Kulikuwa na tatizo gani wanyama kupelekwa Qatar?

Kawaulize maafisa wa Ikulu wa Jakaya Kikwete wakuambie ni kwanini sio tatizo kusafirisha wanyama maana wao ndio wahusika wakuu
Daaaaa!!!, huyo aende kwa kikwete? Huyo kazi yake ni kushinda lumumba tu kuwapokea wanene tu
 
Kuwapa Wafalme wa Uarabuni wanyama haina tatizo. Haya ni mambo ya Kidiplomasia. Yanasaidia kukuza urafiki baina ya Tanzania na nchi za Kiarabu.

Hamna mnyama kama Panda, hazaii ovyo na wapo wachache sana duniani. Lakini serikali ya China, inawapa marafiki zake wapendwa, Panda kudumisha urafiki. Wataalam wameita tabia hiyo " Panda diplomacy".

Tanzania kuna wanyama wengi. Hata kama wingine ni wachache kama tembo, kifaru au simba, wagaiwe kama itasaidia kuwachunga zaidi kuliko kuuawa Serengeti na majangili. Serikali imeonyesha kabisa haina uwezo wa kuwalinda wanyama kama tembo.

Panda wa Kichina wanapelekwa katika zoo katika nchi rafiki na China. Pia wataalam tofauti wanajaribu namna tofauti ya kuwazalisha, kuzidisha idadi yao.

Nimewaona wanyama kutoka nchi mbalimbali Ueno Zoo, Japan. Wanaangaliwa na wataalam kuliko huko Serengeti. Serengeti wanaua wanyama na wataalam wake.

Sioni sababu yoyote twiga au wanyama wengine wowote wasiuzwe au kugawa bure kwa jina la urafiki baina nchi mbili. Kila nchi hufanya hivyo.

Oman na UAE wanatoa misaada ya kila aina kwa Tanzania. Raia wa Tanzania wanakwenda kufanya kazi na kutembea huko bila kizuizi. Kama itasaidia kuendeleza urafiki huu kwa kuwapa au kuwauzia wanyama, sioni shida. Hasa kama itasaidia kukuza idadi yao kama tembo na kifaru. Twiga hawindwi kwa wingi, hana thamani kama tembo na kifaru katika masoko ya madawa Asia.

Kangaroo ni nembo ya Australia. Wanawapa nchi rafiki na kuuza nyama yake duniani kote.

Shida ni siasa tu. Tunapenda kuweka siasa katika kila kitu.

Serengeti itabaki kivutio cha aina yake duniani. Wanyama watazaliana kama kawaida yao. Serikali ikishindwa kuwalinda wanyama kama tembo na kifaru, watakwisha hata kama hawatakwenda nje ya nchi kukuza urafiki.
 
Unasahau kwamba hawa ni wanyama tu na si vinginevyo, na kati ya wanyama uliowataja hakuna mmoja ambaye yuko hatarini kutoweka siyo Punda milia, wala Simba, Twiga au Kiboko, hawa wanyama wako kwa wingi tu TanZania na ni rahisi sana kuwazalisha kwa wingi, wanyama ambao wako hatarini kutoweka wanajulikana kama vile aina fulani ya faru nafikiri ni faru weupe lkn siyo hawa wengine!

Unanifurahisha sana unasema kwani hawawezi kurudisha, urudishe Mnyama ktk Uarabuni wakati unaweza ukazalisha hata 500 leo hii ukitaka? Vipi hawa wanaopigwa risasi kwenye vitalu na Wazungu kila siku?
Ni nani alikwambia TanZania kuna uhaba wa Twiga au Tembo au sijui Simba?
Ulishawahi kufika mbuga za wanyama? Mimi nilishafika zaidi ya mara 8. Ni Tanzania gani hiyo unayoiongelea?

Ningependa kufahamu hizo njia za kuzalisha hao wanyama unazozizungumzia. Kwa hilo mimi niko ignorant. Ninachokijua akizaliwa panda mmoja kwenye zoo dunia nzima tuna pata hiyo habari.

Naona hii issue imekugusa on a personal level. Kama huamini observation yangu nenda wizara husika au nenda kwenye mbuga uongee na wale guides wenye umri mkubwa. Lakini kama unataka kuhalalisha kuuzwa wanyama wetu basi hapa kutakufaa maana ninachoona hapa ni timu fulani na timu fulani.

Si support uwindaji kama sport. Wazungu wanachotaka ni trophies, wanachokifanya wengi wao kulipia mnyama mmoja na kulipa guides wawawindie hao wanyama. Personally ngozi ya mtu hainibabaishi ninachojali kinachoendelea kichwani kwake na moyoni mwake.

Pale ambapo wanyama watavamia maeneo ya watu nakuhatarisha maisha, nasema bila kusita, wauwawe au vinginevyo wanavijiji kwa utaratibu utakaofaa wapewe dawa za kushoot hao wanyama na kuwalewesha.
 
Aisee nilijua Victor Wanyama mchezaji wa kimataifa wa Kenya , kapelekwa kucheza Qatar
 
Hivi yule twiga wetu ALBINO bado yupo? Nina wasiwasi, tutaambiwa aliliwa na akina Simba kumbe kishakwea pipa.
 
Kiukweli kisheria hakuna tatizo
sheria zipo wazi kabisa
anaetaka kubeba wanyama hai
anaruhusiwa mradi aombe kibali

kama hatutaki tubadili sheria
 
Ulishawahi kufika mbuga za wanyama? Mimi nilishafika zaidi ya mara 8. Ni Tanzania gani hiyo unayoiongelea?

Ningependa kufahamu hizo njia za kuzalisha hao wanyama unazozizungumzia. Kwa hilo mimi niko ignorant. Ninachokijua akizaliwa panda mmoja kwenye zoo dunia nzima tuna pata hiyo habari.

Naona hii issue imekugusa on a personal level. Kama huamini observation yangu nenda wizara husika au nenda kwenye mbuga uongee na wale guides wenye umri mkubwa. Lakini kama unataka kuhalalisha kuuzwa wanyama wetu basi hapa kutakufaa maana ninachoona hapa ni timu fulani na timu fulani.

Si support uwindaji kama sport. Wazungu wanachotaka ni trophies, wanachokifanya wengi wao kulipia mnyama mmoja na kulipa guides wawawindie hao wanyama. Personally ngozi ya mtu hainibabaishi ninachojali kinachoendelea kichwani kwake na moyoni mwake.

Pale ambapo wanyama watavamia maeneo ya watu nakuhatarisha maisha, nasema bila kusita, wauwawe au vinginevyo wanavijiji kwa utaratibu utakaofaa wapewe dawa za kushoot hao wanyama na kuwalewesha.

Tatizo ni kwamba mmekaririshwa sana mambo na Wazungu na mnashindwa kufikira nje ya kile Wazungu walichowafundisha!
Wanyama kama Tembo, Twiga, Simba n.k TanZania hawana hatari yoyote ile ya kutoweka na maadamu hawana hatari ya kutoweka basi hakuna tatizo lolote lile kuwauza kama export na kuongeza mapato ya nchi maadamu tu kunakuwa na uangalizi wa kutosha, kwa mfano hutokea mara nyingi sana huwa na Tembo wengi klk wanavyohitajika kwa mfano Afrika Kusini tembo wamezidi na sasa wanawafanyia uzazi wa mpango ili wasiendelee kuongezeka na wengine kupigwa risasi na wawindaji kuingiza fedha za kigeni, hivyo siyo ishu kihivyo, ila sema kuna wanyama ambao wako hatarini kutoweka kwa mfano Faru weupe hapo sawa hawa ni lazima kuwalinda!
 
Wanyama hai wanasafirishwa kinyemela now ya nchi
2ndege ya kesho la Qatar ndio imekuja kuwabeba violation of international laws
3biashara haramu
 
Siyo kweli Tembo ni wengi sana mpaka wanaharibu mazao na kuvamia makazi, na isitoshe ninaposema wanyama hawawezi kuisha namaanisha kwamba ni rahisi kuzaana kama ukiuza Twiga 50 nje ni rahisi kuzalisha Twiga 100 wengine, ni swala la mpangilo tu, ndio maana nashindwa kuelewa tatizo la kuuza wanyama nje kama bidhaa na kujipatia fedha za kigeni ambazo zinahitajika hapa nchini, liko wapi?
Daaah!! Umelewa nini?
 
Tatizo ni kwamba mmekaririshwa sana mambo na Wazungu na mnashindwa kufikira nje ya kile Wazungu walichowafundisha!
Wanyama kama Tembo, Twiga, Simba n.k TanZania hawana hatari yoyote ile ya kutoweka na maadamu hawana hatari ya kutoweka basi hakuna tatizo lolote lile kuwauza kama export na kuongeza mapato ya nchi maadamu tu kunakuwa na uangalizi wa kutosha, kwa mfano hutokea mara nyingi sana huwa na Tembo wengi klk wanavyohitajika kwa mfano Afrika Kusini tembo wamezidi na sasa wanawafanyia uzazi wa mpango ili wasiendelee kuongezeka na wengine kupigwa risasi na wawindaji kuingiza fedha za kigeni, hivyo siyo ishu kihivyo, ila sema kuna wanyama ambao wako hatarini kutoweka kwa mfano Faru weupe hapo sawa hawa ni lazima kuwalinda!
Wazungu wametufundisha nini?

Hao wanyama waliozidi huku kwetu ni wapi?
 
Hawa wanyama walitoroshwa,nchi haijanufaika.
ningependa Kama ungehoji mbona madini (dhahabu,tanzanite etc.) yanatoroshwa na watu hawapigi kelele kama hili la wanyama.
kama hadi jana Sakata hili ulikuwa hujalielewa basi nikushauri upende kujisomea,utakuja zomewa na watoto Wako bure
 
Tatizo ni kwamba mmekaririshwa sana mambo na Wazungu na mnashindwa kufikira nje ya kile Wazungu walichowafundisha!
Wanyama kama Tembo, Twiga, Simba n.k TanZania hawana hatari yoyote ile ya kutoweka na maadamu hawana hatari ya kutoweka basi hakuna tatizo lolote lile kuwauza kama export na kuongeza mapato ya nchi maadamu tu kunakuwa na uangalizi wa kutosha, kwa mfano hutokea mara nyingi sana huwa na Tembo wengi klk wanavyohitajika kwa mfano Afrika Kusini tembo wamezidi na sasa wanawafanyia uzazi wa mpango ili wasiendelee kuongezeka na wengine kupigwa risasi na wawindaji kuingiza fedha za kigeni, hivyo siyo ishu kihivyo, ila sema kuna wanyama ambao wako hatarini kutoweka kwa mfano Faru weupe hapo sawa hawa ni lazima kuwalinda!
Once upon a time, faru weupe walikuwepo kwa kiasi chake na sasa ni endangered species. Tokea mwanzo nilisema mimi sina list hiyo na bahati mbaya pia sifahamu ni wanyama gani waliouzwa Qatar zaidi ya twiga, ninachokijua mimi ni kwamba wanyama wetu mbugani wamepungua. Ujangili, uwindaji na utoroshwaji wa wanyama ni baadhi ya sababu zilizochangia upungufu huo.

Hawa wanyama ambao ni unique kwa Africa, ni urithi wetu na ni source of income. Ndio kinachowafanya watalii wa ndani na nje kwenda mbuga za wanyama kuona maajabu ya Mungu.

Na hao tembo wa Afrika kusini unaowazungumzia wamekuwa wengi kwa vile wao SA na Zimbabwe walikuwa serious na hiyo issue tofauti na sisi huku ambapo biashara ya wanyama pori inafanywa na viongozi wetu wa juu wa chama na serikali. Kwa maoni yangu walichotakiwa kufanya ilikuwa kutengua hizo sheria kabla ya kuendelea na transactions zao. Kwa vile sheria zilivunjwa basi tuache sheria ifuate mkondo wake lakini siyo kwa kuwaadhibu waliolazimishwa kusign documents. Tunamtaka mhalifu halisi.

Hayo ya wazungu nashindwa hata kucomment maana hata sielewi nimeunganishwaje nao.
 
Wala hapana tatizo Muungwana wale viumbe walipelekwa tu study tour na shopping kidogo natumaini watakuwa wamesha rejea, ah! wabunge kelele si ndio zinazo waweka ndani ya mjengo usijali,Vibali halikuwa tatizo kabisa na yule kijana wa kiasia sijui Kamlesh alisha waombea visa na hata yeye alipo hitajika mahakamani hakupatikana kutokana na umuhimu wa kwenda kuwa attend wageni wake muhimu,natumaini umepata msaada ulio kusudia.
 
Wewe jamaa huwa mbishi lakini hapa naona upo sahihi, kuwauza wanyama wetu nje sio issue, ni kama vile tunavyouza mifugo, lakini issue ni kama utaratibu unaofaa haukufuatwa inavyostahiki. Hapa Kenya kuna siku tumewauzia Wanyarwanda simba wetu.

Umuhimu wa kufuata sheria na taratibu inahakikisha idadi ya wanyama wanaobaki imetosha ili tusije uza wote.
 
Wanyama siku zote wanasafirishwa baina ya mataifa sababu ya mahitaji ya zoo na vyuo vya utafiti na pia ni moja ya njia ya kuwahifadhi hawa wanyama kwa kufanya utafiti na kuwafunza watu tabia na mzingira ya hawa wanyama na juhudi za kuwahifadhi zinazoendelea duniani.

Kuna wanyama duniani walipotea kabisa sehemu walizikuwa kwa wingi mfano Arabian Oryx lakini walikuwa wamebaki zoo Marekani na wakazalishwa na kurudishwa katika mazingira yao ya asili na sasa wanastawi sana.

Tupunguze kuingiza siasa na chuki kwenye kila kitu. Siasa nyingi = Umasikini wa fikra na maisha bora
 
Back
Top Bottom