Kulima mafuta ya gari langu -ewura sasa basi

newmzalendo

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
1,378
550
Mafuta ya kuendeshea gari langu yanazidi kupanda bei. kwa wiki natumia elfu 70.kwa mwezi ni around 250,000. hapo sijafanya tripu za kutembelea nje ya dar ktk kusaka mashamba etc.nikipiga hesabu ya mwaka gharama ya mafuta tu ni around 4millioni ,EWURA watazidi kupandisha bei ya mafuta na shiliingi yetu itazidi kushuka thamani.ikifika 2012 bei ya lita itakuwa sh.2700.

Nimeamua kulima mafuta ya kuendeshea gari langu. kwani gharama ya kumlipa mtu alime miti ya kuzalisha Biodiesel kwa mwezi na chakula ni kama laki 2. kwa mwaka ni 2.5 mil. nitaweza ku control fuel prices bila kuiomba serikali ipunguze bei za mafuta.

Nafanya udadisi ni Nianze kulima mmea upi,kwa sasa nina Jatropha na Mawese.na hivyo vyote unavuna baada ya 3 years ,sijajua kama kuna mmea unaweza kuvuna ktk muda mfupi ili nianze kuvuna biodiesel shambani kwangu.
 
naomba miche na mimi nioteshe, niko serious
Mkuu KARIBU katika Timu bado sijaanza kupanda ,natafuta mbegu bora,unataka kupanda wapi?mimi nitapanda mkuranga 54Km kutoka Samora Avenue ya DAR.
 
Nina Acre kama 30 hivi,nakaribisha wabia ktk kulima zao hili.SIYO UMILIKI WA HIZO ACRES.kwa makubaliano rahisi tu ,tutashirikiana kupanda na kuvuna kwa matumizi binafsi.sehemu lilipo shamba kuna uwezekano mkubwa tu wa Kununua majirani.
Mkuu Malila wapi kuna mbegu bora za Jatropha.
 
Huku pwani inaitwa mibono kaburi, pale Mfuru mwambao niliwahi kuiona, ngoja nitamuuliza Tall aniambie kama zile mbegu bado zipo. Sasa akisema zipo utatoa bei gani kwa kila mche?
 
Mzalendo kabla ya kwenda chini zaid hebu kwanza tujuze ule mpango wako wakuwatoka TANESCO ulifaikiwa na kama ulifanikiwa tujuze ili nasi tukwamuke kwenye janga la kizahiki kisicho julikana hatmayake. pia huo mbadala wa dizeli unahitaji mitambo gani yakuyasafisha hayo matunda mpaka uweze kuyatumia kwenye gari? tunaomba ufafanuzi mkuu

PAMOJA INAWEZEKANA
 
Mimi naona sera za serikali ni tatizo kubwa mfano mimi nipo hapa Texas na ninalipa $55 kwa gari yangu ya US gallon 16 ambayo ni sawa na lita za Tanzania 60.56. Soko la dunia bei ya mafuta inafanana, usafirishaji wa hapo ni karibu sana na vyanzo vya mafuta ukilinganisha na sisi huku lakini tatizo ni kuna uizi hapo.
 
Gharama za processing umezingatia? Ninavyoelewa biodiesel sio bei nafuu kuliko diesel inayotengenezwa kutoka crude oil.

the US DOE was reporting average costs of B20 15 cents per gallon higher than petroleum diesel ($2.69/gal vs. $2.54/gal).[SUP][37][/SUP] B99 and B100 generally cost more than petrodiesel except where local governments provide a tax incentive or subsidy.
 
nawashauri kabla ya kuanza kilimo cha aina hii mfanye upembuzi yakinifu. kuna jamaa wapo masaki wanashughulika na zao la Jatropha.. nikipata contacts zao nitawapa
 
Mzalendo kabla ya kwenda chini zaid hebu kwanza tujuze ule mpango wako wakuwatoka TANESCO ulifaikiwa na kama ulifanikiwa tujuze ili nasi tukwamuke kwenye janga la kizahiki kisicho julikana hatmayake. pia huo mbadala wa dizeli unahitaji mitambo gani yakuyasafisha hayo matunda mpaka uweze kuyatumia kwenye gari? tunaomba ufafanuzi mkuu

PAMOJA INAWEZEKANA
Mkuu ule mpango wa kuwatoka Tanesco nilifanikiwa nusu-nusu.
1.Nilifanikiwa kutengeneza Wind-Mill.tatizo nipo Inner DAR upepo wa kusua sua.Usiku inacharge vizuri kuliko mchana.na Capacity ya kuendesha vitu kama friji ikawa issue kidogo.nilichofanya nimetengeza Power BackUp system.umeme ukikatika natumia Stored power kuwasha Taa,Feni na TV.
Sijakata Tamaa hivi Sasa ninaproject ya kufua umeme kwa Generator ya 5KVA kwa kutumia Vumbi la Mbao(Maranda) ambayo yanaweza kuendesha Internal Combustion Engines ,Technologia hii siyo mpya ilikuwepo miaka ya 1920's ila kwa sababu na HILA za kibeberu hii technologia ikawa suppressed na wazungu hawapendi iwe common knowledge ktk developing nations.Nikifanikiwa kufua Zaidi ya 5KVA ntaweka tangazo JF kwa ajili ya Expansion partnership.

Kuhusuu Bio-diesel.
Mr.Diesel alitengeneza Engine itumie mafuta ya mimea shambani,i.e Vegetable Oil.hivyo basi engine ya Diesel inaweza kutumia mafuta ya mimea bila wasi.Kuna Mitambo inauzwa ya kuchuja around dola elf3-5.ila kiubishi ubishi unaweza kutengeneza kwa kutumia mapipa ya liter200.nimepata data nyingi online na watu ambao tayari wanatumia haya mafuta.
Kwa ufanisi zaidi unayachuja mafuta kwa kumia Methanol unapata bio-diesel na Glycerine (ambayo unaweza kuweka manukato )ukauza kama mafuta ya mgando e.g Vasiline .
Matumizi yangu ya sasa ktk gari ni Lita 135 kwa Mwezi=283,500/- Ambayo ni around 3.4Mil kwa mwaka.nina hakika nikilima japo Acre 5 Tu.itatosha kukidhi mahitaji yangu ya mwaka na haitozidi 1.5mil na pia itakuwa mfano wa kuigwa TZ nzima kwani sitaki na sitoweka MSAADA WA SERIKALI WALA MSAAADA WA WATU WA MAREKANI. isitoshe TZ tumebarikiwa na Ardhi ya kutosha kila kijiji kikipanda hii mimea kando kando ya barabara baada ya miaka 10 tunaweza kupunguza matumizi ya Petrol-diesel by 30% wazungu wanajilinda sana na utegemezi wa mafuta ndiyo maana kuna msemo wa Energy Security.

Nilichojifunza kila kitu kinawezekana ilimradi uweke Effort za kutosha
 
Wakuu habari,mi huwa naperuz sana humu jf but mara 1 1 sana kupost.Kwanza nawashukuru wote kwa michango yen.Nimeshawishika kuwa mjasiliamali japo mtaj ndo ishu.Ila kwa kukusanya mawazo yenu nitakua na wide chance ya kuchagua.Pamoja JF
 
Mafuta ya kuendeshea gari langu yanazidi kupanda bei. kwa wiki natumia elfu 70.kwa mwezi ni around 250,000. hapo sijafanya tripu za kutembelea nje ya dar ktk kusaka mashamba etc.nikipiga hesabu ya mwaka gharama ya mafuta tu ni around 4millioni ,EWURA watazidi kupandisha bei ya mafuta na shiliingi yetu itazidi kushuka thamani.ikifika 2012 bei ya lita itakuwa sh.2700.

Nimeamua kulima mafuta ya kuendeshea gari langu. kwani gharama ya kumlipa mtu alime miti ya kuzalisha Biodiesel kwa mwezi na chakula ni kama laki 2. kwa mwaka ni 2.5 mil. nitaweza ku control fuel prices bila kuiomba serikali ipunguze bei za mafuta.

Nafanya udadisi ni Nianze kulima mmea upi,kwa sasa nina Jatropha na Mawese.na hivyo vyote unavuna baada ya 3 years ,sijajua kama kuna mmea unaweza kuvuna ktk muda mfupi ili nianze kuvuna biodiesel shambani kwangu.

Si lazima kutumia gari kama huwezi kuimudu gharama zake. Anza kutumia pikipiki, ikikushinda tumia baiskeli na public transport, ikikushinda tumia miguu na kuomba lifti, ikikushinda kaa nyumbani utulizane.

Watu ndio kwanza tuna negotiate kuleta ndege na hellicopters na ma hummer wewe unalalamika, uko dunia ipi wewe? kwani ulilazimishwa kutumia gari? Unanchekesha!
 
Binadamu kwa jinsi MWENYEZI MUNGU alivyotuumba tunapishana mambo mengi, mfano maumbile, vipaji, vipato, n.k. Kwa hivo kila mmoja atajikuna anapoweza, ingawa kutamani vitu vizuri ambavyo hatuna uwezonavyo ipo sana miongoni mwetu. Binafsi napendezwa na mtu anayeonyesha jitihada na ubunifu kwa kadri yake. Ulaya tunayoiona leo, pamoja na mambo mengine, ni mchango mkubwa wa wabunifu. Tuwape moyo, hasa vijana wajitume, kuliko kukaa vijiweni kupiga porojo za siasa wasizozijua.
B
 
faizafoxy ukweni haujaondoka tu?? bado mwali? duh..... enjoy tu incentive ndugu
 
Hii miti ya mibono mtaweza kuiendeleza?Kuna kampuni moja inaitwa Bio-shape ilinunua eneo la ekar kama 200 huko kusini katika wilaya ya Kilwa katika kijiji kimoja kinaitwa Mavuji! Hawa wazungu walifanikiwa kupanda hii mimea ila mwisho wa siku nasikia wamekimbia sasa sijui kama ni gharama kuihudumia au jamaa kuna vitu wakivitaka eneo lile na wamevipata wametambaa navyo
 
Binadamu kwa jinsi MWENYEZI MUNGU alivyotuumba tunapishana mambo mengi, mfano maumbile, vipaji, vipato, n.k. Kwa hivo kila mmoja atajikuna anapoweza, ingawa kutamani vitu vizuri ambavyo hatuna uwezonavyo ipo sana miongoni mwetu. Binafsi napendezwa na mtu anayeonyesha jitihada na ubunifu kwa kadri yake. Ulaya tunayoiona leo, pamoja na mambo mengine, ni mchango mkubwa wa wabunifu. Tuwape moyo, hasa vijana wajitume, kuliko kukaa vijiweni kupiga porojo za siasa wasizozijua.
B

Na haohao vijana tuwafunze kuwa kama huwezi kitu unachoweza ku "afford" ni bora kuachana nacho kwani ukilazimisha unaweza kuishia lupango.
 
Back
Top Bottom