Kumbe JK alikuwa anampinga Lowassa kimya kimya?

Wakuu tatizo la Tanzania si nani kasema nini lini na wapi. Cha msingi ni nani kafanya nini lini na wapi. Maneno ya hawa woooote JK na genge lake yamekuwa na utata mara nyingi sana. Kitakachosemwa kinaweza kumaanisha kitu kingine kabisa au ni mtego wa kumyaka ngedere mwingine aliye mbali!!!
Waswahili wanasema Waarabu wa Pemba hujuana kwa Vilemba..hii ikiwa na maana zaidi kufikiria kwamba kila mwarabu ni Mpemba..Vilemba vyao ndio kitambulisho na sii rangi au lugha!
 
Kama sikosei strategy ya Tanzania kwenye utalii ni tofauti na ya Kenya. Wakati wakenya wana aim at low margin mass tourism; yaani watalii wengi wenye kipato cha kawaida, Tanzania tuna aim at high value, high margin, low volume tourism. Hii ndi mbinu za kimasoko na wataalam wa masoko wanajua haya. Ni sawa na Ferrari na Toyota. Kenya wamechukua Toyota Strategy, Tanzania tumechukua Ferrari strategy.

Ni kutokana na strategy hiyo, Tanzania hatutaki kuvutia uendelezaji mwingi wa miradi ya mahoteli katika mbuga zetu. Mbuga zetu zinatakiwa zibaki pristine (natural kama zilivyokuwa miaka nenda rudi). Siku hizi watalii matajiri hawataki kusukumana na kina kajamba nani huko maasai mara. Wale wenye mipesa mingi wanataka waende maeneo ambayo hayako overcrowded kwa sababu zao za kibinafsi na za kiusalama. kwa hiyo wao wanataka mbuga watakazo tembelea ziwe really expensive. Strategy ya Tanzania ilikuwa ni kwenye soko kama hili.

Long term strategy ya Tanzania inaonekana kulipa zaidi. Tanzania tunapata relatively watalii kidogo kuliko kenya, ila tunapata hela karibu sawa. Mazingira katika Mbuga zetu yanakuwa maintained vizuri zaidi na utalii wetu unaweza kupay off vizuri zaidi na ni sustainable.

Hii strategy ikisimamiwa vizuri na tukaacha urafi, miaka kumi mbele tutakuwa tunatengeneza fedha nyingi hata mara mbili kuliko Kenya. Maasai mara imeshakuwa kama mjini, mahoteli kibao; kwenye high season watalii ni wengi mno kiasi cha kupafanya pasifae kuwa mbuga. Tatizo letu, Tangu kuondoka kwa Mwalimu, hatuna long term strategic plan. Hii plan ilikuwa ya mwalimu, baada ya kuona wakenya wanajaza watalii Nyomi, alijua si muda mrefu mbuga zao zitapoteza thamani.

Kwa hiyo Kikwete kuzungumzia ku limit ujenzi wa mahoteli humo mbugani ni for long term strategic interrest za nchi. Hili halihitaji maelezo mengi. Jirani yako akichukua strategy fulani, si lazima u copy ya kwake. Mbinu yetu naamini ni bora zaidi. Hata kwenye madini hiyo ndo ilikuwa strategy ya mwalimu, alijua huko mbele dhahabu zitapanda sana bei kwani hazioti. Akasema sisi tunafungia ardhi yetu hadi baadaye. Makapa akawafungulia ardhi kina Barick sasa hivi wanachota dhahabu bwerere!

Tena inatakiwa tuwe makini zaidi. Strategy yetu ni makini zaidi na viongozi wetu inatakiwa waisimamie!!
 
Mkuu,
Tutegemee nini kutoka kwako pale unapotaka kulazimisha hoja juu ya JK dhidi ya Lowasa?
Kauli ya JK haipingani kwa namna yeyote na hiyo kauli ya Lowasa.
Lowasa amesema zijengwe hoteli nyingi na JK amesisitiza zisijengwe kiholela ni lazima ziwe na ubora wa hali juu zitazovutia watalii. Kwa maana hiyo basi hata zikijengwa 1000 lakini zikiwa nzuri kama Bilila, RUXAAA!!!!!

ASANTE SANA, mimi nilidhani naelewa hivyo PEKE YANGU, kichwa cha habari na HABARI yenyewe imekaa Kiuandisha wa TANZANIA TANZANI. JK kasema zijengwe hotel nzuri EL alisema zijengwe nyingi wapi wanapingana hapo???? Walimu kazi wanayo kwa mtindo huu tutaendelea KUIBA MITIHANI
 
wandugu kwenye siasa au ungwini hakuna aliye sahihi na ambaye si sahihi, kilichopo ni kujenga hoja na kuitetea hoja.

Kikwete amewahi kutofautiana kikauli na lowassa mara nyingi, mojawapo ikiwa ni ile ya "mamilioni ya jakaya". Lowassa alitaka watendaji wa benki wasilete urasimu wa kutoa fedha zile, na kikwete akasema fedha zile ni mikopo, na taratibu zote za kibenki za kugawa mikopo nafuu zifuatwe, na hakuna kugawa fedha kiholela holela. Ni hoja tu, na jinsi mtu anapoweza kuzijenga na kukubalika.

Na wakati mwingine mwenye kisu kikali ndiye mla nyama, na jk ana kisu cha urais, na mara nyingi yeye husema mwishoni.
rejea kugeuka mbogo kwa jk na excuses za wasimamizi juu ya mahela yale!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kichekesho
 
Mzee Mwanakijiji mwanzo nilikuona kama mtu mwenye busara lakini sasa naanza kupata mashaka kidogo kwamba ndiye mwanakijiji huyu huyu aliyekuwa anatuletea hadithi za kuvutia au mwingine.

Sioni sababu ya kumshambulia mtu kama umepishana nae hoja ............cha msingi ni kutoa maoni yako ili mjadala uendelee.........tujaribu kuchangia mada zaidi kuliko kuangalia nani ametuma na amesema nini. Back to the topic .......mimi naona kama kitu sio kizuri basi kizuiwe kwa wote haina sababu ya kuruhusu mmoja na kuacha wengine....things dont work that way.....yanayosemwa labda yapo!
 
I agree,

Lowasa hana jina zuri sana sasa hivi hasa kwa watanzania. JK, kama walivyo wabunge wetu sasa hivi, anajua kuwa 2010 is just around the cornner na anatakiwa kuji disassociate na wote wanaosemekana kuwa mafisadi na kuufanya kila linalowezekana kuwa apease wapiga kura. one other posibility ni kwamba inawezekana in sababu ya kuzuia upinzani sababu huyu mkuu inasemekana ana ubia kwenye hoteli hiyo hiyo. watu wa maeneo yale wanasema hivyo.
 
Date::7/11/2009

Kikwete apinga hoteli kujengwa mbugani

Na Peter Edson

RAIS Jakaya Kikwete amepinga hoja ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowasa aliyoitoa bngeni enzi za uongozi wake ya kutaka zijengwe hotel nyingi maeneo ya hifadhi za taifa.

Badala yake Rais Kikwete ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha kuwa inadhibiti ujenzi holela wa hoteli katika maeneo ya mbuga za wanyama.

Akizungumza wakaki wa uzinduzi wa hoteli ya kitalii ya Bilila Kempinsk yenye hadhi ya nyota tano katika mbuga ya wanyama ya Serengeti, Rais Kikwete alisema kama kutakuwepo na ujenzi holela wa hotel katika mbuga baadaye kunaweza kuleta athari kwa wanyama.

“Tunahitaji hoteli nzuri za kitalii zenye sifa na siyo kila mtu aje mbugani kujenga hoteli. Haitaleta maana yeyote, hivyo nawagiza ninyi Tanapa (Shirika la Hifadhi la Taifa) na wizara husika kusimamia vyema jambo hili,” alisema Kikwete.


Mwaka 2007, Lowasa aliwahi kulieleza bunge kuwa serikali inakusudia kuanza kujenga hotel kwa wingi katika maeneo ya mbuhgani kwa lengo la kuvutia watalii kutokana na ukosefu wa hoteli zenye hadhi nchini.


Alisema sekta ya utalii ni eneo muhimu katika ukuaji wa uchumi hapa nchini kwani katika kipindi cha mwaka 2007/2008 sekta hiyo iliweza kuchangia pato la taifa kwa asilimia 17.2 na kuingiza fedha za kigeni kwa asilimia 25, jambo ambalo halikuwahi kutokea huko nyuma.

Alisema kukamilika kwa hotel hiyo ni sehemu ya kutangaza utalii katika mbuga ya Serengeti nje ya nchi, hivyo ni vema wamiliki na wafanyakazi katika hotel hiyo wakafanya kazi kwa uaminifu ili kuvutia zaidi wawekezaji.

“Tutapokea watalii wengi katika hoteli hii, lakini hata sisi tumepata ajira kutokana na kukamilika kwa hoteli hii, msiiharibu, ipendeni ili nayo iendelee kuwalea,” alisema Rais Kikwete.
Alisema hivi sasa Serikali ipo katika mchakato wa kupunguza kiwango cha malipo kwa hati ya kusafiria kwa watalii kutoka asilimia 100 hadi kufikia 50 kwa mtalii mmoja, lengo likiwa ni kuondoa vikwanzo vinavyosababisha kupungua kwa watalii nchini hasa katika kipuindi hiki cha kuyumba kwa uchumi duniani.



Mwananchi Tanzania Newspaper(MCL)

Hapo sijaona dhamira yoyote ta dhati ya kuzuia ujenzi wa mahoteli mbugani, toafuti yake na EL may be ni presentation ya hoja yenyewe. Tafakari tena
 
Strategically, mbuga zetu inatakiwa ziwe pristine. Development yoyote ndani ya mbuga inatakiwa iwe highly sactioned. Hakuna sababu ya kuwa na mahoteli Serengeti, yajengwe Musoma na Arusha.

When necessary, inatakiwa walipe fees kubwa sana to keep only few and high value investors. Si suala la kuwa ameachiwa kwa sababu labda ni associate. Suala ni je ame meet standards?

Na lazima hizi standards ziwe juu sana na rais akilisimamia hili anafanya kazi yake vizuri na anastahili pongezi. Serengeti should be a different place!!
 
Back
Top Bottom