Kumbe John Tendwa ni Simba wa Makaratasi

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,398
3,243
Hii nimekutana nayo kwenye chambuzi za gazeti moja.
Kwa jinsi ccm inavyokosa mvuto ndivyo na huyu bwana anavyochanganyikiwa.
Tazama kauli zake za hivi karibuni
Alisema atavifuta vyama vyote visivyofanya chaguzi za ndani, mikutano ya hadhara nakutafuta wanachama wapya sanjari na kufungua matawi si kusubiri mpaka wakati wa uchaguzi mkuu tu.
Sasa huyu tendwa anaibuka na kutishia kufuta vyama vinavyofanya mikutano wakati hakuna chaguzi kwani vinahatarisha amani huku akikiacha ccm kikifanya mikutano yake kwa bashasha kubwa bila kukemea chochote.
Huyu bwana ilidaiwa anasajili baadhi ya vyama ili kuua vyama makini sijui hiyo ndiyo kazi aliyonayo ama vp. Kwa nini asijitahidi kujenga uwanja sawa wa demokrasia kwa vyama vyote na pia mazingira mazuri kwa polisi ili wasitumie nguvu na mbinu za ajabu ili kuzima vyama makini visiweze kujitanua hadi vijijini.
Ameidhalilisha sana ofisi yake mpaka uploadfromtaptalk1348117550712.jpg
 
Huyu John ALISHATENDWA! Kwisha kazi!
Kweli katendwa na si kidogo. Yeye ni kada wa magama (ccm) na aliteuliwa na mwenyekiti (JK) na magamba. Hivyo sharti atumikie magamba ili kulinda kitumbua chake kwa gharama yoyote. Si mlisikia aliposema kuwa polisi kuua wananchi/wandishi wasio na kosa si jambo la ajabu eti kwa vile hata nchi za nje wanaua. Si ulishasikia kuwa kuna mtu mzima hovyo? John Tendwa ni mmojawapo.
 
Huyu JOHN TENDWA anadhalilisha wasomi na watanzania kwa ujumla.kila siku anatumia akili za kuambiwa zake zipo LIKIZO.
 
Back
Top Bottom