Kumbe kutekeleza ahadi kazi: Mjane wa Mwangosi alia na Slaa

Status
Not open for further replies.
Tuwe wakweli! Kama Dr. aliahidi kusomesha watoto unataka upewe fyeza ili iweje? Njaa zingine bwana! Je kuna mtoto wake amefukuzwa shule kwa kukosa ada? Huyu mjane naye asigeuze msiba wa mme wake kuwa mtaji bana!
 
Sito uliza umri

AIBU aibu watu kupenda Makamera, maflash na kukaa nyuma ya vinasa sauti mradi uonekane mwenye uchungu kumbe Siasa tu
Hakuna haja ya kutoa ahadi ww toa pole tutakuona
 
Kwani hao watoto/mtoto alikuwa anadaiwa ada ya shule wakati Marehemu yupo hai?
Maana sielewi kwa nini alie badala ya kukaa chini na kumwombea Dr Slaa baraka.

Kwani alimwambia lini atamsomesha? Huyo mtoto yupo nyumbani hana shule? Si amepokea pesa juzi kama kweli anadhamini na anahitaji mtoto aende shule si atumie hizo?

Anataka apewe pesa then atie mfukoni pia? Dr Slaa labda anashughulikia plan ya kusaidiaje, labda kufungua acoount ya pesa zitoke humo direct kwenda shule hapo baadae.

Ok nisaidieni kujua, huyo mtoto haendi shule now? Kwani ni makosa Dr kutaka saidia? Mie nilivyosomaga niliamini ni baadae labda from next year ndo atasaidia au baadae zaidi. Wewe mama hii inakuvunjia heshima as wengine watakimbia kukupa ahadi. Kama kuna mtu mwingine kasema atakusaidia basi usitumie kuharibia Chadema kuongoza.

Umeshindwa kumtafuta simuni kama una shida?

Hapo kwenye red, nimejiuliza hapa, mbona inazungumzwa ahadi ya Dr. Slaa tu. Huyo mama ameshapewa ahadi aliyoahidi Mwandosya? Mbona nae aliahidi kumsomesha mtoto mmoja? Ndio maana nasema anatumia kisiasa!
 
Nimesikia kupitia uchambuzi wa magazeti kwamba Mjane wa Marehemu Daud Mwangosi analilia rambirambi alizoahidiwa na Dr. Slaa kwenye msiba wa mme wake. Anwalilia waandishi wamsaidie kupata hizo rambirambi toka kwa Dr. Slaa.

Kumbe kutekeleza ahadi kazi kweli kweli!

Source ya habari hii ni gazeti la HABARI LEO! Sisi CHADEMA hatuliamini kama chanzo cha kuaminika cha habari!
 
Kama ahadi ya mtu mmoja anashindwa kuitimiza je ya watanzania millioni arobaini ataiweza?
Kitu chochote ambacho si hulka yako kukifanya inakuwa shida,Dr Slaa hana tabia ya kuhudhuria misiba na kutoa rambirambi kwa wafiwa msimlaumu wana JF.

 
Walizichakachuaje picha za CUF Arusha? yaani cuf ilikuwa na watu wachace wao wakaonyesha wengi? au ilikuwa na watu wengi wao wakaonyesha wachache? vyote hivyo ni kuchakachua.na au hawakuonyesha kabisa,kama ndivyo ni blog gani walifanya vizuri kwenye tukio la cuf arusha??

waliweka picha za maandamano ya cuf wakimsindikiza Lipumba kuchukua fomu ya kugombea urais August mwaka 2010 wakasema ni maandamano ya cuf yaliyofanyika juzi Arusha!
 
Mi mwenyewe nimeona hii habar kwenye Habari Leo, but I really dont belive that huyu mama ameenda kulia gazetin. Nadhan Habari Leo has fabricated the story.
 
Katika gazeti la Habari Leo toleo la leo Tar. 05/10/2012 kuna habari inayomnukuu mjane wa Marehemu Mwangosi akimlaumu Dkt. Slaa na CDM kuwa ameshindwa kutimiza ahadi yake ya rambirambi na hata msaada wake wa kusomesha mmoja wa mtoto wa Marehemu Mwangosi.

Mjane huyo analalamika kuwa toka Dkt. Slaa aondoke Iringa hajawahi kuwasiliana na Mjane huyo.

My Take;
-Naona Mjane huyu sasa anatumika kisiasa zaidi maana hata Habari hiyo ya Habari Leo kwa kweli imeandikwa kishabiki na kisiasa sana.
- Kama ni kweli kwa anachokisema (Ingawa si ustaarabu wala jadi kulalama na rambirambi za misiba) ni vema Dkt. Slaa na CDM wakalitolea ufafanuzi kwani linaleta picha mbaya sana hasa ikizingatiwa Marehemu aliuawa na Polisi akiwa kwenye shughuli za CDM.
 
Hayo magazeti hayauziki ndio maana wamegunduwa mbinu mpya ya kuitaja cdm ili yaauzike
 
Mmmh kwahiyo hizo 5M toka kwa Sabodo, alishazipata huyu Mama au bado hazijamfikia?

Swali jengine la kujiuliza baada ya kuhamia CUF bado anastahili kupewa,zitarudishwa kwa Sabodo au ndio kilichoenda kwa mganga hakirudi.
 
Ahadi kazi kweli
kutekeleza..hata juzi kule Arusha kuna mjane wa marehemu aliyafariki
kwenya vurugu za Arusha alililamika kwenye mkutano wa CUF kwamba ahadi
alizoahidiwa na baadhi ya wanasiasa hazikutimizwa..sumu ya siasa ni
ahadi za jazba!!!zinaweza zikakuvunjia heshmaa

huyu mama ndo hamna kitu kukimbilia CUF ndo ufumbuzi wa kupatikana kwa hizo ahadi au ndo kurudia kosa?
 
Soma vizuri post yangu!

Post yako yasema "Mjane alikiri kupokea 5m, na akasema viongozi wa CDM walimtafuta lkn alikuwa Tanga hivyo hawakumpata. Tangu arudi Arusha amekuwa akiwatafuta bila mafanikio"

Sasa kitu ambacho mie sijaelewa hapa ni kwamba kama alikiri kupokea 5m manake imemfikia hata baada ya kuikamata ndio mtu waeza sema nakiri kupokea, sasa hapo kwenye muendelezo wa maelezo hayo ndio yaliponichanganya hata nashindwa kuconnect dots za line ya kwanza na zinginezo"
 
Mkuu mheshimiwa sana Kimbunga, imekuwaje mpaka unapost thread isiyo na mashiko? Hata msiba umekuwa siasa?
Ungeelezea Dr. Slaa aliahidi nini, manake kama ni kumsomesha mtoto huwezi kukurupuka hivyo bana!
Mkuu Mungi mimi nimesikia tu kwenye magazeti mjane akipiga mayowe. Mkuu ule msiba mimi naona kama ulifanywa wa kisiasa. Siku hizi Tanzania tunageuka taratibu kuwa kama wakenya. Wakenya siasa ni kila mahala iwe msibani, kanisani ama smikitini ni siasa kwa kwenda mbele. Msiba wa mwangosi ulifanywa wa kisiasa na matokeo yake ndiyo hayo yanakuwa ya kisiasa.

Nimesikia tena ati Zitto Kabwe ametoa ahadi ya kumpatia mjane wa Marehemu Mwangosi huduma za afya kwa miaka miwili! Ahadi nyingine ya kisiasa toka kwa mwansiasa.
 
Last edited by a moderator:
Aliahidi kumsomesha mtoto, yeye amepeleka taarifa yeyote juu ya hiyo shule ya mtoto? aache kulalamika atimize wajibu wake pia

Nimesikia kupitia uchambuzi wa magazeti kwamba Mjane wa Marehemu Daud Mwangosi analilia rambirambi alizoahidiwa na Dr. Slaa kwenye msiba wa mme wake. Anwalilia waandishi wamsaidie kupata hizo rambirambi toka kwa Dr. Slaa.

Kumbe kutekeleza ahadi kazi kweli kweli!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom