Kumbe kutekeleza ahadi kazi: Mjane wa Mwangosi alia na Slaa

Status
Not open for further replies.
Mkuu naona leo gazeti limeamka vibaya na Dr Slaa na inawezekana, sina uhakika kuna msukumo wa kisiasa nyuma yake.

Halafu mbona habari yenyewe inatoka ktk magazeti ambayo ni ant Chadema tu ?

Kwanza ungetuambia hiyo ahadi aliyoitoa tarehe yake ya mwisho --dead line ni lini ndio tupande msingi wa kumtuhumu Dr Slaa. Bila hilo hatuna haki hiyo. Unajuaje kama amepanga kutimiza ahadi hiyo mwezi Nov 2012?

HabariLeo ni gazeti dada la Uhuru! Mwandishi wa hizi Babari ni mlevi wa Wanzuki aliyekubuu! CCM inajiokoteza vijikashfa vya kuwachafua viongozi wa CHADEMA!
 
Nawakumbusha kuna waziri fulani anayeyokea mbeya alisema na yeye atasomesha watoto wa marehemu sasa huyo mama ili ujie anatumika kisiasa nw kama watoto hawajakwenda shule mbona hakumtaja huyo waziri na akarukia kwa dr he he amakweli nimeamini tanzania kuendelea ni kazi vyombo vya habari vimekalia mipasho tu, well kunamambo mengi ya msingi ya kuandika naona mtumie muda mwingi kuongelea ziwa Malawi linavyo taka kuporwa ili watu wa fahamu hilo na si mipasho

Acha uvivu wa kusoma habari yote, soma ndo utajua huyo waziri uliyeshindwa kumtaji ambae ni Mwandosya.amefikia wapi na ahadi yake.
 
Naunganisha na Signature yako "CCM na CDM vyote ni vyama vya siasa vinavyoongozwa na wanasiasa; tofauti yao kubwa ni moja kwamba kimoja kina dola kingine kinataka kushika dola."... Sasa swali je unaweza kuwa na chama cha kisiasa ambacho hakiongozwi na wanasiasa? tutakiitaje?

Hoja ya Mungi ni kuwa unafahamu ahadi ya Dr Slaa? Kama jibu ndio aliahidi nini? na Mjane wa Mwangosi anadai nini? Kuna uhusiano wa ahadi ya Dr na madai ya mjane? From there sasa tunakuwa kwenye position ya kuhukumu as Great Thinkers who dares to talk openly.

Mkuu mimi nimetoa taarifa niliyoisikia kwamba mke wa mwangosi analalama. Sikujishughulisha na ahadi gani alitoa. Nilisikia ahdi nyingi tu mara Prof. Mwandosya kuwasomesha watoto mara Dr. Slaa naye sijui ahadi gani. Ahadi zilikuwa lukuki na zinaendelea kutoka kwa wanasiasa. Nimesikia Zitto naye katoa ahadi nyingine.
 
Nimesikia kupitia uchambuzi wa magazeti kwamba Mjane wa Marehemu Daud Mwangosi analilia rambirambi alizoahidiwa na Dr. Slaa kwenye msiba wa mme wake. Anwalilia waandishi wamsaidie kupata hizo rambirambi toka kwa Dr. Slaa.

Kumbe kutekeleza ahadi kazi kweli kweli!

============

.

Dr. Slaa aliahidi yafuatayo... Aliahidi kusomesha mtoto wa Mwangosi, na sio kutoa rambi rambi !!
Acheni unafiki wa kutafuta umaarufu kwa bei ya chini sana kwa kuweka post kama hizi.
Ukinukuu uozo, na wewe utahusishwa kwenye uozo huo huo !!

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema watabeba jukumu la kumsomesha mtoto wa kwanza wa Mwangosi aitwae Nehemiah, ambaye kwa sasa yupo kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Malangali iliyopo Mufindi, mkoani Iringa.

“Mtoto huyu alifika na kutaka kujua sababu za kifo cha baba yake kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nimewasiliana na mdau wangu na kuahidi kubeba kujumu la kumsomesha na pia naahidi kufuatilia ahadi hiyo kwa kipindi chote cha masomo yake,” alisema Dk. Slaa.

Source:
http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=45474
 
"Mtoto huyu alifika na kutaka kujua sababu za kifo cha baba yake kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nimewasiliana na mdau wangu na kuahidi kubeba kujumu la kumsomesha na pia naahidi kufuatilia ahadi hiyo kwa kipindi chote cha masomo yake," alisema Dk. Slaa.

Source:
http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=45474

Mkuu,
Post yako imesema kila kitu. Ina maana huyo Nehemiah anadaiwa ada hapo Malangali ambapo ataanza mitihani yake ya mwisho kuanzia Jumatatu (08/10/2012)?

Mi hata sielewi. Maggid Mjengwa, tafadhali tusaidie hii issue imekaaje especially content na context
 
Maggid Mjengwa, ukijibu utupe taarifa kwanza je rambirambi umekwisha ziwasilisha? Isiwe kama huyo mwenzako.
 
Hivi Rambirambi ni deni? Mbona inakuwa kazi?

rambi rambi ni ahadi na ahadi ni deni.
Nani aliwatuma kuahidi wasicho weza kutekeleza?

Kumbe yule mama wa arusha analaumiwa bure.
Wanasiasa wa ni walewale tu, hakuna jipya.
 
Ahadi ni deni wampe rambirambi zake.!!

JF inageuka kuwa forum ya Low Thinkers !!

Napendekeza kuanzishwe forum ya Low Thinkers hapa JF !! (kwa ajili ya watu kama wewe) !!

hebu soma hapa kuhusu ahadi za Dr. Slaa....

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema watabeba jukumu la kumsomesha mtoto wa kwanza wa Mwangosi aitwae Nehemiah, ambaye kwa sasa yupo kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Malangali iliyopo Mufindi, mkoani Iringa.

“Mtoto huyu alifika na kutaka kujua sababu za kifo cha baba yake kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nimewasiliana na mdau wangu na kuahidi kubeba kujumu la kumsomesha na pia naahidi kufuatilia ahadi hiyo kwa kipindi chote cha masomo yake,” alisema Dk. Slaa.

Source: Home
 
Dr Slaa aliahidi kuwasomesha watoto! Sasa msiba umeisha juzi tu, leo ameanza kulia. Au alifikiri atapewa hela!? Huu ni uchuro!

Mkuu Filipo, Gazeti Habari Leo, waleta thread Kimbunga na WOWOWO; Kwa vyovyote vile masaburi ya Magamba yanapumua kuchafua hali ya hewa humu jf.
 
Hz ndo siasa za uongooo yani hata aibu huoni dr slaa kwahiyo siku ile ilikuwa unataft cheap popularty ee!!
 
Nawakumbusha kuna waziri fulani anayeyokea mbeya alisema na yeye atasomesha watoto wa marehemu sasa huyo mama ili ujie anatumika kisiasa nw kama watoto hawajakwenda shule mbona hakumtaja huyo waziri na akarukia kwa dr he he amakweli nimeamini tanzania kuendelea ni kazi vyombo vya habari vimekalia mipasho tu, well kunamambo mengi ya msingi ya kuandika naona mtumie muda mwingi kuongelea ziwa Malawi linavyo taka kuporwa ili watu wa fahamu hilo na si mipasho

Inawezekana alimtaja huyo pia huenda na wengine zaidi ila mwandishi kaona wa kuuza habari yake ni Dr. Slaa so akaamua kumtumia katika habari yake.
 
Nimesikia kupitia uchambuzi wa magazeti kwamba Mjane wa Marehemu Daud Mwangosi analilia rambirambi alizoahidiwa na Dr. Slaa kwenye msiba wa mme wake. Anwalilia waandishi wamsaidie kupata hizo rambirambi toka kwa Dr. Slaa.

Kumbe kutekeleza ahadi kazi kweli kweli!

============

Mjane wa Mwangosi alilia rambirambi za Slaa

HabariLeo | Oktoba 05, 2012

UTAMADUNI mpya wa siasa za misibani, unaoendana na mauaji yaliyotokana na ukaidi wa wanasiasa kwa Jeshi la Polisi, umeanza kuiumbua Chadema ambayo imejikuta ikishindwa kutimiza ahadi ndogo ndogo za kutoa rambirambi inazoahidi kwa wafiwa.

Juzi, mjane wa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, Aneti, alijikuta akiomba wanahabari wasaidie kufuatilia rambirambi iliyoahidiwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kutokana na kiongozi huyo, kukata mawasiliano baada ya msiba.

“Nina mawasiliano na Profesa Mark Mwandosya ambaye pia aliahidi kumsomesha mtoto mmoja, yeye aliniambia nitakapokuwa tayari nimjulishe ili atume fedha kwenye akaunti ya shule, lakini sina mawasiliano na Dk Slaa,” alisema Aneti.

Mwangosi aliuawa Septemba 2 mwaka huu, kwa kupigwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Aliuawa wakati Polisi ikizuia wafuasi na viongozi wa Chadema kufanya mikutano ya hadhara ambayo ilipigwa marufuku ili kuruhusu shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi, kufanyika bila kuingiliwa.

Baada ya mauaji hayo, wakati wa maziko ya mwandishi huyo, Dk Slaa aliahidi kubeba jukumu la kusomesha mtoto wa kwanza wa Mwangosi aitwaye Nehemiah, ambaye yuko kidato cha nne katika Sekondari ya Malangali, Mufindi, Iringa.

“Mtoto huyu alifika na kutaka kujua sababu za kifo cha baba yake, kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nimewasiliana na mdau wangu na kuahidi kubeba jukumu la kumsomesha na pia naahidi kufuatilia ahadi hiyo kwa kipindi chote cha masomo yake,” alinukuliwa Dk Slaa akiahidi.

Hata hivyo ahadi hiyo, mbali na ukweli kuwa haijatekelezwa, lakini pia hata mawasiliano kati yake na mjane wa Mwangosi hayapo mpaka mjane huyo kuamua kuomba waandishi wamfuatilie.

Mwingine aliyeahidi kusaidia familia hiyo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mwandosya, ambaye aliiwakilisha Serikali na katika salamu zake za rambimbambi msibani, alisema atabeba jukumu la kusomesha watoto wengine wa marehemu huyo.

Aliahidi pia kufuatilia ahadi za watu wengine katika kuisaidia familia ya Mwangosi kwa kuwa ni ndugu yake na jirani. “Nitahakikisha familia hii inaishi maisha kama ambavyo angelikuwapo baba yao kwa kuhakikisha kila mtoto wa familia hiyo anasoma kwa kila hatua kwa kuzingatia kuwa hao ni sehemu ya familia yangu,” alisema Mwandosya, ambaye pia ni Mbunge wa Rungwe Mashariki (CCM).

Gazeti hili lilipompigia Dk Slaa simu kujua mipango yake ya kutekeleza ahadi hiyo, simu yake ilikuwa inaita mara zote bila kupokewa.

Rambirambi zingine Wakati huo huo, wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Iringa, wametoa rambirambi zao kwa mjane huyo. Mhasibu Mkuu wa Tanroads Iringa, Alex Mgeta alikabidhi Sh 265,000 juzi katika nyumba yao iliyopo Kihesa Bwawani mjini hapa.

“Nashukuru sana lakini pia nawaomba kwa kupitia michango ambayo nimeambiwa inaendelea kukusanywa mnisaidie nimalizie nyumba hii,” alisema Aneti.

Aneti alisema nyumba hiyo yenye vyumba vinne vya kulala haijakamilika na ikikamilika, atapangisha baadhi ili kiasi cha fedha atakachopata kitumike kuendesha familia yake.

Septemba 30 katika harambee iliyofanyika Iringa kwa mujibu wa blogu ya Mjengwa, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto alijitolea kumchangia mjane huyo kwa kumlipia ada ya uanachama wa Bima ya Afya kila mwezi kwa miaka mitatu mfululizo.

Alikaririwa akisema: "Nimeona nami niunge mkono harambee hii. Pamoja na michango ya fedha iliyotolewa kumsaidia mjane kuanzisha mradi wa kujikimu, naona ni muhimu akawa na uhakika wa huduma ya afya yake na watoto wake wanne. Hivyo, mchango wangu utakuwa ni kwenye eneo hilo la Bima ya Afya kwa miaka mitatu."

Baadhi ya watu wengine maarufu waliojitokeza kumchangia mjane kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com ni pamoja na Shy-Rose Bhanji, Ananilea Nkya, John Bukuku na Mobhare Matinyi aliyepata kuwa Mhariri wa Majira.

we msandiki kweli kweli, CDM walikuwa wanafanya mikutano ya hadhara au walikuwa wanafunguwa matawi? na ahadi aliyotoa ni ya pesa au ni ile ya kusomesha watoto?
 
Huyo mama, kalia baada ya Slaa kukata mawasiliano na ni baada ya kutoa ahadi hewa!
 
============ [COLOR=#0000ff said:
Mjane wa Mwangosi alilia rambirambi za Slaa[/COLOR]

HabariLeo | Oktoba 05, 2012

UTAMADUNI mpya wa siasa za misibani, unaoendana na mauaji yaliyotokana na ukaidi wa wanasiasa kwa Jeshi la Polisi, umeanza kuiumbua Chadema ambayo imejikuta ikishindwa kutimiza ahadi ndogo ndogo za kutoa rambirambi inazoahidi kwa wafiwa.

Juzi, mjane wa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, Aneti, alijikuta akiomba wanahabari wasaidie kufuatilia rambirambi iliyoahidiwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kutokana na kiongozi huyo, kukata mawasiliano baada ya msiba.

Baada ya mauaji hayo, wakati wa maziko ya mwandishi huyo, Dk Slaa aliahidi kubeba jukumu la kusomesha mtoto wa kwanza wa Mwangosi aitwaye Nehemiah, ambaye yuko kidato cha nne katika Sekondari ya Malangali, Mufindi, Iringa.

"Mtoto huyu alifika na kutaka kujua sababu za kifo cha baba yake, kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nimewasiliana na mdau wangu na kuahidi kubeba jukumu la kumsomesha na pia naahidi kufuatilia ahadi hiyo kwa kipindi chote cha masomo yake," alinukuliwa Dk Slaa akiahidi.

Ni aibu kwa gazeti linalolipwa kwa kodi zetu kuandika udaku kama huu. Kwanza katika paragraph ya kwanza tu tayari wanahukumu kesi ambayo ipo mahakamani na kuna upashkuna mwingi tu hapo. Sijui Uwazi Risasi nk ziandike maana utadhani ni habari za kina Wema na Lulu.

Kwa msomaji makini hebu ona contradictions zinazojitokeza katika page zinazofuata. Shame upon them. Unaweza tu kuwahukumu kwa habari hii hii waliyoandika wenyewe kwani huhitaji ushahidi wa nje ya hapo maana ukweli wa alichokisema Dr. Slaa pia wameuweka hapa. Nadhani watakuwa wamefundishwa kusema/kuandika uongo na Kova. Kusema uongo unahitaji kuwa smart sana. Shame kwa mhariri na mwandishi wake kutuletea upashkunata kwenye chombo kinachogharamiwa na fedha za umma!

Mtoto yuko form IV na anaanza mitihani jumatatu ijayo... hivyo ni wazi ada ya mwaka huu ilikwishalipwa. Kama sivyo Mwandishi huyu ninayemuona ni boonge la uchwara alikwenda shuleni na kuambiwa mtoto anadaiwa ndipo aje aandike utumbafu? Kwani ni lazima uhuru na Habari leo yaandike taarifa za kupika kuhusu CHADEMA kila siku? kwanini wasipumzike kama hawani kuni za kutosha kupika taarifa zao?
 
Kama ahadi ya mtu mmoja anashindwa kuitimiza je ya watanzania millioni arobaini ataiweza?

Ahadi gani ??
Hapa JF kuna ugonjwa wa watu kuwa wavivu kutafuta ukweli.
Leo hii mtu anaweza kuweka thread na kusema jambo lolote lile na watu wakaamini na kuanza kuchangia !!
Unaweza kusema kuwa:-
' ..Kikwete kakimbia nchi ..' - Watu wataamini na kuanza kuchangia 'hoja' !!
Sishangai kama gazeti moja likiandika habari yoyote na watu wakaamini na kuanza kuchangia 'hoja'.!!

Guys, kuweni great thinkers !! Chunguza kwanza ukweli wa habari yenyewe ndio uanze kuchangia !!

Kwa mfano wewe Tony Almeda umechangia bila kutafuta ukweli.
Sasa angalia ukweli huu, kisha uanze upya kuchangia ....

Dr. Slaa aliahidi yafuatayo ....

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema watabeba jukumu la kumsomesha mtoto wa kwanza wa Mwangosi aitwae Nehemiah, ambaye kwa sasa yupo kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Malangali iliyopo Mufindi, mkoani Iringa.

“Mtoto huyu alifika na kutaka kujua sababu za kifo cha baba yake kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nimewasiliana na mdau wangu na kuahidi kubeba kujumu la kumsomesha na pia naahidi kufuatilia ahadi hiyo kwa kipindi chote cha masomo yake,” alisema Dk. Slaa.

Umeona ahadi ya Slaa ??

Aliahidi kusomesha mtoto wa Mwangosi, Hakuahidi kutoa rambi-rambi !!!!
Jiulize, je ameshindwa, au amaingia mitini kumsomesha huyo mtoto ??

Umeona ???
Sasa anza upya kuchangia !!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom