Kumbe bila migomo na maandamano haki hazipatikani???

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
Inasikitisha sana kuona baada ya mgomo wa madaktari uliosababisha baadhi ya watanzania kupoteza maisha yao pasi na hatia yoyote na wengine kuzidiwa na maumivu na wengine kulazimika kuingia gharama kubwa kupata tiba hospitali za binafsi hatimaye serikali imesikiliza kilio chao!! Kumbe basi hata sisi watumishi wa serikali wa sekta zingine tusitegemee kupandishwa mishahara, vyeo au kulipwa malimbikizo yetu bila kugoma, somo kutoka kwa madaktari limetuingia sasa kila mfanyakazi kwa eneo lake aangalie anachodai tuige mfano wa madaktari.Serikali yetu uwezo inao ila ni mpaka isukumwe kwa migomo na maandamano.
 
Back
Top Bottom