Kumbe Katibu Mkuu CCM analipwa Mil11 kwa mwezi

Vita: Mishahara makatibu wakuu wa CCM, Chadema
a Joseph Mwendapole
14th May 2011

Malumbano kati ya viongozi wa CCM na Chadema yamendelea kupamba moto, safari hii Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akitangaza hadharani mshahara aliodai ni wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, kwa madai ya kutaka kuthibitisha kuwa halipwi fedha nyingi.
Kauli ya Nape aliyoitoa jana ni juhudi za kutaka kuusadikisha umma kwamba mshahara wa bosi wake haufui dafu kwa mshahara wa Katibu Mkuu wa (Chadema), Dk. Willbroad Slaa.Nape alisema kuwa Mukama analipwa mshahara wa Sh. milioni 1.5 na posho ya mwezi ya Sh. 300,000.

Juzi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa Chadema, Mabere Marando, alisema Mukama analipwa mshahara wa Sh. milioni 11 wakati Dk. Slaa analipwa Sh. milioni 7.1, hivyo CCM hawana sababu ya kushangaa mshahara wa Slaa.
Malumbano hayo ya mishahara ya viongozi wa vyama hivyo viwili yanatokana na kauli ya Nape kuwa Dk. Slaa ameshinikiza kulipwa mshahara mnono akieleza msimamo huo unakinzana na wakati akiwa mbunge alipokuwa akishinikiza malipo kwa wabunge yapunguzwe.
Nape alidai kuwa mshahara wa Dk. Slaa ni sawa na wa mbunge.

Hata hivyo, uchunguzi huru wa NIPASHE uliofanywa juu ya mishahara ya viongozi watendaji wa CCM umebaini kuwa makatibu wa CCM wa mikoa wanalipwa mishahara ya Sh. milioni moja baada ya kodi, wakati makatibu wa wilaya wanalipwa Sh. 700,000 baada ya kodi, ilahali Katibu wa UVCCM akitia kibindoni Sh. milioni 1.5. Kwa vigezo vya mishahara hiyo, ni sawa na kusema kwamba mishahara ya makatibu wa jumuiya na pengine ya makatibu wa mikoa haitofautiani na ile ya katibu mkuu.

Vile vile jana, Nape amekanusha madai yaliyotolewa na Mwanasheria wa Chadema, Marando kwamba yeye (Nape), alikwenda kuomba agombee ubunge Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya chama hicho na wakamkatalia kwa kukosa sifa.
Akizungumza na NIPASHE jana akiwa mkoani Singida, Nape alisema Chadema ndio walimfuata na kumwomba achague jimbo la kugombea kupitia chama hicho.
“Waliniambia nichague Jimbo lolote la uchaguzi Dar es Salaam nigombee isipokuwa Ubungo, lakini nikawakatalia, niliwaeleza wazi kuwa mimi kuhama CCM ni sawa na kumsilimisha Papa sasa hiyo kauli ya Marando ni uzushi wa hali ya juu,” alisema Nape.

Alidai hata alipohudhuria Baraza Kuu la chama hicho walimuomba avae sare za chama hicho na kisha kumwomba ajiunge na chama hicho, lakini alikataa na hata sare alizijaribu na kuwarudishia hapo hapo.
“CCM ni chama kikubwa na kinapata ruzuku kubwa kuliko Chadema, lakini angalia mshahara wa Katibu Mkuu wetu linganisha na Sh. milioni 7.5 anazolipwa Dk. Slaa, Marando ameamua kwa makusudi kuupotosha umma hivyo kama ni muungwana basi aombe radhi kwa Watanzania aliowadanganya,” alisema Nape. Alisema mshahara wa Mukama unalipiwa kodi wakati wa Dk. Slaa haukatwi kodi hivyo alimshauri kwanza kujisalimisha kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kulipa kodi anayodaiwa.

“Kutolipa kodi ni ufisadi wa hali ya juu, lakini mtu huyu huyu ambaye halipi kodi anajifanya ana uchungu na umaskini wa Watanzania, hata pale ofisini kwake kuna watu wanalipwa mishahara midogo hata haitoshi kujikimu kwa siku kumi, kuna msemo kwamba kabla hujatoa boriti kwenye jicho la mwenzako anza kutoa kwako,” alisema Nape.

“Tafsiri ya fisadi kwa mujibu wa Ilani yao ni mtu anayeishi kiujanja ujanja, sasa Dk. Slaa anaishi kwa mtindo huo maana huwezi kukwepa kodi inayotumiwa na serikali kuwaletea maisha bora wananchi, kisha mtu huyo huyo ukajifanya unawapenda Watanzania,” alisisitiza.
Alisema hata Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alifanya ufisadi kwa kukiuzia chama magari makuu kuu aina ya Mitsubishi Fuso, ambayo chama kilikuwa kimeyakodisha kwa ajili ya matumizi yake.

Kuhusu madai kuwa alinufaika na fedha za EPA, Nape alisema huko ni kutapatapa kwani hawajawahi kutajwa katika kashfa hiyo tangu ianze miaka mingi iliyopita na wameanza kumpakazia baada ya kuanza kuwashambulia.
“Hivi siku zote wanawataja wahusika wa EPA kwanini wasinitaje na mimi, leo hii wameona nimeanza kuanika maovu yao ndipo wanaanza kuhangaika kutafuta mambo ya kutunga, waambie Chadema ukivuliwa taulo chutama usikimbie, walizoea kusema wenzao sasa yamewageuka wanahaha” alisema.

Kuhusu madai kuwa anapokea mishahara miwili, wa U-DC na wa CCM, Nape alisema alishakabidhi ofisi hiyo siku nyingi na madai hayo si ya kweli kwani hajawahi kupokea hata mshahara mmoja tangu ateuliwe katikati ya mwezi uliopita.
“Tangu niteuliwe sijapata hata mshahara mmoja, inamaana Marando anamaanisha kuwa nalipwa mshahara kila wiki,” alihoji Nape.
Alisema gari analotumia hivi sasa ni mali ya CCM tofauti na madai ya Marando kuwa anatumia gari la serikali.

Juzi Marando akiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa chama hicho, Anthony Komu, waliwaambia waandishi wa habari kuwa mashambulizi ya Nape dhidi ya chama hicho yanatokana na chuki na hasira aliyonayo baada ya kukataliwa kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kadhalika, chama hicho kilidai kuwa mshahara wa Sh. milioni 7.1 anaolipwa Dk. Slaa na chama hicho ni kiasi kidogo ikilinganishwa na ule wa Mukama wa Sh. milioni 11.
 
Habari,

Katika pitapita zangu nimeona mengi lakini kwa wanasiasa kweli ni ubabaishaji tuu. Nimekutana na mtu ambaye alikuwa akifanya utafiti kuhusu mishahara ya watu wa CCM.

Lakini nikaja kugundua sio mshahara wa CCM bali wa Nape baada ya "kupandishwa cheo" kutoka ukuu wa wilaya kwenda ukatibu ropoka wa CCM.

Kwa mujibu wake mkuu wa wilaya anatia kibindoni kiasi cha mil 2 hivi kwa mwezi. Kisha na marupurupu unaweza fika kwenye mil 5 hivi na ushee hivi. Sasa hiki cheo hakina raha saana kama ukiwa mbunge. Maana unakuwa vuvuzela la mkuu tuu pale wilayani. Lakini ubunge unakamata sana marefu.

Sasa yeye akaendelea kudai kuwa kama mtu ukiamua kumpa madaraka makubwa zaidi hasa ndani ya chama ni lazima uamue kumpa "Bakshishi" kidogo ili atulize moyo. Akaenda mbali zaidi akasema ukiangalia tuu hapo utagundua dogo analipwa "kihesabu tuu" mil 6 na ushee kwa sasa.

Kuhusu katibu mkuu wa CCM bado haijawa wazi kwani mshahara wake unahisiwa kuwa mill 11 hivi. CCM wako katika harakati za kutaka kutangaza mishahara yao lakini wanaogopa kutaja ukweli "wameng'ang'ania" wa Dokta Slaa. Kwa style ileile ya propaganda kuliko ukweli.

Lakini kuhusu Dr. Slaa hela anazopata ni sawa na mbunge in value lakini ikumbukwe mbunge anapewa mill 100 kila mwaka kwa ajili ya maendeleo jimboni pia mill 200 kuweza kukopa kwenye benki yoyote nchini. Nape alitaka ubunge akaangukia pua sasa kaamua kuwa vuvuzela la JK kwa mtindo uleule wachafue CHADEMA nikupe ugali. Nape anahasira sana na CHADEMA baada ya kumpa ukweli kuwa kwa Ubungo hapendwi. Naona maneno haya yanamtesa saana!!

Kama jamaa akifanikiwa kupata document ya mishahara CCM tutaweka hapa uwanjani kisha nyingine atapasiwa vuvuzela la walalahoi Mhe Dr.Slaa

Pamoja

SOURCE: TISS
 
duh nadhani ungekuja na full documents...tungeappreiate sana...bt welnoted
 
habari,

katika pitapita zangu nimeona mengi lakini kwa wanasiasa kweli ni ubabaishaji tuu. Nimekutana na mtu ambaye alikuwa akifanya utafiti kuhusu mishahara ya watu wa ccm.

Lakini nikaja kugundua sio mshahara wa ccm bali wa nape baada ya "kupandishwa cheo" kutoka ukuu wa wilaya kwenda ukatibu ropoka wa ccm.

kwa mujibu wake mkuu wa wilaya anatia kibindoni kiasi cha mil 2 hivi kwa mwezi. Kisha na marupurupu unaweza fika kwenye mil 5 hivi na ushee hivi. Sasa hiki cheo hakina raha saana kama ukiwa mbunge. Maana unakuwa vuvuzela la mkuu tuu pale wilayani. Lakini ubunge unakamata sana marefu.

sasa yeye akaendelea kudai kuwa kama mtu ukiamua kumpa madaraka makubwa zaidi hasa ndani ya chama ni lazima uamue kumpa "bakshishi" kidogo ili atulize moyo. Akaenda mbali zaidi akasema ukiangalia tuu hapo utagundua dogo analipwa "kihesabu tuu" mil 6 na ushee kwa sasa.

Kuhusu katibu mkuu wa ccm bado haijawa wazi kwani mshahara wake unahisiwa kuwa mill 11 hivi. Ccm wako katika harakati za kutaka kutangaza mishahara yao lakini wanaogopa kutaja ukweli "wameng'ang'ania" wa dokta slaa. Kwa style ileile ya propaganda kuliko ukweli.

Lakini kuhusu dr. Slaa hela anazopata ni sawa na mbunge in value lakini ikumbukwe mbunge anapewa mill 100 kila mwaka kwa ajili ya maendeleo jimboni pia mill 200 kuweza kukopa kwenye benki yoyote nchini. Nape alitaka ubunge akaangukia pua sasa kaamua kuwa vuvuzela la jk kwa mtindo uleule wachafue chadema nikupe ugali. Nape anahasira sana na chadema baada ya kumpa ukweli kuwa kwa ubungo hapendwi. Naona maneno haya yanamtesa saana!!

Kama jamaa akifanikiwa kupata document ya mishahara ccm tutaweka hapa uwanjani kisha nyingine atapasiwa vuvuzela la walalahoi mhe dr.slaa

pamoja

source: Tiss

chadema wako kazini sasa! Nasikia dr slaa ataongeze mshahara na kuwa milioni 15!
 
Habari,

Katika pitapita zangu nimeona mengi lakini kwa wanasiasa kweli ni ubabaishaji tuu. Nimekutana na mtu ambaye alikuwa akifanya utafiti kuhusu mishahara ya watu wa CCM.

Lakini nikaja kugundua sio mshahara wa CCM bali wa Nape baada ya "kupandishwa cheo" kutoka ukuu wa wilaya kwenda ukatibu ropoka wa CCM.

Kwa mujibu wake mkuu wa wilaya anatia kibindoni kiasi cha mil 2 hivi kwa mwezi. Kisha na marupurupu unaweza fika kwenye mil 5 hivi na ushee hivi. Sasa hiki cheo hakina raha saana kama ukiwa mbunge. Maana unakuwa vuvuzela la mkuu tuu pale wilayani. Lakini ubunge unakamata sana marefu.

Sasa yeye akaendelea kudai kuwa kama mtu ukiamua kumpa madaraka makubwa zaidi hasa ndani ya chama ni lazima uamue kumpa "Bakshishi" kidogo ili atulize moyo. Akaenda mbali zaidi akasema ukiangalia tuu hapo utagundua dogo analipwa "kihesabu tuu" mil 6 na ushee kwa sasa.

Kuhusu katibu mkuu wa CCM bado haijawa wazi kwani mshahara wake unahisiwa kuwa mill 11 hivi. CCM wako katika harakati za kutaka kutangaza mishahara yao lakini wanaogopa kutaja ukweli "wameng'ang'ania" wa Dokta Slaa. Kwa style ileile ya propaganda kuliko ukweli.

Lakini kuhusu Dr. Slaa hela anazopata ni sawa na mbunge in value lakini ikumbukwe mbunge anapewa mill 100 kila mwaka kwa ajili ya maendeleo jimboni pia mill 200 kuweza kukopa kwenye benki yoyote nchini. Nape alitaka ubunge akaangukia pua sasa kaamua kuwa vuvuzela la JK kwa mtindo uleule wachafue CHADEMA nikupe ugali. Nape anahasira sana na CHADEMA baada ya kumpa ukweli kuwa kwa Ubungo hapendwi. Naona maneno haya yanamtesa saana!!

Kama jamaa akifanikiwa kupata document ya mishahara CCM tutaweka hapa uwanjani kisha nyingine atapasiwa vuvuzela la walalahoi Mhe Dr.Slaa

Pamoja

SOURCE: TISS
nape nnauye ni vuvuzela anataka yeye tu ndio alipwe mshahara mzuri. nape usijaribu kujiringanisha na dr slaaa
 
Sio kila habari ya mtaani uilete humu mkuu!!

.....Nape alisema kuwa Mukama analipwa mshahara wa Sh. milioni 1.5 na posho ya mwezi ya Sh. 300,000.

Juzi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa Chadema, Mabere Marando, alisema Mukama analipwa mshahara wa Sh. milioni 11 wakati Dk. Slaa analipwa Sh. milioni 7.1, hivyo CCM hawana sababu ya kushangaa mshahara wa Slaa.
Malumbano hayo ya mishahara ya viongozi wa vyama hivyo viwili yanatokana na kauli ya Nape kuwa Dk. Slaa ameshinikiza kulipwa mshahara mnono akieleza msimamo huo unakinzana na wakati akiwa mbunge alipokuwa akishinikiza malipo kwa wabunge yapunguzwe. Nape alidai kuwa mshahara wa Dk. Slaa ni sawa na wa mbunge.

Hata hivyo, uchunguzi huru wa NIPASHE uliofanywa juu ya mishahara ya viongozi watendaji wa CCM umebaini kuwa makatibu wa CCM wa mikoa wanalipwa mishahara ya Sh. milioni moja baada ya kodi, wakati makatibu wa wilaya wanalipwa Sh. 700,000 baada ya kodi, ilahali Katibu wa UVCCM akitia kibindoni Sh. milioni 1.5.

Kwa vigezo vya mishahara hiyo, ni sawa na kusema kwamba mishahara ya makatibu wa jumuiya na pengine ya makatibu wa mikoa haitofautiani na ile ya katibu mkuu.

"CCM ni chama kikubwa na kinapata ruzuku kubwa kuliko Chadema, lakini angalia mshahara wa Katibu Mkuu wetu linganisha na Sh. milioni 7.5 anazolipwa Dk. Slaa, Marando ameamua kwa makusudi kuupotosha umma hivyo kama ni muungwana basi aombe radhi kwa Watanzania aliowadanganya," alisema Nape. Alisema mshahara wa Mukama unalipiwa kodi wakati wa Dk. Slaa haukatwi kodi hivyo alimshauri kwanza kujisalimisha kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kulipa kodi anayodaiwa.
"Kutolipa kodi ni ufisadi wa hali ya juu, lakini mtu huyu huyu ambaye halipi kodi anajifanya ana uchungu na umaskini wa Watanzania, hata pale ofisini kwake kuna watu wanalipwa mishahara midogo hata haitoshi kujikimu kwa siku kumi, kuna msemo kwamba kabla hujatoa boriti kwenye jicho la mwenzako anza kutoa kwako," alisema Nape.
"Tafsiri ya fisadi kwa mujibu wa Ilani yao ni mtu anayeishi kiujanja ujanja, sasa Dk. Slaa anaishi kwa mtindo huo maana huwezi kukwepa kodi inayotumiwa na serikali kuwaletea maisha bora wananchi, kisha mtu huyo huyo ukajifanya unawapenda Watanzania," alisisitiza.
 
"Tangu niteuliwe sijapata hata mshahara mmoja, inamaana Marando anamaanisha kuwa nalipwa mshahara kila wiki," alihoji Nape.
Alisema gari analotumia hivi sasa ni mali ya CCM tofauti na madai ya Marando kuwa anatumia gari la serikali.
Juzi Marando akiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa chama hicho, Anthony Komu, waliwaambia waandishi wa habari kuwa mashambulizi ya Nape dhidi ya chama hicho yanatokana na chuki na hasira aliyonayo baada ya kukataliwa kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam.
 
Sio kila habari ya mtaani uilete humu mkuu!!

.....Nape alisema kuwa Mukama analipwa mshahara wa Sh. milioni 1.5 na posho ya mwezi ya Sh. 300,000.

Juzi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa Chadema, Mabere Marando, alisema Mukama analipwa mshahara wa Sh. milioni 11 wakati Dk. Slaa analipwa Sh. milioni 7.1, hivyo CCM hawana sababu ya kushangaa mshahara wa Slaa.
Malumbano hayo ya mishahara ya viongozi wa vyama hivyo viwili yanatokana na kauli ya Nape kuwa Dk. Slaa ameshinikiza kulipwa mshahara mnono akieleza msimamo huo unakinzana na wakati akiwa mbunge alipokuwa akishinikiza malipo kwa wabunge yapunguzwe. Nape alidai kuwa mshahara wa Dk. Slaa ni sawa na wa mbunge.

Hata hivyo, uchunguzi huru wa NIPASHE uliofanywa juu ya mishahara ya viongozi watendaji wa CCM umebaini kuwa makatibu wa CCM wa mikoa wanalipwa mishahara ya Sh. milioni moja baada ya kodi, wakati makatibu wa wilaya wanalipwa Sh. 700,000 baada ya kodi, ilahali Katibu wa UVCCM akitia kibindoni Sh. milioni 1.5.

Kwa vigezo vya mishahara hiyo, ni sawa na kusema kwamba mishahara ya makatibu wa jumuiya na pengine ya makatibu wa mikoa haitofautiani na ile ya katibu mkuu.

"CCM ni chama kikubwa na kinapata ruzuku kubwa kuliko Chadema, lakini angalia mshahara wa Katibu Mkuu wetu linganisha na Sh. milioni 7.5 anazolipwa Dk. Slaa, Marando ameamua kwa makusudi kuupotosha umma hivyo kama ni muungwana basi aombe radhi kwa Watanzania aliowadanganya," alisema Nape. Alisema mshahara wa Mukama unalipiwa kodi wakati wa Dk. Slaa haukatwi kodi hivyo alimshauri kwanza kujisalimisha kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kulipa kodi anayodaiwa.
"Kutolipa kodi ni ufisadi wa hali ya juu, lakini mtu huyu huyu ambaye halipi kodi anajifanya ana uchungu na umaskini wa Watanzania, hata pale ofisini kwake kuna watu wanalipwa mishahara midogo hata haitoshi kujikimu kwa siku kumi, kuna msemo kwamba kabla hujatoa boriti kwenye jicho la mwenzako anza kutoa kwako," alisema Nape.
"Tafsiri ya fisadi kwa mujibu wa Ilani yao ni mtu anayeishi kiujanja ujanja, sasa Dk. Slaa anaishi kwa mtindo huo maana huwezi kukwepa kodi inayotumiwa na serikali kuwaletea maisha bora wananchi, kisha mtu huyo huyo ukajifanya unawapenda Watanzania," alisisitiza.

Je wajua kwa nini JF waliweka sehemu uchague kama ni news, tetesi au Hoja?
Nani kakulazimisha kufungua thread ambayo ni tetesi? Kimbelembele tuu au umbeya tuu au ujinga wako ? Mimi nimeeleza vizuri tuu kuwa nimeambiwa. Pia nikaamua kwa dhati kuweka "tetesi" kabla ya thread... Sasa uCCM wako usikufanye ukasikia kufakufa....

Nawasilisha
 
ngoja nikugongee thanks mkuu kama hataki nani kamlazimisha asome au upumbavu wake tu ila nashukuru umemweleza vizuri sana hongera analeta ukada hapa sio lazima kila mtu ajue uko ccm?haina faida kwetu mnatapatapa tu.
 
ngoja nikugongee thanks mkuu kama hataki nani kamlazimisha asome au upumbavu wake tu ila nashukuru umemweleza vizuri sana hongera analeta ukada hapa sio lazima kila mtu ajue uko ccm?haina faida kwetu mnatapatapa tu.
 
Habari,

Kama jamaa akifanikiwa kupata document ya mishahara CCM tutaweka hapa uwanjani kisha nyingine atapasiwa vuvuzela la walalahoi Mhe Dr.Slaa

Pamoja

SOURCE: TISS

Kweli mkuu hilo beat lako la source yako ndiyo nimeipenda sana mkuu, full confidence.
 
Mimi sijui kwa nini issue hii inapotoshwa tena kwa makusudi. Suala la mishahara ya viongozi wa vyama vya siasa halikupaswa kuwa issue. Kilicho issue hapa ni mshahara wa Dr. Slaa na hiyo inatokana na kile kinachdaiwa kuwa ni "unafiki" kwa sababu kabla ya hapo alipigia kelele sana ukubwa wa mishahara ya wabunge na picha ilionyesha kana kwamba kama yeye angeendelea na ubunge asingepokea mshahara mnono wanaolipwa wabunge. Pale ilipobainika kwamba CDM wameingia makubaliano na Slaa kumlipa mshahara ulio sawa na wa mbunge ndipo Nape alipopaza sauti na kuhoji kama huo si unafiki. Na ndiyo maana hakuna mwenye interest ya kujua Mtemelwa au Komu au Mrema wanalipwa kiasi gani, na isingekuwa issue hata kama wangekuwa wanalipwa milioni 10 au zaidi kila mmoja. Sasa kama Mukama analipwa milioni 11 au Nape analipwa milioni 6, bado hilo siyo jibu la hoja ya Nape. Lakini swali lingine muhimu ni je, kwa nini mshahara wa mtumishi wa chama uwe pegged kwenye mshahara wa mbunge na huku kazi zao au majukumu yao ni tofauti? Mengine yote yatazungumzwa lakini katika hili Dr. Slaa alipotoka na sasa aubebe mzigo wake kwa yanayozungumzwa sasa juu yake. Tatizo ni kwamba mijadala inapokuwa inahusu viongozi wa CDM na hasa kunapokuwa na chembe ya lawama, baadhi ya wana jamvi humu jazba huwapanda na mijadala inageuka kuwa so adolescent! Reasoning inaondoka na kila mtu anayepingana nao ni adui na ajiandae kwa matusi!
 
DONNOT DWELL MUCH ON SALARY!! MSHAHARA NI UJIRA STAHIKI KUTOKANA NA MAKUBALIANO KATI YA MWAJIRI NA MWAJIRIWA NA SI UFISADI!! KAMA NAPE AMEZUNGUMZA HIVYO THEN HE IZ AFTER CHEAP POPULARITY OR ANASAMBAZA UONGO KAMA KAWAIDA YA WA2 WA MAGAMBA. HUWEZI KUITA MALIPO HALALI UFISADI THATS WHY EVEN SLAA DIDNOT CALL MPs SALARIES NI UFISADI BALI ALILALAMIKA KIWANGO. GUYS LET US NOT LOOSE 4CUS
 
Malumbano kati ya viongozi wa CCM na Chadema yamendelea kupamba moto, safari hii Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akitangaza hadharani mshahara aliodai ni wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, kwa madai ya kutaka kuthibitisha kuwa halipwi fedha nyingi.

Kauli ya Nape aliyoitoa jana ni juhudi za kutaka kuusadikisha umma kwamba mshahara wa bosi wake haufui dafu kwa mshahara wa Katibu Mkuu wa (Chadema), Dk. Willbroad Slaa.

Nape alisema kuwa Mukama analipwa mshahara wa Sh. milioni 1.5 na posho ya mwezi ya Sh. 300,000.
Juzi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa Chadema, Mabere Marando, alisema Mukama analipwa mshahara wa Sh. milioni 11 wakati Dk. Slaa analipwa Sh. milioni 7.1, hivyo CCM hawana sababu ya kushangaa mshahara wa Slaa.

Malumbano hayo ya mishahara ya viongozi wa vyama hivyo viwili yanatokana na kauli ya Nape kuwa Dk. Slaa ameshinikiza kulipwa mshahara mnono akieleza msimamo huo unakinzana na wakati akiwa mbunge alipokuwa akishinikiza malipo kwa wabunge yapunguzwe.

Nape alidai kuwa mshahara wa Dk. Slaa ni sawa na wa mbunge.
Hata hivyo, uchunguzi huru wa NIPASHE uliofanywa juu ya mishahara ya viongozi watendaji wa CCM umebaini kuwa makatibu wa CCM wa mikoa wanalipwa mishahara ya Sh. milioni moja baada ya kodi, wakati makatibu wa wilaya wanalipwa Sh. 700,000 baada ya kodi, ilahali Katibu wa UVCCM akitia kibindoni Sh. milioni 1.5.
Kwa vigezo vya mishahara hiyo, ni sawa na kusema kwamba mishahara ya makatibu wa jumuiya na pengine ya makatibu wa mikoa haitofautiani na ile ya katibu mkuu.

Vile vile jana, Nape amekanusha madai yaliyotolewa na Mwanasheria wa Chadema, Marando kwamba yeye (Nape), alikwenda kuomba agombee ubunge Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya chama hicho na wakamkatalia kwa kukosa sifa.
Akizungumza na NIPASHE jana akiwa mkoani Singida, Nape alisema Chadema ndio walimfuata na kumwomba achague jimbo la kugombea kupitia chama hicho.

"Waliniambia nichague Jimbo lolote la uchaguzi Dar es Salaam nigombee isipokuwa Ubungo, lakini nikawakatalia, niliwaeleza wazi kuwa mimi kuhama CCM ni sawa na kumsilimisha Papa sasa hiyo kauli ya Marando ni uzushi wa hali ya juu," alisema Nape.

Alidai hata alipohudhuria Baraza Kuu la chama hicho walimuomba avae sare za chama hicho na kisha kumwomba ajiunge na chama hicho, lakini alikataa na hata sare alizijaribu na kuwarudishia hapo hapo.
"CCM ni chama kikubwa na kinapata ruzuku kubwa kuliko Chadema, lakini angalia mshahara wa Katibu Mkuu wetu linganisha na Sh. milioni 7.5 anazolipwa Dk. Slaa, Marando ameamua kwa makusudi kuupotosha umma hivyo kama ni muungwana basi aombe radhi kwa Watanzania aliowadanganya," alisema Nape. Alisema mshahara wa Mukama unalipiwa kodi wakati wa Dk. Slaa haukatwi kodi hivyo alimshauri kwanza kujisalimisha kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kulipa kodi anayodaiwa.

"Kutolipa kodi ni ufisadi wa hali ya juu, lakini mtu huyu huyu ambaye halipi kodi anajifanya ana uchungu na umaskini wa Watanzania, hata pale ofisini kwake kuna watu wanalipwa mishahara midogo hata haitoshi kujikimu kwa siku kumi, kuna msemo kwamba kabla hujatoa boriti kwenye jicho la mwenzako anza kutoa kwako," alisema Nape.
"Tafsiri ya fisadi kwa mujibu wa Ilani yao ni mtu anayeishi kiujanja ujanja, sasa Dk. Slaa anaishi kwa mtindo huo maana huwezi kukwepa kodi inayotumiwa na serikali kuwaletea maisha bora wananchi, kisha mtu huyo huyo ukajifanya unawapenda Watanzania," alisisitiza.

Alisema hata Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alifanya ufisadi kwa kukiuzia chama magari makuu kuu aina ya Mitsubishi Fuso, ambayo chama kilikuwa kimeyakodisha kwa ajili ya matumizi yake.

Kuhusu madai kuwa alinufaika na fedha za EPA, Nape alisema huko ni kutapatapa kwani hawajawahi kutajwa katika kashfa hiyo tangu ianze miaka mingi iliyopita na wameanza kumpakazia baada ya kuanza kuwashambulia.

"Hivi siku zote wanawataja wahusika wa EPA kwanini wasinitaje na mimi, leo hii wameona nimeanza kuanika maovu yao ndipo wanaanza kuhangaika kutafuta mambo ya kutunga, waambie Chadema ukivuliwa taulo chutama usikimbie, walizoea kusema wenzao sasa yamewageuka wanahaha" alisema.

Kuhusu madai kuwa anapokea mishahara miwili, wa U-DC na wa CCM, Nape alisema alishakabidhi ofisi hiyo siku nyingi na madai hayo si ya kweli kwani hajawahi kupokea hata mshahara mmoja tangu ateuliwe katikati ya mwezi uliopita.
"Tangu niteuliwe sijapata hata mshahara mmoja, inamaana Marando anamaanisha kuwa nalipwa mshahara kila wiki," alihoji Nape.

Alisema gari analotumia hivi sasa ni mali ya CCM tofauti na madai ya Marando kuwa anatumia gari la serikali.
Juzi Marando akiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa chama hicho, Anthony Komu, waliwaambia waandishi wa habari kuwa mashambulizi ya Nape dhidi ya chama hicho yanatokana na chuki na hasira aliyonayo baada ya kukataliwa kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kadhalika, chama hicho kilidai kuwa mshahara wa Sh. milioni 7.1 anaolipwa Dk. Slaa na chama hicho ni kiasi kidogo ikilinganishwa na ule wa Mukama wa Sh. milioni 11.

Chanzo: Nipashe 14/05/2011
 
Khaa!! Dr Slaa si KATIBU MKUU TENA.

''Inabidii tusogeze shule mbele kidogo'' - Dr W Slaa
 
Back
Top Bottom