Kumbe inawezekana, India waandamana na kusababisha Bunge kusimamisha shughuri zake

matongo manawa

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
336
79
Wadau kituo cha tv ya magamba kimerusha taarifa saa mbili
usiku kuhusu maandamano ya kihistoria nchini India yaliyo
sababishwa na kukamatwa kwa mwanaharakati anayeheshimika
nchini humo,
Mwanaharakati huyo mwenye umri wa miaka 74 anapinga ufisadi
na amegoma kula mpaka serikali itakapokuwa tayari kuptisha
mswada wa kupambana na ufisadi.

Baada ya kukamatwa wananchi wa India ktk miji mkubwa mitatu
wamefanya maandamao makubwa na kupelekea bibi kiroboto
wa bunge la huko kusitisha shughuli za bunge.

Kazi kwenu watawala wa bongo,fungueni macho mnapoona
mambo haya yanatokea ninyi mnaendelea na sarakasi za
umeme na mafuta,kupora rasilimali km ardhi siku yaja hasira
za mbayuwayu zitawawakia nanyi mtajificha kwenye magamba
na gamba halitawasaidia.

Nivyema mkasikia vilio vya watu wenu ikiwa ni pamoja
na kupambana na ufisadi km wa meremeta,tangold,kagoda na ule unaofanana na wa jairo,pamoja na ufisadi mbaya wa
demokrasia ikiwa ni pamoja na ufisadi mliouanzisha bungeni
ufisadi wa kanuni na mwongozo wa spika.

Wakati ni huu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom