Kumbe jaji werema ni mwanachama wa ccm!

kanganyoro

Senior Member
Jun 22, 2011
127
33
Wadau nimetembelea site ya bunge na kukuta profile ya mwanasheria mkuu wa serikali jaji fredriki mwita werema kuwa ametokana na chama cha mapinduzi kupitia ex officio type of membership. Kwa ninavyojua katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania inazuia kwa mahakimu na majaji kuwa na uanachama wa chama chochote cha siasa wakiwa bado wapo katika utumishi wa umma. Na jaji werema bado ni jaji a mahakama kuu, hajastaafu. Leo akitolewa kwenye uanasheria mkuu anarudi kwenye kazi yake, na ninakukbuka alipoteuliwa kwa mara ya kwanza alisema bungeni kuwa yeye ni mwanasheria mkuu wa serikali, hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha kisiasa hapa nchini. Je leo bunge liweje limuandike kwamba ni mbunge anayetokana na chama cha mapinduzi. Je wadau huu si ndiyo uvunjwaji wa katiba? Je ni nani achukuliwe hatua?

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom