Kumbe kutekeleza ahadi kazi: Mjane wa Mwangosi alia na Slaa

Status
Not open for further replies.
Bwana Kimbunga basi ukasikia tu kwenye uchambuzi wa magezeti,kabla hata hujalisoma hilo gazeti ukajua kilichomo ndani kwa kirefu ukaja na thread "Kumbe kutekeleza ahadi kazi: Mjane wa Mwangosi alia na Slaa". Aisee!
Pamoja na kuwa gazeti lenyewe ni "Habari leo", ukisoma bado huwezi onesha mahali ambapo mjane wa watu "anamlilia" Dr. Slaa; hakuna mahali panapoonesha kuwa wengine wote walioahidi wamekwishatekeleza; hakuna mahala popote panapoonesha kuwa ahadi ya Dr. Slaa ni overdew labda na mtoto amefukuzwa shule au amepitiliza umri wa kwenda shule; hakuna mahala popote inapoonesha mjane alijaribu kutafuta mawasiliano na Dr. Slaa bila mafanikio (Seriously kwa nafasi yake mjane asingeshindwa kupata kitu so "public" kama namba ya ktibu mkuu taifa wa chama kama CHADEMA!).
Nisingeshangazwa kama thread ingeanzishwa na hawa jamaa wengine hawa akina Ritz and co. But you Kimbunga ...? Too low broda!!
 
Last edited by a moderator:
Ahadi ni deni na miongoni mwa mambo yanayomfanya mtu kuingia kwenye kundi la unafiki ni kutotimiza ahadi, kuaminiwa ukafanya hiana pamoja na kusema uongo, cdm wapo kwenye kipindi cha kujiimalisha na wapenda mabadiliko wengi wana imani kubwa juu yao hivyo wawe makini na mambo yanayogusa hisia za wapenda haki wengi..

Nakumbuka chama kiliahidi laki 5 na kusomesha kijana mmoja kama hazijatekelezwa basi cdm itumie vizuri fursa hii ya ukumbusho kutekeleza hilo.


...Nakubaliana nawe Mkuu, lakini je kuna muda maalumu umepangwa kwa Ahadi kuonekana ni Hewa na Haijatimizwa?? Imeishapita Miezi Mingapi baada ya Dr Slaa Kutoa Ahadi yake hadi Ionekane kuwa Hajaitimiza?? Huyu mama aangalie sana asije akaanza kutumika Kisiasa...!

 
Nimesikia kupitia uchambuzi wa magazeti kwamba Mjane wa Marehemu Daud Mwangosi analilia rambirambi alizoahidiwa na Dr. Slaa kwenye msiba wa mme wake. Anwalilia waandishi wamsaidie kupata hizo rambirambi toka kwa Dr. Slaa.

Kumbe kutekeleza ahadi kazi kweli kweli!

============

Mjane wa Mwangosi alilia rambirambi za Slaa

HabariLeo | Oktoba 05, 2012

UTAMADUNI mpya wa siasa za misibani, unaoendana na mauaji yaliyotokana na ukaidi wa wanasiasa kwa Jeshi la Polisi, umeanza kuiumbua Chadema ambayo imejikuta ikishindwa kutimiza ahadi ndogo ndogo za kutoa rambirambi inazoahidi kwa wafiwa.
.
.
.
“Mtoto huyu alifika na kutaka kujua sababu za kifo cha baba yake, kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nimewasiliana na mdau wangu na kuahidi kubeba jukumu la kumsomesha na pia naahidi kufuatilia ahadi hiyo kwa kipindi chote cha masomo yake,” alinukuliwa Dk Slaa akiahidi.

.

Hapo kwenye red,
Mwandishi wa mada hii (Kimbunga) kashindwa kabisa kusoma makala yake mwenyewe na kuona kuwa ina kasoro kubwa sana.
Kakurupuka, kaiweka hapa JF, na sasa anaumbuka kwa kuonyesha udhaifu wa hali ya juu sana wa kufikiri.
Yaani hakuweza kutofautisha kati ya ahadi ya rambi-rambi na ahadi ya kusomesha mtoto !!
Makala inajipinga yenyewe, halafu mwandishi wa mada anaiweka na kuiunga mkono moyoni mwake na kutoa hitimisho (conclusion) la mawazo yake !!
Huyu mwandishi wa mada hii (Kimbunga) naye ni 'Great Thinker' wa JF !! ??
CCM na vijibaraka wake wana kaazi kweli - kweli !!!
 
Mjane wa Mwangosi amekanusha vikali habari zilizochapishwa na gazeti la habari Leo kuwa eti yeye alilia rambirambi za Slaa.akiongea alipokuwa nyumbani kwa kwangu kwa uchungu amesikitishwa sana kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na Kama angukuwa na Shida na Dr Slaa angenitafuta Mimi. kwanza ni jirani yake na pili anajua ukaribu wangu na Dr.anasema kitendo hicho ameamsha Msiba kwani kina lengo la kutaka Jamii imdharau. Anaomba watanzania kuupuza habari hizo na ameshanga ni maadili gani haya ya uwandishi. Naomba kuwasilisha(Nimeitoa kule Facebook kwenye wall ya Msigwa).
 

Attachments

  • iringa.jpg
    iringa.jpg
    131.6 KB · Views: 30
Mkuu mheshimiwa sana Kimbunga, imekuwaje mpaka unapost thread isiyo na mashiko? Hata msiba umekuwa siasa?
Ungeelezea Dr. Slaa aliahidi nini, manake kama ni kumsomesha mtoto huwezi kukurupuka hivyo bana!
Duuh, pole, imekuwaje ukapata BAN? ni ya muda gani?
 
Ahadi ilikuwa ni ya kusomesha watoto. Mjane anachotakiwa ni kusema shule walipo watoto awasiliane na viongozi wa CDM karibu naye. Kwani watoto wamerudishwa nyumbani kwa kukosa ada?? na je ada ya muhula huu haijalipwa???

Hii habari ni ya kisiasa zaidi na sidhani kama lengo lake ni kumsaidia mjane. Wenye shida ni wale watoto waliofiwa na baba yao sio waandishi wa habari mchwara. Ni uongo kusema Dr Slaa hapatikani ni uongo mkubwa sana.

Dr Slaa hajawahi kutoa ahadi ya uongo, sio mwongo na siku zote anasimamia maneno yake. Hakuna siasa za msibani, marehemu alikufa kwenye shughuli ya CDM ni utu wa mwanadamu. Waandishi wa habari walikuwa wakitimiza majukumu yao wakitafuta habari za kisiasa polisi wakaamua kuwawauwa kwa makusudi. Msiba umegusa wengi na hauhusiana na siasa.

Ni kawaida waandishi wa habari kuwepo kwenye matukio mengi, misiba, siasa, vita, sherehe nk na mara nyingi kama kuna hali ya kuhatarisha amani polisi, jeshi nk huwa wanapa ulinzi waandishi. Nimeshuhudia waandishi wakiwahoji boko haramu, waasi wa somalia, taliban, wakiwa vitani na hawauwawi kazi yao ni kukusanya habari na kuripoti. Sasa tujiulize polisi waTanzania wanaogopa nini kisiripotiwe kama kweli walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kuwashughulikia M4C??

Waandishi wa habari mmekuwa target ya polisi halafu leo mnafitinisha watetezi wenu. Leo ni Mwangosi kesho ni mwingine. Mauaji ya waandishi yameanza zamani kumbuka katabalo nk.

Uhuru wa vyombo vya habari ni njia kubwa ya kutuletea maendeleo.

Sauti ya
Chief Mkwawa wa Kalenga
Woga na rushwa ndio inayoangamiza Taifa, Wazelando ni wachache sana.
 
...Nakubaliana nawe Mkuu, lakini je kuna muda maalumu umepangwa kwa Ahadi kuonekana ni Hewa na Haijatimizwa?? Imeishapita Miezi Mingapi baada ya Dr Slaa Kutoa Ahadi yake hadi Ionekane kuwa Hajaitimiza?? Huyu mama aangalie sana asije akaanza kutumika Kisiasa...!


Hilo ndilo swali la msingi na wafitini wetu hawalijibu na hawawezi kulijibu kwa sababu proganda siku zote huwa haina ground ya kuisimamia. Tunawauliza kama kulikuwa na tarehe iliyoahidiwa ni tarehe ngapi basi? Kimya! Sasa tusemeje kama siyo propaganda?
 
Ukiangalia hata uahdishi wa huyu anayejiita Mwendishi Wetu si wa kufuata utalaam maana anatoa hukumu kwa kesi ambayo ndio kwanza inasomwa mahakamani, lakini yeye anasema "unaoendana na mauaji yaliyotokana na ukaidi wa wanasiasa kwa Jeshi la Polisi" anasema mauaji yalitokana na ukaidi kitu ambacho mahakama haijasema hivyo. Halafu paragraph ya kwanza imeandikwa kishambi akitumia maneno "utamaduni wa ahadi za kisiasa" kama vile ahadi imeshindwa kutekelezwa, ametumia neno tena "kuumbua".
Ndiyo maana Dr Slaa aliwambia wazi kuwa halipendi gazeti ili Mhariri wake Joseph Kulangwa akaja juu na hoja uchwara kwamba Dr Slaa hafanyi tafiti. Utahitaji tafifiti gani kujua kuwa gazeti ili ni la kinafiki, hata mtoto wa darasa la kwanza anayejua kusoma atajua kuna unafiki na uzadiki mtupu
 
Angetaja sifa za mtu anayetakiwa kuwa rais wa nchi.
mfano, Padre wa kikatoriki (katoliki) hana sifa za kuwa rais wa nchi, Mchungani wa Kilutheri hana sifa za kuwa rais, Mufti anatakiwa kuwa rais nk.
lukatony anaonekana anajazba sana, ama jina la Dr. Slaa ni hatari kwake na chama chake!

Mbona Alhaj Mwinyi alikuwa Rais hakusema, mbona Alhaj Kiketwe ni Rais, Mbona kuna masheikh na maalhaj wengi ni viongozi wa serikali hatusemi
 
Nimesikia kupitia uchambuzi wa magazeti kwamba Mjane wa Marehemu Daud Mwangosi analilia rambirambi alizoahidiwa na Dr. Slaa kwenye msiba wa mme wake. Anwalilia waandishi wamsaidie kupata hizo rambirambi toka kwa Dr. Slaa.

Kumbe kutekeleza ahadi kazi kweli kweli!

============

Mjane wa Mwangosi alilia rambirambi za Slaa

HabariLeo | Oktoba 05, 2012

UTAMADUNI mpya wa siasa za misibani, unaoendana na mauaji yaliyotokana na ukaidi wa wanasiasa kwa Jeshi la Polisi, umeanza kuiumbua Chadema ambayo imejikuta ikishindwa kutimiza ahadi ndogo ndogo za kutoa rambirambi inazoahidi kwa wafiwa.

Juzi, mjane wa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, Aneti, alijikuta akiomba wanahabari wasaidie kufuatilia rambirambi iliyoahidiwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kutokana na kiongozi huyo, kukata mawasiliano baada ya msiba.

“Nina mawasiliano na Profesa Mark Mwandosya ambaye pia aliahidi kumsomesha mtoto mmoja, yeye aliniambia nitakapokuwa tayari nimjulishe ili atume fedha kwenye akaunti ya shule, lakini sina mawasiliano na Dk Slaa,” alisema Aneti.

Mwangosi aliuawa Septemba 2 mwaka huu, kwa kupigwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Aliuawa wakati Polisi ikizuia wafuasi na viongozi wa Chadema kufanya mikutano ya hadhara ambayo ilipigwa marufuku ili kuruhusu shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi, kufanyika bila kuingiliwa.

Baada ya mauaji hayo, wakati wa maziko ya mwandishi huyo, Dk Slaa aliahidi kubeba jukumu la kusomesha mtoto wa kwanza wa Mwangosi aitwaye Nehemiah, ambaye yuko kidato cha nne katika Sekondari ya Malangali, Mufindi, Iringa.

“Mtoto huyu alifika na kutaka kujua sababu za kifo cha baba yake, kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nimewasiliana na mdau wangu na kuahidi kubeba jukumu la kumsomesha na pia naahidi kufuatilia ahadi hiyo kwa kipindi chote cha masomo yake,” alinukuliwa Dk Slaa akiahidi.

Hata hivyo ahadi hiyo, mbali na ukweli kuwa haijatekelezwa, lakini pia hata mawasiliano kati yake na mjane wa Mwangosi hayapo mpaka mjane huyo kuamua kuomba waandishi wamfuatilie.

Mwingine aliyeahidi kusaidia familia hiyo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mwandosya, ambaye aliiwakilisha Serikali na katika salamu zake za rambimbambi msibani, alisema atabeba jukumu la kusomesha watoto wengine wa marehemu huyo.

Aliahidi pia kufuatilia ahadi za watu wengine katika kuisaidia familia ya Mwangosi kwa kuwa ni ndugu yake na jirani. “Nitahakikisha familia hii inaishi maisha kama ambavyo angelikuwapo baba yao kwa kuhakikisha kila mtoto wa familia hiyo anasoma kwa kila hatua kwa kuzingatia kuwa hao ni sehemu ya familia yangu,” alisema Mwandosya, ambaye pia ni Mbunge wa Rungwe Mashariki (CCM).

Gazeti hili lilipompigia Dk Slaa simu kujua mipango yake ya kutekeleza ahadi hiyo, simu yake ilikuwa inaita mara zote bila kupokewa.

Rambirambi zingine Wakati huo huo, wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Iringa, wametoa rambirambi zao kwa mjane huyo. Mhasibu Mkuu wa Tanroads Iringa, Alex Mgeta alikabidhi Sh 265,000 juzi katika nyumba yao iliyopo Kihesa Bwawani mjini hapa.

“Nashukuru sana lakini pia nawaomba kwa kupitia michango ambayo nimeambiwa inaendelea kukusanywa mnisaidie nimalizie nyumba hii,” alisema Aneti.

Aneti alisema nyumba hiyo yenye vyumba vinne vya kulala haijakamilika na ikikamilika, atapangisha baadhi ili kiasi cha fedha atakachopata kitumike kuendesha familia yake.

Septemba 30 katika harambee iliyofanyika Iringa kwa mujibu wa blogu ya Mjengwa, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto alijitolea kumchangia mjane huyo kwa kumlipia ada ya uanachama wa Bima ya Afya kila mwezi kwa miaka mitatu mfululizo.

Alikaririwa akisema: "Nimeona nami niunge mkono harambee hii. Pamoja na michango ya fedha iliyotolewa kumsaidia mjane kuanzisha mradi wa kujikimu, naona ni muhimu akawa na uhakika wa huduma ya afya yake na watoto wake wanne. Hivyo, mchango wangu utakuwa ni kwenye eneo hilo la Bima ya Afya kwa miaka mitatu."

Baadhi ya watu wengine maarufu waliojitokeza kumchangia mjane kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com ni pamoja na Shy-Rose Bhanji, Ananilea Nkya, John Bukuku na Mobhare Matinyi aliyepata kuwa Mhariri wa Majira.

Habari hii inabidi kuthibitishwa wadau... Kuna thread humu inayomnukuu mke wa marehemu Mwangosi ambayo imeikanusha habari hii. Siku zote nikisikia habari za magazeti ya Uhuru au Habari Leo napata kichefuchefu!
 
Kwa sisi wakatoriki mtu akishajitolea kumtumikia Mungu ktk wito wa upadri amekuwa amefunga nadhiri ya kweli,na akijitoa kwa sababu yeyote ile huyo ANA LAANA YA KANISA MILELE,huyo padri alitoka kwa mambo yake ya uzinz,daima laana inamsumbua na kamwe asifikir atatuongoza watanzania!!!shame on you!!!!!

...Kwa Nyinyi WAKATORIKI??...I See! Afadhali. Bila shaka ni Kanisa Jipya. For Moment I thought You Were Talking About WAKATOLIKI! Thank God....!
 
Moderators tunaomba muifunge hii thread kwa sababu ni ya upotoshaji, ukweli umeshajulikana hizi ni siasa za mtaroni ni mwendelezo ule ule wa taariri ya Gazeti la Daily News mwaka 2010 kuhusu Dr Slaa.

Ushauri kwa Kimbunga ni kujishushia heshima bure kuleta habari ambazo hata wewe mwenyewe unafamu fika si za kweli na source siyo reliable. nadhani ipo siku utacopy Gazeti la Uhuru na kutuletea habari zao hapa kwa ubongo wako mdogo uliounesha leo.
 
Tumaini Makene hivi mtaacha habari za uzushi kama hizi kila siku mpaka lini? au baraza la habari nako wamejaa CCM? ni kwa nini msipeleke malalamiko baraza la habari au itisheni Press Conference ili kuwaweka uchi hawa mashetani.
 
Last edited by a moderator:
Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi amekanusha vikali habari zilizochapishwa na gazeti la habari Leo kuwa eti yeye alimshutumu Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa kuhusu rambirambi za mumewe.Akiongea na Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa amesema kwa uchungu mkubwa kuwa amesikitishwa sana kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na ni aibu kubwa chombo kikubwa cha habari kama Habari Leo kutoa habari ya uongo kwa viwango hivyo. Mjane huyo amesema kama angekuwa na Shida na Dr Slaa angemtafuta mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CDM na kwa hapa Iringa yeye na Msigwa ni majirani. Mjane huyo ameendelea kusema kitendo hicho kilichofanywa na gazeti hilo kimeamsha Msiba upya kwake kwani kina lengo la kutaka Jamii imdharau. Anaomba watanzania kuupuza habari hizo na ameshanga ni maadili gani haya ya uandishi na hajui kwa hali hii Taifa linakwenda wapi.


 
Wana-JF wote someni habari hii hapa....

Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi amekanusha vikali habari zilizochapishwa na gazeti la habari Leo kuwa eti yeye alimshutumu Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa kuhusu rambirambi za mumewe.

Akiongea na Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa amesema kwa uchungu mkubwa kuwa amesikitishwa sana kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na ni aibu kubwa chombo kikubwa cha habari kama Habari Leo kutoa habari ya uongo kwa viwango hivyo.

Mjane huyo amesema kama angekuwa na Shida na Dr Slaa angemtafuta mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CDM na kwa hapa Iringa yeye na Msigwa ni majirani.

Mjane huyo ameendelea kusema kitendo hicho kilichofanywa na gazeti hilo kimeamsha Msiba upya kwake kwani kina lengo la kutaka Jamii imdharau.

Anaomba watanzania kuupuza habari hizo na ameshanga ni maadili gani haya ya uandishi na hajui kwa hali hii Taifa linakwenda wapi.


Source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wangosi-apinga-vikali-kumshutumu-dr-slaa.html

Muhimu:
CCM, Kimbunga, Habari Leo, na wana-CCM wote waliokuwa wanatetea oungo huu wameumbuka vibaya saaana.
Penye ukweli, uongo na unafiki hujitenga.
Watu wengi sana walitetea uongo ulioletwa na Kimbunga toka gazeti la habari leo !!

Sasa wako wapi waongo wote hao !!!!
 
Hapo kwenye blue,wkt Dr anaahidi hakujua hayo uliyohoji?Hapo kwenye red kwani hizo pesa umeambiwa ndizo ziliahidiwa na DR?Hapo kwenye cyan colour hivi inachukua muda gani kuchakata mfumo wa akaunti?Usitetee aibu ibebeni nzima nzima!!

Mtu mwenye shida husubiria au kutoa heshima kumtafuta aliye mpromise sio kumuweka kwenye magazeti.

sasa hizo pesa za magazeti aende kulipia ada ya mtoto, kwani wamemwandika bila kumripa?

ndugu zake wapo si awaliie hao, sio kumsema mtu mwingine ambaye hata kesho akisema hata msaidia hana la kufanya kwani atapunguka nini???? (kama sio kisiasa......) mmmhhhhh

wangapi na ndugu za ndugu hata wazazi hawawezi timiza ahadi hadi wakiwa tayari?

hana shukurani huyo mama full stop.
 
Issue siyo Dr Hajatoa Rambirambi issue ni kwamba huyo mjane hajaweza kumpta Dr kwa mawasiliano! Hii habari ya kishabiki, mbona mwandosya na yeye hajatoa?

Huyu anashawishiwa na watu, mwenye kutaka msaada akiwa shidani kwei uvumilia. ameshindwa kumpata ndo magazeti yatampata. Dr amtolee nje tu. amenikasirisha msaada wa kurukia magazeti. Siasa ndani lazima mapema kaanza kabla hata ya kusubiri misaada itolewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom