Kumbe Michuzi Photopoint sio ya kwake!!!

Ndugu yetu amekuwa akisema yeye ni mmoja wa wamiliki wa zile sehemu za kupigia picha na mpaka gari lake lina "poster za photo point" inasemekana yeye wala hausiki kabisa na photopoint, yeye ni kama deiwaka vile. Kama yumo humu atueleze basi

Kamanda inabidi utafute issue nyingine ya kufanya...Hebu soma vizuri majibu ya wadau hapa chini.

Akueleze wewe na nani?
Sasa yeye akiwa deiwaka au mmiliki inakuhusu nini?
Alishawahi kukwambia ni ya kwake?
Huu ndio upashkuna, acha kujadili vitu vya watu, jifunze utu kidogo....

Tafadhali usimuite Mhe Balozi wa Zain deiwaka. Alihusika kwa kiasi kikubwa katika uanzishwaji wa Photo Point. Amiliki au asimiliki hio siyo issue hapa JF. Nadhani unataka kuleta umbea wa kumtafuta mmiliki halisi wa photo point ili iweje. Maadam ulimsikia Michuzi akisema yeye ni mmiliki, naomba amini hivyo hivyo, waliokuambia yeye ni dei waka ni wanga.

Kwahiyo?

Sasa ajieleze ili iweje?

- Brother Issa Michuzi for president! Lyampinga ingia mjini taratibu mkuu! Siku hizi kuna shares kwenye umiliki kwa hiyo unaweza kuwa mmiliki usiwe mmiliki pia, lakini mmiliki anyways!

Have a nice day bro!

Nakuakikishia jamaa sio mmiliki na pia niko JF sikunyingi mkulu nimeamua kurudi upya... Kama malumbano yataendela basi inabidi tulete vithibitisho, when it comes to shares hana hata moja

Naona hapa umeamua kumshikia bango Michuzi.... Kama una vithibitisho weka hapa sio maneno marefu na kulia lia tu..

Tena msome vizuri mdau hapa chini

Unataka kufahamu umiliki wake wa Photpoint ili iweje???? Kwani wewe una kampuni gani??? Discuss great issues for the jamii ana not individuals!!!! Great minds..............Naona una lako jambo na Michuzi so mtafute muyamalize!!!!! Yaani mambo ya saloon,, vijiweni na upashukuna wa wakao barazani unataka kuuleta hapa kwenye jamii Forum ili tupoteze muda kuujadili???? Kwanza unatakiwa umwombe Michuzi msamaha.
 
Ndugu yangu Kibunago wewe ni mpenzi wa Michuzi inaelekea, lakini ukweli unabakia palepale kwamba alidanganya watu kwamba yeye ni mmiliki wakati yeye sio mmiliki.
 
Ulipokuja na thread uliita tetesi, kwamba huna uhakika na unataka kujua wengine wanasemaje. Thread yako ikaitwa hivi:

Tetesi: Kumbe Michuzi Photopoint sio ya kwake!!!

Baadaye, watu wakatoa maoni yao, lakini pamoja na kwamba uliita ni tetesi, ukaja tena kutuambia una uhakika. Ukasema hivi:

Nakuakikishia jamaa sio mmiliki na pia niko JF sikunyingi mkulu nimeamua kurudi upya... Kama malumbano yataendela basi inabidi tulete vithibitisho, when it comes to shares hana hata moja

Sasa je, ilikuwa ni tetesi ili upate maoni ya wengine wajuavyo au ilikuwa ni tangazo dogo kuwajulisha watu kile ujuacho? Kama the former is true, basi kubaliana na waliyosema watu na itakuwa mwisho wa thread. Na kama the later is true, ndo hapo watu wanakuuliza, ili iweje?
 
Admin afanye mpango wa kuchuja thred vinginevyo atoe warning kabla ya kubun mtu. Kuna issue nyingine unaizumzia bila kujua wanaitafsiri kama kashfa.

Inagaliwe hiyo.
 
This is too low! Let us discuss issues. Kumiliki au kutomiliki photo studio, kunasaidiaje kuboresha nchi yetu.
 
Lyampinga, au uliambiwa kuwa hiyo photo point ilianzishwa kwa fedha za EPA? Tunajua Michuzi sio fisadi na kama wakwapuaji wa EPA ndio wamiliki basi ni dhahiri Muhudin hawezi kuwa mmoja wa wamiliki!! Hii imekaa vipi wanajanvi?
 
Admin afanye mpango wa kuchuja thred vinginevyo atoe warning kabla ya kubun mtu. Kuna issue nyingine unaizumzia bila kujua wanaitafsiri kama kashfa.

Inagaliwe hiyo.

Bi.Mkubwa pamoja na wenzio taratibu!!!!
Jamaa kaanzisha thread akihitaji kujua/kujulishwa hicho kinachomkereketa.
Sasa kama unaona haina chochote cha maana kwako, soma then achana nae.
Sasa mambo ya kusema admin achuje sijui am-ban yanatoka wapi???
Au kwakuwa mmezoea kuwaona akina fulani tu wakianzisha thread na nyie kuichangamkia, wakianzisha wengine inakuwa nongwa????
Thread ngapi zinaanzishwa zinazozungumzia watu na mbona hamlalamiki???
Halafu mnatakiwa mjue kuwa hii thread iko mahali gani, jukwaa la siasa, michezo, celebrities au jokes.Msikurupuke tu kumshambulia Lyampinga kwa kuwa tu mnataka akina fulani ndo waanzishe thread.Lyampinga usife moyo we endelea kukandamiza tu utapata majibu hapa hapa muda si mrefu.
Eti michuzi hawezi kuwa fisadi????ingawa simaanishi kuwa ni fisadi lakini mtu huwezi kusimama mbele ya watu kusema kuwa fulani sio fisadi kwa kuwa tu unamjua.Kuna mambo mengi sana ambayo watu wanayafanya lakini hatuyajui.
Kwahiyo kama mtu una jambo la kuchangia uzungumzie suala la michuzi kumiliki au kutomiliki photo point, na si kusema kuwa michuzi ni fisadi au sio fisadi, anachouliza mdau ni kuhusu umiliki tu.
 
Una hakika kama Lyampinga anauliza kutokana na kutofahamu anachouliza? Au ni udaku tu uliokukaa hadi vidoleni?
 
...
Kwahiyo kama mtu una jambo la kuchangia uzungumzie suala la michuzi kumiliki au kutomiliki photo point, na si kusema kuwa michuzi ni fisadi au sio fisadi, anachouliza mdau ni kuhusu umiliki tu.

Kuhusu kumiliki au kutomiliki Photopoint, huyo Lyampinga aliyeleta thread hii alishajijibu mwenyewe, ndio maana watu wanahoji sisi tufanye nini sasa! Alijijibu hapa:

Nakuakikishia jamaa sio mmiliki na pia niko JF sikunyingi mkulu nimeamua kurudi upya... Kama malumbano yataendela basi inabidi tulete vithibitisho, when it comes to shares hana hata moja
 
...ni mali ya cornel apson mwangonda

na ile plot 87 kipawa iliyotajwa kaama registered office ya kagoda...na faili kupotezwa kwa maagizo ya rais......sasa hivi ile plot ndio makao makuu ya CASPIAN CONSTRUCTIONS......[
jibu]

siku zote namuona michuzi kama mhangaikaji aliyejituma mpaka kufika hapo alipofika kwani mimi nimemuona tangu enzi alipokuwa mpiga picha wa mtaani. na kwa hili nimekuwa namsifu sana.

hata hivyo kama hii ya kuhusisha photo shop na huyo mkuu aliyetajwa na pm inabidi nijiulize mara mbili mbili. wahenga walisema "ndege wa aina moja huruka pamoja". mahali nchi yetu ilipofika kwa kweli siku zote najitayarisha kukumbana ukweli wa busara za "ukistaajabu ya musa utaona ya firauni".
huenda chini ya hii thread kuna habari kubwa itafuata. ngoja nisubiri
 
Na pia naomba watu muanze kuwaza mbona kile kijarida chetu cha cheche Mwanakijji hapeleki tena kwa ndugu yetu Michuzi. Radio mbao zinasema kuna mnene mmoja ambaye ndio anasemekana ni mmiliki wa Photo Point na Mwanakijiji kamuandika sana kwenye kijarida cha cheche kwa mabaya aliyofanya
 
Last edited:
Ndugu yetu amekuwa akisema yeye ni mmoja wa wamiliki wa zile sehemu za kupigia picha na mpaka gari lake lina "poster za photo point" inasemekana yeye wala hausiki kabisa na photopoint, yeye ni kama deiwaka vile. Kama yumo humu atueleze basi

Huyo jamaa anayo blogu.Mwandikie huko.Atakujibu kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
 
Does it matter? Si bora tuwatafute wa Kagoda italeta maana zaidi?
 
- Umasikini bwana, mtu akipata kidogo tu imekua nongwa ukiona hivi ujue Michuzi keshafanyiwa kila njama aanguke, lakini wapi riziki ya Mungu binadam utaiweza wapi, watch sasa hivi watamtupia Michuzi mkono wa Albino bwa! ha! ha!,

- Mkuu Michuzi, siku hizi hakuna Azimio La Arusha, wewe kusanya Michuzi tu mara ya mwisho nilipoangalia list of shame ya Dr. Slaa sikuona jina lako, umewashika pabaya maadui wewe ni kukamata hapo hapo! Wameanzisha wee vi-blogu uchwara sasa vinajifia vyenyewe huku yako ikitanua tu sasa wameanza mikingamo hawa! Wamezoea lazima wawe kina Msuya, Warioba, Mkapa, na Kingunge ndio wenye mali ukiwa Michuzi hawataki, lol!

Michuzi for presidente!
 
mhh hebu niunganishe dots, au kwasababu michuzi yuko close sana na mafisadi kwenye kila party zao anahudhuria nilimuona kwenye kitchen party ya mtoto wa mataka alikuwa bize sana na mama lowasa tehetehe!
 
Na hii inahusiana vipi na photopoint? Kazi ya Michuzi unahifahamu lakini?
 
mhh hebu niunganishe dots, au kwasababu michuzi yuko close sana na mafisadi kwenye kila party zao anahudhuria nilimuona kwenye kitchen party ya mtoto wa mataka alikuwa bize sana na mama lowasa tehetehe!

Lorah..ikiwa kazi yako wewe ni kupiga picha utaanza kuchagua nani umpige na nani usimpige....?
 
Back
Top Bottom