Kumbe Madaktari ndo wanaongoza kwa mishahara Mikubwa?

Marumeso

JF-Expert Member
Oct 3, 2009
1,410
1,313
Hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Afya Dkt. Mponda wakati akiongea na media jana tar 26. By the way hivi malipo ya wenzetu hawa yakoje?

Tuwekane wazi wadau.
 
kwa ngazi yangu ya degree take home ni kama laki 6 elfu 80000......hivi wa tra au bot wanakula ngapi mpaka waseme siye Ndo tuna mishahara mikubwa?
 
Wabunge ndo wanaongoza kwa kulipwa Mishahara midogo na Posho ndogo.
 
tatizo ni siasa imengilia kila kitu...huyo mponda kasema hayo ili watanzania waone daktari ana mshahara mkubwa saaana.... Mbona na yeye hasemi wake?
 
Kuna TANAPA, form four leaver mshahara wake zaidi ya laki 5, zaidi ya Mwalimu mwenye shahada
 
Tatizo si mishahara mikubwa,madr wanadai malimbikizo ya 'duty/call allowance' ambayo hawajayapata kwa zaidi ya miezi 4 sasa.
 
Tuwekeni sawa jamani juu ya madai ya hawa wapiganaji wenzetu, kwa nchi kama ya kwetu naamini hatuna sababu ya kutoa madai yetu kwa kulinganisha na nchi za watu (Benchmark yetu ni humuhumu ndani ya nchi) Daktari analipwa mshahara shs....ngapi? na hizo call allowance kama stahili ni shs ngapi? na wagonjwa ninachojua tunalipa gharama ya kumwona daktari (consultation fees) kwa hosptali zetu za rufaa shs 15,000/=sijui daktari anaipataje hii. Pili nigependa katika hili tujue TRA wanalipwa vipi?, BOT, Wabunge, na nafikiri hatuhitaji kuwa na gepu kubwa sana katika vipato vyetu.
 
Tatizo si mishahara mikubwa,madr wanadai malimbikizo ya 'duty/call allowance' ambayo hawajayapata kwa zaidi ya miezi 4 sasa.

Hili jipya sasa! Ndo kwanza nalisikia. Nshakuwa mzee mara hii?
 
Tatizo si mishahara mikubwa,madr wanadai malimbikizo ya 'duty/call allowance' ambayo hawajayapata kwa zaidi ya miezi 4 sasa.

kwa hiyo wanatupozea na kudai wanadai mishahara zaidi? ...... CCM kiboko kwa kuhamisha mjadala
 
Hii nchi imekaa muda mrefu katika ombwe la uongozi sasa inalekea kukata roho,

Hivi kweli hawana hata haya kusema kuwa daktari anapata mshahara mshara mkubwa wakati anazidiwa na wafagiaji wa baadhi ya taasis?

Halafu wamesahau kuwa wanasiasa wanalipwa mishahara isiyokatwa kodi wakati daktari analipa kodi hadi asilimia 30%? Yaani daktari bingwa mwenye mshara wa 3mil analipa kodi ya karibia laki 9, wakati mbunge anakomba karibia 9mil bila kodi yoyote. Na kama Mbunge naye angelipa kodi, ingekuwa ni shs 2.7mil karibia sawa na mshahara wa daktari bingwa!!
 
hivi mbayuwayu yupo nchini...

Yuko Ulaya anatembeza bakuli, sikutegemea angeondoka na kuacha nchi katika hali hii. Msiba wa Sheikh Yahaya alikatisha safari kuja kushiriki. Madaktari wana mgomo, wagonjwa wanakufa, anaenjoy wine huko.
 
Back
Top Bottom