Kumbe Kikwete alikuwa na share Kempinski!? UNESCO walituokoa...

Kaka / Dada nikusahihishe kidogo kama huto mind, ni kweli management ya Bilila, Zamani na Kilimanjaroi imebadilika na sio rahisi kwa new management kutumia jina la previous management, managemet name inalipiwa tena maelfu ya dola kwa mwezi, huezi ktumia logo ya kempiski bila kibali cha kempiski, vile vile nasisitiza mmiliki ni ASB Tanzania Ltd na sio Kikwete, Kikwete amepewa milki ya Tanzania na waTanzania kwa mujibu wa Katiba, vinginevyo ushahidi utimie

Wewe ndio Kikwete?. Mbona unasisitiza sana kwamba Kikwete sio mmiliki wakati huo huo kwenye post yako ya kwanza umesema atafutwe mmiliki wa ASB Tanzania Ltd, ina maana wewe pia humfahamu.

Hiyo ASB Tanzania Ltd inayomilki hizo hotels bado Kikwete anaweza kuwa na share nyingi au hata 100%...
 
Duh! hii story inavutia ila ipo tofauti na ufahamu wangu, nimetembelea Bilila, Kilimanjaro na Zamani Zanzibar Kempiski kwa nyakati tofauti mara kadhaa kutokana na kazi zangu, ila ninachofahamu hoteli zote hizi zipo chini ya ASB Tanzania Ltd, Kempiski alihusika na menejimenti tu! kama iivyokuwa Net Group Solutions kwa Tanesco, na hao kempiski wana manage hotels nyingi duniani ila nyingi wanazo zimanage hawazimiliki sasa JK anahusishwaje? na kwa mfan Bilila Lodge, ni hoteli nzuri ila haifikii sasakwa lodge ipo humo humo Serengeti ni nzuri tena ni ghali mara mbili ya billila.

Kempiski walishindwana na ASB Tanzania Ltd sio UNESCO, na tusimwingize Kikwete katika hili tuitafute ASB ni kampuni ya nani?
Usichanganye mambo........soma vitu na kuelewa........hapa UNESCO haijahusishwa na mikataba ya biashara kati ya kempiski na ASB Ltd.......hapa UNESCO imetajwa ilisaidia kuzuia ujenzi wa serengeti highway project na pia ujenzi wa hotel ya kempski kule ngome kongwe-zanzibar (mambo msige)walikosemekana kununua ardhi kwa malipo mbuzi ya dola 10,000 kwa mwaka kwa miaka 99.Haya maeneo tajwa yanahusishwa na UNESCO kwasababu ni world heritage sites.Kwa taarifa tu ni kwamba UNESCO walisema kuwa kama ujenzi tajwa utaendelea basi walisema(UNESCO) kuwa wangeyaondolea haya maeneo tajwa hadhi ya kuwa world heritage sites na ndio sababu mwandishi anasema baadae serikali walipeleka barua UNESCO kusema kuwa hawataendelea na ujenzi huu(kupitia kwa Hezekiel Maige).JK anahusishwa na issue kwasababu ya kusemekana kuwa alikuwa na investment kwenye property(hotel)zote 3 zilizokuwa zinamilikiwa na kempiski kipindi hicho(yaani Zamani,Bilila na Kilimanjaro)na kempiski ndio walitaka kujenga hotel kwenye haya maeneo tajwa.Ikumbukwe pia kuwa Bilila lodge imo humo humo karibu na eneo tajwa lililokuwa lijengwe serengeti highway project.

Kwa zaidi soma hii: Victory in the Serengeti! «

Angalizo: Hizi ni habari za kusoma zisizokuwa na udhibitisho......na si kazi yetu humu jf kuthibitisha(hatuna nyenzo).......wako walioajiriwa kwa kodi zetu kufanya hizi kazi kwa maana ya kufanyia kazi taarifa.

Pili: Aliyeandika habari hizi kwenye blog yake ni huyu bwana:Jim Heck, director of http://ewtravel.com/: African Safari Guide since 1972 and author of three African travel guide books. Hivyo kwa wale wenye kutaka kujua zaidi hii issue wamtafute huyu bwana.
 
Taarifa ya mtandao wa africaanswerman.com inasema Kempisky wameondoka lakini mmiliki ni yuleyule hapa kuna kitu hakiko sahihi
Mwandishi wa Makala hii ange declare interest. Ukisoma between the line utagundua mwandishi aidha ni mtu wa SERENA au analipwa na Serena kupotosha ukweli. Ajenda kubwa ya Serena ni kucontrol industry ya mahoteli Afrika ya Mashariki. Wamefanikiwa upande wa Kenya,na Uganda...Tanzania umekuwa mfupa mgumu kuuvunja. Ndio maana wamefika mahala wanaendesha kampeni za uwongo na uzishi. Labda niwape picha ya maslahi ya Serena na article hii inavyolenga kudistort ukweli bila kuonyesha interest zao:
Serena wanamiliki Hoteli kwenye mbuga upande wa pili wa Serengeti (yAani kule Kenya). Wanapata watalii wengi sana kule. Uamuzi wa serikali ya tanzania kuruhusu Belila Lodge (Kempinski) kujenga lodge upande wa pili wa serengeti waliona kama ni kuwaletea competition. walilobby sana na kuonga watu wengi mradi huo usifanikiwe-na mara nyingine walitumia visingizio vya mazingira. Lakini mradi ukafanyika-na matokeo yake nusu ya biashara yao ikapotelea Tanzania. Hawakufurahi!

Kama hiyo haitoshi mwekezaji mwingine alitaka kuweka five star property kule ngorongoro- serena wakaona hiyo itawaulia biashara yao nyingine (pale Ngorongoro wana lodge yao). Wakaendesha kampeni kubwa ya kudai mazingira yanaharibiwa etc etc...hotel hiyo haikujengwa. Upo ushahidi wa watu walioongwa kuhakikisha mradi huo hautekelezeki. Athari zake kwa nchi ni kukosekana mapato ya kodi, ajira kwa watz na fursa nyinginezo za biashara ya kuuza vyakula na huduma mbalimbali

Kama hiyo haitoshi,Serena wamekuwa mstari wa mbele ku distort ukweli juu ya kiwanja walichopewa hao Kempinski pale Zanzibar kujenga 5 star property....kama kawaida wamewaonga watu ili hotel hiyo isijengwe kwakuwa ikijengwa itawaletea competiton wao Serena maana hotel yao nyingine ipo pale pale mita 40 tu kutoka kiwanja walichopewa Kempinski. Sasa kimbilio lao ni kudai JK ndio ame influence. Mambo ya utalii ya zanzibar sio ya muungano-iweje leo JK ahusishwe? Wangedai ni Karume au Shain ingeeleweka.lakini uzuri ni kwamba SMZ ishalitoea msimamo suala hili-hoteli itaendelea kujengwa kwakuwa itatoa ajira kwa wazanzibari,italipa kodi na kutoa fursa za biashara kwa wazenji

Vita ya serena haijaishia hapo...sasa wanapinga barabara ya serengeti isijengwe,kwakuwa itarahisisha watalii kufikia maeneo ya mbuga kwa haraka na hivyo kuwafanya watalii wengi ku opt kupitia upande wa TZ badala ya kenya ambako wao ndio wamewekeza zaidi. Kwanza ukweli ufahamike,barabara inayojengwa na TZ haiigii mbugani....lami inajengwa kupita njia yote hadi eneo la mbuga pale hapatawekwa lami,sana sana patachongwa vizuri ili papitike bila taabu kama ilivyo kule ngorongoro.

Mwisho ni vema mkajua mmiliki wa serena ni aghakhan ambaye katika miaka ya karibuni biashara zake TZ hazipewi preferential treatment kama walivyozoea miaka ya nyuma. Walitaka wamegewe kipande cha Gymkhana kujega hoteli wamenyimwa! Siku hizi safari za aghakhan pale Magogoni zimepungua....kama ilivyokuwa zamani.

Matokeo yake ameamua kuwa mpinzani wa chinichini wa serikali ya TZ kupitia vyombo vya habari habari anavyomiliki nchini kama vile gazeti la mwananchi na the citizen.

Wakati umefika kureview hizi preferential treatment anazopata huyu bw agakhan hapa kwetu. Hospitali yake ya Dar hailipi kodi hata senti moja. Kila kitu kuanzia madawa,fenicha mpaka toilet paper vipo tax exempted and yet Agakhan ni the most expensive hospitali TZ ukiachilia ile ya wasouth africa ya Trauma centre(walau wale wanalipa kodi)

Main investment base ya agakhan ipo Kenya; Tz ni proxy tu. Wasituchanganye!
 
eti kwenye hotuba yake juzi anawasingizia wakoloni walituachia msingi mbovuwa uchumi,sijui alitaka watusaidieje,rasirimali zote waliacha,wizi anaendekeza yeye,anatutania tu
 
Msekwa ndiye mwenyekiti wa bodi wa hii pande inayohusika na Serengeti (presidential appointee) na ni huyu huyu Msekwa ana nafasi kubwa CCM ya kucheza chekundu-cheusi kwa niaba ya rais. Pia ni Msekwa na Makinda pekee ndio spika MSTAAFU pekee aliyetunukiwa nishani ya uhuru kati ya ma-spika wastaafu 4 (Makinda bado hajastafu). Connecting the dots!
 
The former French president has been found guilty and sentenced for two years over corruption and embezzlement when he was the Mayor of Paris.....This one day might as well happen to our former presidents....
 
Ukisoma hbr hii mwili unasisimuka!
sasa iweje apewe hongo ya suti wkt ana share pale? kati ya source na wikileaks tuamini ipi?
 
Please msipotoshe watu.
Kempinski na Hyatt ni hotel management companies.
The owner of the property is still the same, Mr. Ali Bawadry.

Mkataba wa kumanage umeisha na Ali kawapa tender Hyatt.
Kempinski was never the owner nor is Hyatt.

Unlike Royal Palm, hiyo ilikuwa inamilikiwa na Prince Waleed aliyeinunua toka kwa yule mgiriki.
Prince Waleed aliwaajiri Moevenpick to manage the property.
Ila kwa sasa Waleed ameuza kwa Serena ambao wao wenyewe wataimanage pia.

Good, What do you say about huu mchezo wa kuuza na kununua? May be ya JK sio muhimu, lakini hii uza na nunua ina maanisha nini? Shamba la bibi, nchi ya watu wasio makini, wachache wanakula rushwa.....
 
Msekwa ndiye mwenyekiti wa bodi wa hii pande inayohusika na Serengeti (presidential appointee) na ni huyu huyu Msekwa ana nafasi kubwa CCM ya kucheza chekundu-cheusi kwa niaba ya rais. Pia ni Msekwa na Makinda pekee ndio spika MSTAAFU pekee aliyetunukiwa nishani ya uhuru kati ya ma-spika wastaafu 4 (Makinda bado hajastafu). Connecting the dots!

I have connected.

Hata hivyo Makinda ni kituko cha mwaka. only last week kapata nishani ya kwua spika bora, leo nii ana kashfa ya posho za wabunge ambazo serikali nzima imekosa ufafanuzi!
Makubwa sana haya!
 
watawala kama hawa watafanya juu chini wasitoke madarakani wakihofu mashitaka...nifikiriavyo mie, ukiingia upinzani tz, haya yote yatakuja kufumuka na hapo ndo tutaanza safari ndefu ya maendeleo ya kweli kwa nchi hii
 
Nimeshtuka kusikia kwamba Hoteli ya Kempimsk kwa mara nyingine tena imebadilishwa jina na kuitwa Hyatt Hotel. Ina maana miaka mitano imeshifika hivyo Hoteli imepata wamiliki wengine ambao kwa mujibu wa sheria zetu mbovu za kodi nao watapewa msamaha maalum wa kodi (tax break/tax exemption) kwa kipindi cha miaka mitano?Kwahiyo ile filamu ya tax break kwa wamiliki wa tangu ilipokuwa ikiitwa sijui Hilton Hotel hadi Kempimsk na sasa Hyatt Hotel bado inaendelea.Hakika nchi yetu ya Tanzania inaongozwa na viongozi wasiokuwa na uchungu wala uzalendo nayo.Pumzika kwa amani Baba yetu wa Taifa,Nchi uliyotumia juhudi nyingi kuijenga inaharibiwa na warithi wako.
 
Wenyenchi yao watakujia kwa mapanga shauri yako.Kwanza utaulizwa hizo pesa za serikali au za mlipa kodi?Na mwisho watakwambia inabidi tujadili shule yako uliyokwenda kama kweli ulifaulu au lah.Shauri yako Mwananchi mwenzangu.Waache wenyenchi yao wale.
 
Back
Top Bottom