Kulikuwa na tatizo gani wanyama kupelekwa Qatar?

Kuna jambo mpaka leo hii nashindwa kulielewa nalo ni hili la ndege ya Uarabuni kupakia Wanyama pori kama Twiga na wengineo na kuwapeleka kwao, swali langu tatizo lilikuwa wapi hapo?

Ni kwanini kulikuwa na kelele nyingi mpaka Bungeni?

Je, ni kwa sababu wanyama hawakulipiwa kodi au tatizo lilikuwa nini?

Mnaweza kunisaidia hapo?
Unajua maana ya maliasili?
 
Ile zoo ya dubai ilikua lazima ipate wanyama,na wanyama walitolewa toka nchi mbalimbali wakapelekwa huko,ila hapa ikawa kelele utadhani wamechukua makontena ya dhahabu,
nchi zinafanya hiyo biashara na si kitu cha ajabu
Kila nchi ina sheria na taratibu zake. Tuncholalama ni kwamba mambo yalifanyika gizani.
 
Mkuu, Twiga waliopanda ndege ni wale waliochorwa kwenye nembo ya ATC. Si twiga wa kweli. Waulize wenyewe watakufafanulia vizuri.
 
Kuna jambo mpaka leo hii nashindwa kulielewa nalo ni hili la ndege ya Uarabuni kupakia Wanyama pori kama Twiga na wengineo na kuwapeleka kwao, swali langu tatizo lilikuwa wapi hapo?

Ni kwanini kulikuwa na kelele nyingi mpaka Bungeni?

Je, ni kwa sababu wanyama hawakulipiwa kodi au tatizo lilikuwa nini?

Mnaweza kunisaidia hapo?

Pamoja na kwamba sheria hairuhusu kusafirisha nje wanyama hao, lakini pale inapokuwa lazima basi sheria na taratibu zote muhimu zizingatiwe kwa maslahi mapana ya Taifa, na sio kufanywa ki ujanja ujanja kwa manufaa binafsi ya watu waliopewa dhamana ya kuhudumu kwenye ofisi husika.
 
Kuna jambo mpaka leo hii nashindwa kulielewa nalo ni hili la ndege ya Uarabuni kupakia Wanyama pori kama Twiga na wengineo na kuwapeleka kwao, swali langu tatizo lilikuwa wapi hapo?

Ni kwanini kulikuwa na kelele nyingi mpaka Bungeni?

Je, ni kwa sababu wanyama hawakulipiwa kodi au tatizo lilikuwa nini?

Mnaweza kunisaidia hapo?
Naunga Mkono hoja ya kuongezwa hospital za Vichaa na Pia Naungana na Proff Ndalichako kwa kufuta ule upuuzi wa grades za Division for Secondary School.
Madhara yake ni kuwa na Kizazi cha watu kama wewe.

Iko hivi,Hakuna Sheria inayoruhusu Twiga Kuuzwa.
Full Stop
 
Kuna jambo mpaka leo hii nashindwa kulielewa nalo ni hili la ndege ya Uarabuni kupakia Wanyama pori kama Twiga na wengineo na kuwapeleka kwao, swali langu tatizo lilikuwa wapi hapo?

Ni kwanini kulikuwa na kelele nyingi mpaka Bungeni?

Je, ni kwa sababu wanyama hawakulipiwa kodi au tatizo lilikuwa nini?

Mnaweza kunisaidia hapo?
Kwa aliyetembelea mbuga miaka 30 iliyopita utaona tofauti na sasa hivi, wanyama walikuwa ni wengi. Makundi ya zebra, makundi ya tembo, nyumbu ndio usiseme, simba sio wakutafuta usiku na mchana. Miaka 6 iliyopita kwenye trip ya ngorongoro tulipishana na yale magari makubwa ya barafu tulipouliza wenyeji walituambia hao wanamzigo wa wanyama pori wanapelekwa Uarabuni Kama nyama.

Sina list ya endangered species, aliyekuwa nayo atusaidie. Inawezekana wako kwenye kundi hilo au kuna sheria zinazokataza. Na sio kila kitu unaweza kukiwekea thamani, vingine ni priceless. Thamani yake ni kubwa kuliko kiasi chochote cha pesa. Actually nilikuwa shocked kusoma hapa JF kwamba waliuzwa sh 1 point something million average bei inayolingana lingana na bei ya mbwa wa polisi.

Kwani hawawezi kurudishwa? Tutafute wanasheria wazalendo wasiokuwa na mikakati ya kupoteza kesi.

Sema nashangaa sana watu kureact na hiyo ya uarabuni peke yake na kufumbia humu JF.
 
Biashara ya wanyama tumeijua leo kuwa ni pato la taifa.
London zoo iliqnzishwa miaka 200 iliyopita hebu fikiria wakati huo wazungu walikuwa wanajichukulia tu wanyama, samaki, wadudu, mimea na maua bila kulipa chochote na bado wapagazi wanawabeba bure.

Kwa sasa wapo wanyama aina 756 waliotolewa sehemu tofauti duniani na kwa ujumla wapo viumbe 17,480.

London zoo ilianzishwa mwaka 1828

Tukiangalia upande wa mimea nilifika Royal Botanic Garden (1787) iliyoko Kew hapo kuna aina 1,040,426 ya mimea na yote hiyo imekusanywa toka sehemu zote duniani na Tanzania ikiwemo.

Ina wafanyakazi 750 wakiwemo scientists 250, wenye PhD 40, Honorary researchers wako 88 na inaongozwa na professors kutoka vyuo vikuu mbali mbali duniani ikiwemo Harvard.

Hivyo basi kuuzwa kwa wanyama na viumbe wengine isiwe hoja kubwa ila tujiulize tunafaidika na nini baada ya hapo? Na tumepoteza vingapi ambavyo hatujui? Kama mtu anachukua mbegu tu ya mmea na kwenda kupanda Kew garden na watafiti wote hao wa kimataifa wanafanya kazi hapo unafikiri wanaingiza ngapi?
Iwapo kiingilio tu ni £8 (28,000)
Think about it
 
Kwa aliyetembelea mbuga miaka 30 iliyopita utaona tofauti na sasa hivi, wanyama walikuwa ni wengi. Makundi ya zebra, makundi ya tembo, nyumbu ndio usiseme, simba sio wakutafuta usiku na mchana. Miaka 6 iliyopita kwenye trip ya ngorongoro tulipishana na yale magari makubwa ya barafu tulipouliza wenyeji walituambia hao wanamzigo wa wanyama pori wanapelekwa Uarabuni Kama nyama.

Sina list ya endangered species, aliyekuwa nayo atusaidie. Inawezekana wako kwenye kundi hilo au kuna sheria zinazokataza. Na sio kila kitu unaweza kukiwekea thamani, vingine ni priceless. Thamani yake ni kubwa kuliko kiasi chochote cha pesa. Actually nilikuwa shocked kusoma hapa JF kwamba waliuzwa sh 1 point something million average bei inayolingana lingana na bei ya mbwa wa polisi.

Kwani hawawezi kurudishwa? Tutafute wanasheria wazalendo wasiokuwa na mikakati ya kupoteza kesi.

Sema nashangaa sana watu kureact na hiyo ya uarabuni peke yake na kufumbia humu JF. Inaelekea kuna nyumbu wengi humu.

Unasahau kwamba hawa ni wanyama tu na si vinginevyo, na kati ya wanyama uliowataja hakuna mmoja ambaye yuko hatarini kutoweka siyo Punda milia, wala Simba, Twiga au Kiboko, hawa wanyama wako kwa wingi tu TanZania na ni rahisi sana kuwazalisha kwa wingi, wanyama ambao wako hatarini kutoweka wanajulikana kama vile aina fulani ya faru nafikiri ni faru weupe lkn siyo hawa wengine!

Unanifurahisha sana unasema kwani hawawezi kurudisha, urudishe Mnyama ktk Uarabuni wakati unaweza ukazalisha hata 500 leo hii ukitaka? Vipi hawa wanaopigwa risasi kwenye vitalu na Wazungu kila siku?
Ni nani alikwambia TanZania kuna uhaba wa Twiga au Tembo au sijui Simba?
 
Kuna haja serikali ikaangalia namna ya kuongeza hospitali nyingine ya vichaa maana naona Mirembe imezidiwa.
Ipo siku utakuja kituuliza hapa kuna tatizo gani Jecha kufuta uchaguzi wa Zanzibar.
Jamaa kauliza swali gumu lakini anajibiwa kirahisi rahisi sana, tatizo mimi sizijui vizuri sheria za Usafirishaji wanyama pori, hapo ndo palikua pa kujikita wakati wa kumjibu huyu jamaa.
 
Napinga uuzwaji wa wanyama nje bila ya kufwata sheria yaani kama kodi hazilipwi lkn kama kodi inalipwa sioni tatizo lolote kwani kati ya wanyama wanaouzwa hakuna hata mmoja mwenye hatari ya kutoweka wote wapo kwa wingi sana tu, kuzalisha Tembo wengi na kuuza siyo ishu hiyo ni kazi rahisi sana vile vile Twiga na wanyama wengine ni swala la kujua unauza wangapi na unazalisha wangapi basi, maadamu hauuzi wanyama ambao wana hatari ya kutoweka ambapo hapa kwetu siyo Tembo wala Twiga wenye hatari ya kutoweka TanZania!

Usisahau kwamba Wazungu kila siku wanapiga risasi wanyama wao kama Simba ya milimani huko Marekani, Bears Ulaya, zamani Ulaya kulikuwa na mabears Wazungu wakawaua wote kwa sababu walikuwa wanakula mifugo yao hata leo hii baadhi ya bear wanaanza kurudi Ulaya lkn Wazungu bado wanawapiga risasi kwa sababu hawawataki hata Panda Uchina inapeleka Panda Dunia nzima kila siku hata sisi tukitaka Panda leo Uchina watatupa na kuzalisha wengine, hivyo siyo big deal maadamu unaweza kuwa na rekodi unauza wangapi na wangapi wanazaliwa ambayo ni kazi rahisi sana!

Hivyo kwangu mimi siyo ishu kuuza wanyama kama bidhaa nyingine export na kujipatia fedha za kigeni maadamu tunajua tumeuza wangapi na kuzalisha mara mbili yake!

Kuuza wanyama kama bidhaa ingine ni tatizio, kumbuka kwamba, wanyama nao wanayo haki ya kukua katika mazingira waliyoyazoea, na sheria za animal conservation inakataza uuzaji ili kutoa nafasi kwa watu wasiowezakuwaona wanyama huko kwao, "ZOO".

Ni tofauti wakiuzwa na kukaa zoo, na wakiwapo katika hali ambayo ukiwaona wapo ki-asili, na wana-respond, wanaendana na mazingira, na pia wanasaidia evoulution ya mahala husika.

Hivyo bnasi, kama mtu anataka kuwaona, atatota fedha za kigeni, atasafiri kuja hapa nasi tutapata faida sisi na vizazi vyetu.

Wanyama wa mwituni wakibadilishiwa mazingira vitu vingi sana katika mifumo yao ya maisha pia vinabadilika ndo maana watetezi wa haki za wanyama duniani katika ulumwengu huu ulioendelea wanapinga kisheria kusafirisha hao wanyama.

Na pia, jambo lililotokea TZ lina alama nyingi za kifisadi ndo maana unaona wengi wana hasira wanapokujibu ndugu. Nafikiri nimechangia kwa ulewa wetu sote mkuu.
 
Nijibu swali moja, wanyama kama Simba,Tembo, Punda milia, Faru, Mamba, Twiga na wengineo walifikaje kwenye mazoo Ulaya, Marekani na Asia kama kuwasafirisha kulingana na sheria za kimataifa kama ulivyosema ni kosa?

Afrika Kusini kuna ma Zoo yana Bear ambao siyo wanyama asili ya Afrika bali ni Ulaya na Marekani, je walifikaje AK?
 
inamaana wewe hujui kabisa madhara ya kutoa rasilimali za nchi! hujui kabisaa na huoni tatizo? think twice men!
 
Kila mahali unang'ang'ania kuzalisha kuzalisha umekuwa mkunga wewe? C2PD Kumbuka kuna wanyama wengine kuzaana kwao ni mbinde mfano Faru. Hata tembo uzazi wao unachukua muda.
 
Kuna jambo mpaka leo hii nashindwa kulielewa nalo ni hili la ndege ya Uarabuni kupakia Wanyama pori kama Twiga na wengineo na kuwapeleka kwao, swali langu tatizo lilikuwa wapi hapo?

Ni kwanini kulikuwa na kelele nyingi mpaka Bungeni?

Je, ni kwa sababu wanyama hawakulipiwa kodi au tatizo lilikuwa nini?

Mnaweza kunisaidia hapo?
Tatizo ni kuwa viongozi wa ccm waliwaiba hao wanyama na kuwauza kinyemela majizi wakubwa
 
Back
Top Bottom