Kumbe hatuna wataalamu wa hili pia?

je swali linarudi pale pale bwana Undi mchupo; ni kweli kuwa hatuna arbitrators hapa Tanzania isipokuwa Marmo.

mimi ninajua wapo tu kwa habali nilizozipata kutoka kwa jamaa yangu. pia naona Mwehozi kanijibu kama nilivyotaka kufanya.

pia katika swala hili, wanasheria wamependelea sana hii kazi yaaniAlternative Dispute settlements.

hii inamaana kuwa unakuta mwanasheria kabobea katika shera za mikataba na aridhi, sasa anataka kuchukua hiyo. maana licha ya masomo ya fani hiyo, bado legal reasoning yaani jurisprudence inahitakiwa kama fani nyingine wanavyotakiwa kuwa na angalau Falsafa katika usuluhishi.

sasa jambo hili wanasheria wamekuwa wakiipendelea sana, na ndio maana ndugu yangu huyo, Yahaya hamadi alishangaa sana ( ref. to Mwehozi Supra).
 
The devil is always in the details.

Tunapoongelea wasuluhishi kama Marmo wapo tunaangalia mpaka kwenye level ya certification au mambo ya field aliyosomea tu?

Maana unaweza kuwa muhasibu na mwenzako muhasibu aliyesajiliwa na NBAA, vitu viwili tofauti kwenye kazi.
 
Fundi,

Kama serikali ni sehemu ya mkataba, na Tanzania kuna watu waliokuwa certified na vyombo vinavyoheshimika kimataifa, sioni kwa nini serikali isihakikishe kuwa katika vifungu vinavyohusu mizozo na upatanishi wasiweke wazi kuwa kukitokea mzozo basi msuluhishi lazima awe certified na chombo chenye heshima ya kimataifa.Uzuri ni kuwa kama tuna Watanzania wenye hizo certifications wata-qualify.Juhudi ziwekwe ku-define wasuluhishi kwa taaluma zao (e.g certification) na siyo kwa utaifa.

Tukifanya hivi, na kama mikataba inaandikwa vizuri, wawekezaji hawatakuwa na msingi wa kisheria kutoka kwenye mkataba kukataa msuluhishi kutoka Tanzania.Mara nyingi kutambua certification maana yake ni kumtambua mbeba certification, hiyo pia inakuja na kutambua neutrality yake.Unless ame-Kivuitu something in which case he should be immediately de-certified kama UDSM wanavyotaka kumvua degree Kivuitu.

Pundit, uko sahihi Mkuu. Kama nilivyosema awali kwa Tanzania chombo kinachoorodhesha maarbitrators wa mikataba ya ujenzi ni National Construction Council( Ofisi zake zilikuwa mtaa wa Mkwepu). http://www.intafrica.com/ncc/services.htmlKwa mikataba baina ya makampuni ya Tanzania mara nyingi kanuni zao ndizo zinazotawala na inawekwa hivyo katika mikataba. Kwa hiyo, kwa swali la msingi, arbitrators WAPO Tanzania. Mheshimiwa Marmo si arbitrator wa pekee Tanzania( Ingawa inawezekana yuko pekee aliyesajiliwa na institute iliyomsajili). Lakini tukiendeleza hoja, ni kuwa kwenye mikataba ya kimataifa, ambapo mhusika mmoja ni kampuni ya nje, mara nyingi kanuni zinazotumiwa ni za ICC ( International Chamber of Commerce). Kwenye hili, sina hakika kama kuna waTanzania waliorodheshwa nao kama arbitrators. Kama wapo, na mkataba unasema kuwa kwenye masuala ya disputes, utaongozwa na kanuni za ICC, serikali itakuwa na haki ya kumpendekeza arbitrator mTanzanzania mwenye utaalamu katika suala husika. Mathlani kama ni masuala ya ujenzi awe ni mtaalamu wa masuala ya ujenzi. Lakini taratibu za arbitration ni tofauti na mahakama. Ni muhimu katika arbitration kwa pande zote husika kukubaliana kuhusu arbitrator. Kwa hiyo upande wa pili wana kila haki kukataa pendekezo la serikali kama serikali walivyo na haki kukataa pendekezo lao. Ninavyofahamu, kwa ICC, kama pande zote zitashindwa kukubaliana, ICC wana haki ya wao kutoa pendekezo ambazo halitapingwa bila sababu za msingi. Mikataba yote ya kimataifa ni lazima iwekwe wazi kuwa endapo mgogoro au dispute itatokea ni kanuni za chombo gani zitafuatwa kutatua hiyo dispute. Nguvu ya serikali ni kuhakikisha kabla ya kusign mkataba chombo hicho ni kile ambacho wana imani nacho. Ukisha sign huna jinsi. Tatizo letu ni pale tunapo'negotiate' mkataba ni wagumu sana kusisitiza kuwa maslahi yetu yanalindwa. Hii ni pamoja na pale dispute zitakapotokea. Tunakimbilia mno utekelezaji na kudharau hatua zote za kabla ya utekelezaji at our cost. Tunaamini tu kuwa hawa hawawezi kutufanyia ubaya! Kinachotakiwa ni kuwa na wataalamu wenye uwezo wa kunegotiate mikataba na serikali yenyewe kuielewa mikataba hiyo barabara na nini ni wajibu wao kimkataba. Tukifanya hivi matatizo mengi yataepukwa. Tuwe na subira na tuweke muda wa kutosha wa matayarisho kabla ya utekelezaji. Panapotokea dispute ni vizuri kuhakikisha kuwa tunawahusisha wataalamu wa fani hiyo katika kuelezea position yetu na si kutegemea wanasheria pekee yao. Kwa vile mimi si arbitrator, mwenye la kuongezea anakaribishwa.
 
Back
Top Bottom