Kumbe Matajiri waliovamia uongozi CCM ni majambazi!

Mkira

JF-Expert Member
May 10, 2006
425
119
ii Habari baada ya kuisoma nimeona ni vema . Tupige kelele
ili chama cha CCM kiwangalie matajiri wake kwa macho mawili!!

Na siyo tu kukimbilia michango yao mikubwa at the expense of our people being killed!!

Lengo ni kuhamasisha JK na wana CCM wengine kusafisha chama!
Ili konokono watoke! Nia aibu kwa chama kikubwa kama CCM kukubali kupokea majambazi kuwa viongozi wao simply tu kwa TAMAA YA KUCHANGIWA HELA TENA WAKATI WA UCHAGUZI! HILI LISIKALIWE KIMYA WALIJADILI KWENYE KIAKO CHAO CHA JUNI 2006. NIMEANZA KUFARIJIKA KUWA YALIYOSEMWA KUHUSU WABUNGE WALIOGUSHI VYETI WAMEANZA KUFUATILIWA!
LABDA NI WAKATI MUAFAKA HIYO TOPIC IFUFULIWE(ILIKUWA HOT TOPIC BCSTIMES). LEO NIMESIKIA KUWA WATATU TAYARI WAMEHOJIWA NA DCI NA WOTE NI WA CCM.

HABARI KUHUSU TAJIRI JAMBAZI NI HII

Imetolewa mara ya mwisho: 02.06.2006 0947 EAT

•
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya kizimbani akituhumiwa ujambazi

sogeza Habari Zinazoshabihiana
• Mwenyekiti CCM Wilaya atuhumiwa kwa ujambazi 30.05.2006 [Soma]
• Mfanyabiashara wa Arusha kizimbani akidaiwa kutapeli 19.05.2006 [Soma]
• 'War Bus', wenzake wakamatwa Arusha 24.04.2006 [Soma]

*Asomewa mashitaka tisa ya wizi wa magari, silaha
*Ni mfanyabiashara anayemiliki kiwanda cha samaki
*Nako Dar kesi ya Askofu wa Marekani yanguruma

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa CCM wa Wilaya ya Musoma Mjini, Bw. Joseph Obeto, amefikishwa kizimbani kwa tuhuma za ujambazi ikiwamo kukutwa na magari ya wizi, silaha na risasi.

Mwenyekiti huyo alifikishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Musoma, ambapo alisomewa mashitaka tisa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Bw. Kapita Mwaruka, mtuhumiwa huyo alisomewa mashitaka tisa yakiwamo ya kukutwa na magari ya wizi na kughushi hati za magari.

Pia mashitaka mengine aliyosomewa ni kukutwa na risasi kubwa tofauti na bastola aliyokutwa nayo, hivyo kuashiria risasi hizo zilikuwa ni kwa ajili ya matumizi mengine.

Bw. Obeto ambaye pia ni mfanyabiashara anayemiliki magari na kampuni ya KOTRA, alijisalimisha katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Musoma mwanzoni mwa wiki hii, baada ya Polisi kumtafuta.

Naye Grace Michael, anaripoti kuwa shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka katika kesi ya kujipatia zaidi ya dola za Marekani milioni mbili kwa udanganyifu kupitia jina la Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bw. Jimmy Julius (45) ameieleza mahakama jinsi watoto yatima na wajane walivyokesha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, wakisubiri msaada kutoka Marekani.

Ushahidi huo ulitolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Bi. Euphemia Mingi. Mshitakiwa katika kesi hiyo ni Askofu wa Kanisa moja la Marekani, Bw. Peter Mutafungwa.

Ilidaiwa kuwa wajane, watoto yatima waliokuwa uwanja wa ndege siku hiyo walikuwa wakisubiri msaada wa tani 360 za chakula, viatu, dawa na dola za Marekani 2,250,000 kutoka kwa mshitakiwa huyo.

Bw. Julius ambaye ni Mwenyekiti wa Shirika la Jamii linajishughulisha na kutoa misaada kwa watoto yatima, wajane na wasiojiweza, alidai waliahidiwa kupewa msaada na shirika la Children Pastors International, lililoko Marekani kupitia Taasisi ya Mwalimu Nyerere.

Alidai kuwa baada ya kuambiwa kuna msaada huo walipewa maelekezo na Bi. Angela Chaila ambaye ni Mwandaaji Mipango wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, kuwa wanatakiwa kutafuta kibali cha msamaha wa kodi ili msaada huo uweze kuletwa nchini.

Bw. Julius alidai mahakamani, kuwa walifanikiwa kupata kibali hicho ambacho walipewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya kutuma kibali hicho, Bw. Mutafungwa alidai kimechelewa, hivyo aliwataka wakate tiketi ya ndege kwenda Marekani na kurudi, ili aweze kuleta msaada huo.

Baada ya kupata ujumbe huo, waliamua kwenda kuchukua mkopo katika Benki ya Akiba wa sh. milioni moja na kuwachangisha wajane na watoto yatima sh. 600,050 ambazo walizitumia kwa kukata tiketi ya Bw. Mutafungwa, ambaye alitakiwa kuwasili nchini Septemba 30, mwaka juzi ambapo aliahidi kuwa atalipa gharama hizo baada ya kufika Dar es Salaam.

Alidai kuwa siku hiyo ilipofika, yeye na vikundi mbalimbali vya utamaduni, watoto yatima, wapiga picha na wajane, walikwenda uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea Bw. Mutafungwa, ambaye aliwasili saa 6 usiku, na baada ya kumpokea, alisomewa risala na kuchezewa ngoma na waliambulia kukumbatiwa, na hakuwa na kitu chochote alichokuja nacho kama alivyokuwa ameahidi.

Bw. Julius alidai baada ya kumpeleka kwenye nyumba waliyokuwa wamemwandalia, walimwacha apumzike na aliwaomba kuwa fedha hizo angezilipa Oktoba 2, mwaka juzi, lakini hakuweza kufanya hivyo, aliendelea kuwazungusha bila kuwapa misaada kama alivyotakiwa.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kesho mahakamani hapo ambapo upande wa mashitaka utakuwa na shahidi mwingine.
Tuma kwa Rafiki Nakala inayochapika
 
Hii ni mada nzuri... habari hii iliporipotiwa na gazeti la "Uhuru" wala hawakutaja kama jamaa ni Mwenyekiti wa CCM!! Walimtaja kama mfanyabiashara maarufu!!!
 
Sioni kama lina ziada. Hata kwenye upinzani kuna majambazi. Kama ninavyosisitiza siku zote CCM ipo sawa ila kuna baadhi ya wana CCM ndio hawapo sawa.
 
Sioni kama lina ziada. Hata kwenye upinzani kuna majambazi. Kama ninavyosisitiza siku zote CCM ipo sawa ila kuna baadhi ya wana CCM ndio hawapo sawa.

Mkuu ukisema CCM iko sawa ila baadhi ya wana CCM hawapo sawa inakuwa vigumu kuingia akilini. CMM ni wana CCM na sio bendera tu au majengo. Ukisikia kiongozi wa CCM ni fisadi, CCM haiwezi kukwepa, ni sawa na kusema mimi msafi ila mkono wangu mchafu. Hao hao wana CCM wakifanya jambo zuri wanasema ni CCM, inapaswa kuwa hivyo hivyo hata wakifanya jambo baya.
Ni vizuri kama tukikubali matatizo ya chama yanayosababishwa na kuuza uongozi. Siasa siku hizi imekuwa dili, ni njia ya kujitajirisha lakini inabidi ujanja sana, watanzania ni kama wameanza kuamka, kwa hiyo wanaanza kutambua kuwa wengine ni wezi tu sio viongozi.
 
Sijui kwanini Mwandishi ameweka mambo 2 makubwa ktk Habari moja...lkn pia Habari ya mfanyabiashara (M/Kiti wa CCM) imekuwa Fupi na ndio yenye kichwa cha habari....Wakati ile ya Mchungaji ndio ndefu lkn mwandishi hakuweka kichwa cha Habari au hata Bulletin...Tumwachie mwandishi....

Katika Jambo Baya na la AIBU hakuna kama la huyu mchungaji...!!! Bahati Mbaya hata waombaji nao wamekuwa wajinga..."kumchangia mfadhili"
 
Mkira
Kuna siri kubwa nyuma ya haya mambo ya Obeto_Obeto alikuwa na amekuwa msitari wa mbele si katika kupora ma benki na kuvamia watu pekee ila yeye na Ntombi aliyekuwa RPC Mara wamekuwa wakiendsha shughuli za uvuvi haramu wa kutumia sumu katika Ziwa Victoria .Ntombi alitgemewa kuwa IGP Nchi ingaliwaka moto maana ni haramia na sasa yuko Makao makuu ya Polisi .Kwa watu wa Musoma waulizwe watakueleza juu ya matendo ya Obeto na Ntombi yalipelekea hata watu kuawa hadi leo ziwani lakini hakuna aliye wahinkukamatwa kisa wananchi wamechoka na sumu ya majini lakini Ntombi alikuwa na empire kubwa na Obeto .

Obeto na Mbunge wa Musoma mjini bwana Mathayo wana connection na wana kesi ya mauaji ya mtu ambayo ilifunikwa kwa nguvu ya CCN.Walimuua na kumchoma mti matakoni na kesi hii hadi sasa watu wamekosa pa kwenda kwa kuwa sasa Mathayo ni Mbunge na Obeto ana pesa ba ndiye kiongozi wa CCM kama inavyo semwa .

Ukisha kuwa mwana CCM uko juu ya sheria hata ukiua hakuna wa kukugusa .
 
Vipi umefika salama Moscow? au ulikuwa na maana ya Kinondoni- Moscow?
 
Vipi umefika salama Moscow? au ulikuwa na maana ya Kinondoni- Moscow?

Masatu wewe wanijua vyema sina feki za kijinga hazina maana kwangu .Again ungaliweza kuniuliza hili swali kwenye mada husika kama uliona ni muhimu sana ama kwenye PM na ukaacha mada ya ujambazi ika flow .Spining mlianza zamani sana naona .
 
Sioni kama lina ziada. Hata kwenye upinzani kuna majambazi. Kama ninavyosisitiza siku zote CCM ipo sawa ila kuna baadhi ya wana CCM ndio hawapo sawa.

Kaka usemayo ni kweli kabisa, tenaa huko kwetu kanda ya Ziwa ni balaa, wanasiasa/viongozi wa dini na wafadhili wa siasa/dini ni majambazi ama wafadhili wa ujambazi na wananchi wengi wanawafahamu. Lakini kwa kuwa CCM ni chama tawala ni lazima tuanzie kwao ili wasaidie kusafisha hao majambazi ndani ya chama chao na hata walio ndani ya upinzani na wasije kufanya kama alivyofanyiwa Justine Nyari wa Arusha ambaye alitoka kishujaa na hakuna anayezungumzia tena aaliyoyafanya wakati ule na waliomkamata akiwamo aliyekuwa RPC kule Arusha, Bwana Nzowa (yuko Dar kitengo cha Dawa za Kulevya) hana amani tena na serikali ya sasa maana anaweza kuharibikiwa ama kupata matatizo zaidi.

Binafsi nafahamu viongozi wawili kwa uhakika kabisa ni majambazi na sasa wana nyadhifa katika dola kupitia CCM na hao ni Dar es Salaam na Singida, ukiachia mbali kanda ya ziwa. Hii ni hatari kubwa kwa Usalama wa Taifa letu na jamaa wa UWT wanajua akiwamo Mzee Elisifa Ngowi (yule yule wa EPA ambaye hajaguswa). https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/9246-usalama-wa-taifa-mpo-likizo-10.html
 
Sioni kama lina ziada. Hata kwenye upinzani kuna majambazi. Kama ninavyosisitiza siku zote CCM ipo sawa ila kuna baadhi ya wana CCM ndio hawapo sawa.

Arguments za aina hii ndio zinazoifanya Afrika izidi kudidimia. Mtu anapoambiwa unakosea anahalalisha kosa lake kwa kusema.... "mbona fulani alifanya..."
 
Arguments za aina hii ndio zinazoifanya Afrika izidi kudidimia. Mtu anapoambiwa unakosea anahalalisha kosa lake kwa kusema.... "mbona fulani alifanya..."

Tabia za Mugabe na aina ya utawala wake ndiyo umejaa sehemu kubwa ya watawala wa Afrika maana bado hatujawa na viongozi .Kesi ile ya mauaji Musoma huyu kiongozi wa CCM anahusika na Mbunge Mathayo wote .Lakini no word .
 
Mkira
Kuna siri kubwa nyuma ya haya mambo ya Obeto_Obeto alikuwa na amekuwa msitari wa mbele si katika kupora ma benki na kuvamia watu pekee ila yeye na Ntombi aliyekuwa RPC Mara wamekuwa wakiendsha shughuli za uvuvi haramu wa kutumia sumu katika Ziwa Victoria .Ntombi alitgemewa kuwa IGP Nchi ingaliwaka moto maana ni haramia na sasa yuko Makao makuu ya Polisi .Kwa watu wa Musoma waulizwe watakueleza juu ya matendo ya Obeto na Ntombi yalipelekea hata watu kuawa hadi leo ziwani lakini hakuna aliye wahinkukamatwa kisa wananchi wamechoka na sumu ya majini lakini Ntombi alikuwa na empire kubwa na Obeto .

Obeto na Mbunge wa Musoma mjini bwana Mathayo wana connection na wana kesi ya mauaji ya mtu ambayo ilifunikwa kwa nguvu ya CCN.Walimuua na kumchoma mti matakoni na kesi hii hadi sasa watu wamekosa pa kwenda kwa kuwa sasa Mathayo ni Mbunge na Obeto ana pesa ba ndiye kiongozi wa CCM kama inavyo semwa .

Ukisha kuwa mwana CCM uko juu ya sheria hata ukiua hakuna wa kukugusa .

Asante mkuu Lunyungu. Hii habari si rahisi kuimeza
Kuna mtu alijitapa hapa kuwa JK yuko hapa jamvini namnukuu "tena JK ni bonge ya critic". Ninapata wasiwasi kama JK atakuwa ndio huyu huyu Rais wa Tanzania, Amirijeshi Mkuu na pia na Mwenyekiti wa CCM Taifa yuko hapa jamvini na anasoma haya halafu miaka imepita bado kawakumbatia hawa watu. Huyo Mathayo wakati wa uchaguzi Tarime gari yake ilikutwa na nini? Hoja hii ilijadiliwa, kwa kuwa ni mwanaCCM, he is above the law na hoja imesahaulishwa tayari.
Kama JK yuko hapa jamvini au watu wake wako hapa na habari kama hii ambayo ina ukweli, na bado watu wanapeta, naungana na wakuu wanaomini nchi hii haina serikali!
 
Any lesson ???

There is a very vivid lesson here, Mkuu Kichuguu, chama chochote kinaanzishwa kwa malengo maalum na kinaji-identify na msimamo unaowanufaisha wanachama wake.
Kwa sasa hivi CCM kinamgogoro kubwa wa Itikadi na mwelekeo wa sera zake.Kimsingi kimekuwa tu ni chama tawala lakini itikadi yake haijulikani maana hakuna anayeizungumzia.
Kama Itikadi ingeeleweka hao matajiri wasingekuwa prominent katika chama.Na kwa vyovyote vile wangeeguliwa na wanachama wenyewe.
Msimamo wa CCM haueleweki, mwelekeo wake si dhahiri,viongozi wake wengi hawaitetei ile itikadi yake ya siku nyingi na si ajabu kuwa sasa ndio hao mafisadi wakubwa.
Zaidi ya kukaribisha wafanyabiashara ambao wengi wanakitumia chama hicho kwa kuficha ufisadi wao, CCM inakosa waandaaji wa sera zenye mvuto na ambazo zinazotekelezeka.
 
Ni kweli kuna viongozi ambao ni majambazi wa kuiba kwa silaha. Polisi wanawafahamu baadhi yao. Kwa mfano, walikuwa wanafahamu kiongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM Arusha, Justine Nyari ni jangili, lakini waliogopa kumkamata mpaka alipowaruhusu BWM. Hata hivyo, Lowasa alimtoa baadaye.

Kuna viongozi wengine ambao ni wezi hatari zaidi: Wanaiba sehemu kubwa ya fedha za bajeti kwa udaganyifu. Kwa mfano, mwaka huu wa fedha ELIMU "imetengewa" zaidi ya shilingi trilioni moja. Lakini hakuna independent verification ya kiasi kinachotumika kweli. Kuna ushahidi wa miaka iliyopita unaoonyesha fedha kama hizo huchukuliwa na kutumika vingine.

Kuna mwana JF mmoja wa Jikoni alifunua kwamba kipindi cha bajeti ya kwanza ya Zakia Meghji, zaidi ya nusu ya bajeti yote ilibaki Hazina.

Hakuna kitakachoenda hadi CCM ikae benji kwanza. Juhudi zote nyingine ni za kujidanganya tu.
 
Mkuu ukisema CCM iko sawa ila baadhi ya wana CCM hawapo sawa inakuwa vigumu kuingia akilini. CMM ni wana CCM na sio bendera tu au majengo. Ukisikia kiongozi wa CCM ni fisadi, CCM haiwezi kukwepa, ni sawa na kusema mimi msafi ila mkono wangu mchafu. Hao hao wana CCM wakifanya jambo zuri wanasema ni CCM, inapaswa kuwa hivyo hivyo hata wakifanya jambo baya.
Ni vizuri kama tukikubali matatizo ya chama yanayosababishwa na kuuza uongozi. Siasa siku hizi imekuwa dili, ni njia ya kujitajirisha lakini inabidi ujanja sana, watanzania ni kama wameanza kuamka, kwa hiyo wanaanza kutambua kuwa wengine ni wezi tu sio viongozi.

Bongolander, Hii nchi imeoza mimi ni mmojawapo wa kuamini kuwa hii nchi haiwezi kusafishwa na CCM, Chadema au chama chochote cha siasa. Mimi ninaamini kuwa hii nchi itasafishwa tu na jeshi la wananchi wa TZ.

Kwanza inatakiwa waliojilimbikizia mali zirudi kwa wananchi, sababu kubwa itakaofanya hata vyama vya upinzani zifeli ni hilo. Kuna watu binafsi wana hela za kutisha wana uwezo hata wa kuiyumbisha serikali. Namna pekee ya ku deal nao ni kuwanyang'anya mali ndo unaleta heshima na adabu.

Zaidi ya hilo hata aje BARAKA HUSSENI OBAMA bado atashindwa hii nchi.
 
Fairplayer,
Hata jeshi siamini linaweza kuisafisha nchi hii. Corruption imeshatinga mizizi huko na pia katika UWT. Kitu kingine kinchotisha kuhusu jeshi ni mfano wa Nigeria. Hawa wakishaingia mamlakani hawataondoka.
 
Bongolander, Hii nchi imeoza mimi ni mmojawapo wa kuamini kuwa hii nchi haiwezi kusafishwa na CCM, Chadema au chama chochote cha siasa. Mimi ninaamini kuwa hii nchi itasafishwa tu na jeshi la wananchi wa TZ.

Kwanza inatakiwa waliojilimbikizia mali zirudi kwa wananchi, sababu kubwa itakaofanya hata vyama vya upinzani zifeli ni hilo. Kuna watu binafsi wana hela za kutisha wana uwezo hata wa kuiyumbisha serikali. Namna pekee ya ku deal nao ni kuwanyang'anya mali ndo unaleta heshima na adabu.

Zaidi ya hilo hata aje BARAKA HUSSENI OBAMA bado atashindwa hii nchi.

Mkuu kuamini ni JWTZ pekee ndio wanaoweza kuisafisha nchi hii ni makosa makubwa kwa sababu hata ndani ya JWTZ kwenyewe ni wizi mtupu unaoendelea kuanzia kwenye ajira mpaka maeneo nyeti.

Ukitaka kujua kiwango cha ufisadi ndani ya JWTZ nenda Mwanza airport siku ambapo kuna usafiri wa ndege ya Jeshi kwenda Dar. Utashuhudia jinsi kuanzia Private hadi Makepteni wanavyopigana vikumbo kutaka kila mtu apakie abiria wake kwenye ndege kwa viwango tofauti kuanzia Elfu hamsini hadi kilo.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom