Kumbe mh. Juma Mnkamia amegombea ubunge kuganga njaa?

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,689
Mwanzoni mimi nilitafsiri kwamba Mheshimiwa sana Juma Mnkamia mbunge wa kondoa kusini alitoka VOA kuja kugombea ubunge kwa minajiri ya kusukuma fasta gurudumu la maendeleo la jimbo lake maana Mh. wa awali P. Degela alionekana amechoka. Sasa kutokana na alivyoshobokea suala la nyongeza ya posho nimebadili mtazamo juu yake.

Zitto Kabwe Mbunge kijana kama yeye pamoja na J. Makamba waliona kupokea posho kama hizo za malaki katika kipindi hiki ni kama kutaka kupasua raha wakati wanainchi wako katikati ya shida, wakati Zitto akipinga posho hizo zisilipwe na huenda Rais hajaidhinisha yeye Mkamia alidai ZITTO siyo msemaji wa Rais alikubaliana na maneno ya spika kwamba wavute tu huo mshiko mnene baraka ziliisha tolewa. maskini weee!!! sasa Juma Mnkamia yako wapi posho zimeota mbawa. Wachunguzi wa mambo wanadai kwamba waheshimiwa wote ambao wanataka posho hizo za laki mbili ni wale ambao wanajua wazi kabisa 2015 hawatakuwepo tena mjengoni, hivyo wanataka ile dhana ya chukua chako mapema usepe itendeke, sasa je! na Juma Mnkamia ni mojawapo wa hao? Mbona namwona kama kijana sana. Ana njaa gani? Si asome yaliyomkuta Mwakalebela wa TFF? TFF akakosa na Iringa akakosa.
Mnkamia njaa zako hizo zitakuponza 2015 Kondoa ukose na VOA ukose,

Mliokaribu nae mnisaidie kumhabarisha haya,.
 
Kwanza hajui kazi ya mbunge, pili hana dira na tatu ni mtu anayependa show offs. Nkamia siyo mwanasiasa wala kiongozi bali ni mchumia tumbo!
 
huyu jamaaa kwa utangazaji tu hafai
sijui waliompa ubunge wanafikiri nini
 
Wananchi wa TZ ndo hawafai kabisa; Kwani inakuwaje mjinga au mtu mwenye akili ndogo anapata uongozi? kama jibu ni pesa, basi ache nao wale.
 
Alidhani anatangaza mpira kwa kuleta mambo ya "Goooooooo a laaaa ni mpira wa kurushwaaaaa" huku sisi tunapata pressure kwa kusikia redioni bila kuona LIVE
 
Hivi waandishi/watangazaji wa habari wanafurahia matunda ya Nkamia bungeni. Kama wasanii wanavyofurahia matunda ya Sugu mjengoni?
 
Huyu jamaa aliwahi kupita jeshini. Wakati akiwa huko siku moja aliumia na toka hapo alijifanya mgonjwa mpaka kozi ikaisha. Kimsingi alipita jeshini kama urembo tu hakuna alichoambulia. Hata sasa atapita free. Yaani free, kiuchumi na kiukombozi wa taifa. Walatini wanasema, "Tabula rasa." Maana yake sifuri kabisa.
 
Juma Nkamia ni Kizee.. Uwezi kumlinganisha umri na zitto or j.makamba
 
Juma Nkamia ni Kizee.. Uwezi kumlinganisha umri na zitto or j.makamba
Ila kwa hii kauli aliyoitoa alionyesha kweli yeye ni mzee lakini kwa dodoma anawezakupita tena bwana, watuwadodoma wanahisa na magamba!
 
Mke wake Kapigwa DISCO alikamatwa na DESA,

Nkamia mwenyewe alikuwa anasoma UK muulizeni alipata shahada gani, ni mmoja wa wabunge wenye elimu hewa. Kuna kijana mmoja anaitwa Suedi Mwinyi anamjua vizuri sana Juma Nkamia. Lakini ndio uzuri wa demokrasia yetu, anyone can be mbunge hata Masanja mkandamizaji.
 
.............Unajua kiangalia ile senema ya mjengoni unaona kuna EPISODE ya vijana wa CCM kutaka eti nao kubishana na vijana wa Oposition hususan CDM, na ninaamini watakua wanajipanga kwenye vikao (Chako ni Chako) kuna wakati nilikua naona lUSINDE, Kawawa, Serukamba....(sasahivi naona kabatizwa kwa majimengi katulia tulia kidogo),.......sasa huyu Mkamia aliamua kumkamia Zitto kumbe asijijue hatoshi.......................ameshindwa hata kujiuliza kwa nini JK hakumchukua yeye kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais wa Sudan ya kusini akamchukua Zitto na kutamka anependa kurithiwa na Rais Kijana...............hvyo mwenzie alipotamka kwamba anajua Rais hajasaini Mkamia badala ya kUMKAMIA ZITTO angesoma alama za nyakati na kuona mwenzie ana tie na Mkulu..........
 
Katika mjadala wa posho ulioendeshwa na BBC mwaka jana ndipo nilijua Nkamia hakuna kitu kichwani.
Alikuwa anatetea posho kwa nguvu zote huku akijitetea kwamba zito ameshakula posho miaka mitano sasa anapotaka zifutwe sasahivi anakuwa hamuelewi.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom