Kulikuwa na haja ya kumtimua Kafulila NCCR? Mh. Moses Machali Live on Star TV

Sasa turudi kwenye hoja ya leo, hilo la Kafulila bado mbunge halipingiki.

Tusipoteze muda kujadili hilo.
 
SWALI LANGU:

Katika kumfukuza kafulila katiba ya NCCR Mageuzi imeeleza nini kuhusu hilo? Pia mhe Machali atueleze vipi Mhe kabwe anahusika na mgogoro huu.
Kanuni za NCCR zinaorodhesha makosa zaidi ya kumi, yapo ya kutimuliwa moja kwa moja, matharani kutoa siri za chama, kukashifu uongozi kwa kashifa za kizushi, nk. hayo kafulila aliyafanya. Laiti watu wangesoma kanuni hizo na kuona orodha ya makosa ya Kafulilia.

Aidha, mwenyewe alikiri kufanya makosa hayo
 
Huyu dogo ndio anasoma Saut Mwanza?
Profile yake kwa kifupi hii hapa!

Degree: BA Education, st Augustine University 2010.
Secondary: Newman Sec School ila centre yake ya mtihani ni Kigoma Sec mwaka 2006 (adv level).
College: Kasulu teaching college na kabla ya kuwa mbunge alikuwa Mwalimu wa Kigoma Pr School.
 
Watanzania hatujazoea maauzimu magumu kama hayo, tumezoea mtu akikosa anaamishiwa pengine.

SWALI LANGU:

Katika kumfukuza kafulila katiba ya NCCR Mageuzi imeeleza nini kuhusu hilo? Pia mhe Machali atueleze vipi Mhe kabwe anahusika na mgogoro huu.


MAONI YANGU:

Dawa pekee ya migogoro hii ni katiba mpya ya kuruhusu mgombe binafsi
Huyu mgombea binafsi atasolve vipi inshu kama hii ya Kafulila kama Mbunge atakuwa kagombea kwa tiketi ya chama?
 
Kama tutatumia kanuni ya kanisa katoliki basi ingekuwa vyema sana. Kanisa linasema ni bora kubaki na muumini mmoja safi kuliko kubaki na waumini kumi wachafu.

Kufukuzwa kafulila ni halali kama hafuati utaratibu wa mahala husika.

Hata mkeo akienda tofauti na kanuni za nyumbani lazima mfikie kwenye mjadala na mkishindwa basi lazima kila mtu ajue njia yake.

Kila mahala pana taratibu zake, iwe nyumbani, ofisini, popote pale. Kwanini liwe tatizo?

Hapa lazima tujifunze kuwa David ana tatizo aliondokaje chadema?

Baruan anasema CCM ilianza haya na baadae wengine wakadandia. Hii si kweli kwani CCM ina mauzauza mengi sana lakini haina ujasiri wa kuwachukulia hatua kwani wao wote ni wachafu. Usitake kulinganisha CCM na vyama vingine, chini ya JK haiwezi kumchukulia hatua mwananchama wake yeyote.
 
Vyama haviruhusiwi kufukuza wanachama wake? Kama vinaruhusiwa nini kosa la NCCR Mageuzi kumfukuza Kafulila na watu wengine?

Hili Swala la gharama linakuja kwa Kafulila tu? Hivi Tunataka kuwa na wagombea binafsi Wasiokuwa na nidhamu tu kuogopa vyama kufukuza wabunge?
 
Yahya,

Inaonekana kuna tatizo kubwa sana la kutafsiri ama kuelewa matakwa ya order ya mahakama.

Kama Danda anasema Kafulila na wenzake katika maombi matatu, ya kwanza aliiomba mahakama kuu isitishe ''implementation'' ya maamuzi ya NEC ya NCCR Mageuzi, sasa anasemaje tena kwamba wao wamezuiwa kuchua hatua zaidi? Navyoelewa mimi walizuiwa kuimplement (kutekeleza) maamuzi ya kumvua uanachama.

Labda tumpate mwanasheria atusaidie kufafanua order ya mahakama inasemaje!
 
Katika tuhuma za Kafulila, anamtuhumu Kahangwa kwamba naye ni mamluki chamani, Kahangwa huyu wa hapa JF.
 
Mh. Machali, baada ya kumfukuza Kafulila, mmejiandaaje kichama kulikomboa jimbo la kasulu kusini? Je mtaji aliokuwa nao Kafulila unadhani ni wa NCCR au wa kwake David mwenyewe?
 
Tuwe wakweli tunapojadili mambo haya ya vyama. Nasubiri kuona siku CCM itakapomfukuza member wake kama nyie Star tv mtajadili haya.
 
je ZITTO KABWE anahusika vipi na mgogoro wa DAVID KAFULILA NA NCCR MAGEUZI?

alijihusisha mwenyewe kwa kupiga simu polisi wakati wa kikao cha halmashauri ya NCCR, akawataka waende kuvunja mkutano huo. Labda nia yake ilikuwa kumwokoa rafiki yake asitimuliwe
 
  1. Kuongea mambo ya chama nje ya chama
  2. kumtukana m/kiti kuwa ni CCM ( Kumbe hili ni tusi )

Je haya kweli ni makosa ya kimsingi ya kumfukuza uanachama ????
 
Nimekosa mbele ya mungu na mbele yako baba ninaomba radhi kwa niliyoyafanya baba'. .... ?!
 
Mhe.manchali siku moja ulisikika kwenye vyombo vya habari ukisema kuwa kama hao jamaa wakipata nafasi ya kuongoza chama ( Mhe.Kafurila na wengine nwalioondolewa uanachama) wange pata nafasi ya kuongoza chama ww unge acha siasa na kuwa mwanaharakati na mara zote umekuwa ukiunga mkono hadharani kuondolewa uanachama kwa Mhe.kafulila na wenzake kitendo ambacho kinatofautiana na mwazo ya vijana wengi wakiwemo waheshiwa wabunge kama Zito kabwe.

Je, ni vitendo gani hasa walicho kukela wanachama hao hasa kafulila?Wakati huu ukumbe umekuwa ukiunga mkono hoja na misemo ya za Kafulila ikiwa ni pamoja na kuita serikali ya ccm ni legelege.

Pili, nini maamuzi yako kama Mhe.Kafulila atarejeshewa uanachama na viongozi wa chama chenu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom