEBRITY
Ndugu yetu amekuwa akisema yeye ni mmoja wa wamiliki wa zile sehemu za kupigia picha na mpaka gari lake lina "poster za photo point" inasemekana yeye wala hausiki kabisa na photopoint, yeye ni kama deiwaka vile. Kama yumo humu atueleze basi
Bi.Mkubwa pamoja na wenzio taratibu!!!!
Jamaa kaanzisha thread akihitaji kujua/kujulishwa hicho kinachomkereketa.
Sasa kama unaona haina chochote cha maana kwako, soma then achana nae.
Sasa mambo ya kusema admin achuje sijui am-ban yanatoka wapi???
Au kwakuwa mmezoea kuwaona akina fulani tu wakianzisha thread na nyie kuichangamkia, wakianzisha wengine inakuwa nongwa????
Thread ngapi zinaanzishwa zinazozungumzia watu na mbona hamlalamiki???
Halafu mnatakiwa mjue kuwa hii thread iko mahali gani, jukwaa la siasa, michezo, celebrities au jokes.Msikurupuke tu kumshambulia Lyampinga kwa kuwa tu mnataka akina fulani ndo waanzishe thread.Lyampinga usife moyo we endelea kukandamiza tu utapata majibu hapa hapa muda si mrefu.
Eti michuzi hawezi kuwa fisadi????ingawa simaanishi kuwa ni fisadi lakini mtu huwezi kusimama mbele ya watu kusema kuwa fulani sio fisadi kwa kuwa tu unamjua.Kuna mambo mengi sana ambayo watu wanayafanya lakini hatuyajui.
Kwahiyo kama mtu una jambo la kuchangia uzungumzie suala la michuzi kumiliki au kutomiliki photo point, na si kusema kuwa michuzi ni fisadi au sio fisadi, anachouliza mdau ni kuhusu umiliki tu.
Sio kwamba jamaa ana washabiki wengi humu bali Michuzi anakubalika. Sio lazima kuwa mshabiki kumtetea mtu ila its just appreciation of what he does and not what he has.Mkuu hii thread ingeanzishwa na superstars wa kuchangia kashfa na maneno ya kejeli usinge yaona ungeona tu data zinamwagwa tu.
Ila kwa vile jamaa amegusa penyewe watu wamekuwa mbogo humu ''MKuki kwa .............''Jamaa ana washabiki wengi sana humu JF mmegusa sio penyewe.
Akueleze wewe na nani?
Sasa yeye akiwa deiwaka au mmiliki inakuhusu nini?
Alishawahi kukwambia ni ya kwake?
Huu ndio upashkuna, acha kujadili vitu vya watu, jifunze utu kidogo....
sijui Clouds nk.,
Ndugu yetu amekuwa akisema yeye ni mmoja wa wamiliki wa zile sehemu za kupigia picha na mpaka gari lake lina "poster za photo point" inasemekana yeye wala hausiki kabisa na photopoint, yeye ni kama deiwaka vile. Kama yumo humu atueleze basi
...MICHUZI is a brand,
...brand is a tangible product, jamaa alianzia kupiga picha mitaani leo hii ukisikia MICHUZI huulizi product zotokanazo na brand MICHUZI, kuanzia picha kwenye blog yake, mpaka picha zinazopigwa kwenye studio zake, hata kama yeye hakuhusika...
hata kama photopoint si ya michuzi, brand MICHUZI inaendelea kuwa associated na photopoint, kwa mtaji huu anacholipwa/anachojilipa ibakie ni siri yake!