Kulikuwa na haja ya kumtimua Kafulila NCCR? Mh. Moses Machali Live on Star TV

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Greetings wanaJF

Awali ya yote nichukue fursa hii kuungana na wanaJF wote, familia ya marehemu Regia Mtema na watanzania walioguswa na msiba wa mpiganaji na mwanaforum Regia. Binafsi ulikuwa msaada kwa changamoto na mawazo yako mengi inbox katika kuboresha Kipindi chetu cha TUONGEE ASUBUHI R.I.P Regia.

Tutaendelea kuenzi na kuthamini mawazo yako mema.

Katika Kipindi cha Leo tutakuwa na fursa ya kupata maelezo ya upande Mmoja wa sarafu kuhusu Wimbo la kufukuzana katika vyama na safari hii mgeni wetu ni katibu mwenezi wa NCCR Moses Machali (M) Kama tulivyoahidi JUMAPILI iliyopita.

Muulize Maswali na tutayasoma kwa kadiri muda utakavyoturuhusu
 
Je, ni kweli JAMES MBATIA anatumiwa na CCM kuivuruga NCCR na upinzani kwa ujumla ili kukipa chama cha ccm nguvu zaidi ambapo sasa ccm imepoteza mvuto kwenye jamii? Je tuamini kuwa kwa sasa nccr ni Ccm C?
 
Yahya,

Star tv matangazo yenu yanakatakata huku kigoma vijijin, mfano taarifa za habari kwanini?

(Swali hili ni nje ya mada lakini)
 
Yuko Upande upi ndani ya Bunge? Ule wa kambi ya Upinzani au wa Chama tawala?

Maana wakati CHADEMA wanatoka nje Bungeni wewe ulibaki ndani na Zaituni Buyogela, tukajua upo upande wa CCM sasa kuna Muda unauponda Utawala wa CCM, tupe msimamo wako!
 
Mh. Machali, kuna kauli yako yenye utata uliwahi kutoa hivi karibuni, ulidai kuwa endapo Mbatia angevuliwa uanachama na wewe ungekihama chama.

Sasa: Je, wewe upo NCCR kwa ajili ya Mbatia au Katiba ya NCCR?
 
Wakati wa UCHAGUZI mdogo (RORYA) kata ya Mkoma ambapo CHADEMA ilikuwa na Nguvu wewe (MACHALI) na Mbatia mlienda kupunguza nguvu ya CHADEMA japo mlijua hamtashinda na kulikuwa na kata Nyingi. Je, KWELI hamtumiwi na CCM?
 
Wadau wa Murufiti, nyansha, kidyama, heru juu, kabanga na mhunga, wanakusubiri uje uwaeleze nini agenda zako ndani ya NCCR.
 
Nawapongeza NCCR kwa kusimamia katiba. Kafulila ni mtovu wa nidhamu. Haiwezekan umkejeli mwenyekiti kuwa wewe ni maarufu kuliko mwenyekiti"hata kama kuna ukweli".

SWALI: Mahakama imemrudishia ubunge Kafulila, nini msimamo wa chama?
 
Rest in peace Regia Mtema.

Machali unazungumza kwamba Mhe. Kafulila alikuwa mbunge wa Kigoma kusini, ilhali mahakama imeshasema aendelee na kazi zake za kibunge na kutupilia mbali maamuzi yenu (ya kibwege) ya chama, unatoa wapi huo ujasiri wa kupinga amri ya mahakama?
 
Rest in peace Regia Mtema.

Machali unazungumza kwamba Mhe. Kafulila alikuwa mbunge wa Kigoma kusini, ilhali mahakama imeshasema aendelee na kazi zake za kibunge na kutupilia mbali maamuzi yenu (ya kibwege) ya chama, unatoa wapi huo ujasiri wa kupinga amri ya mahakama?

naam hasan,ya Kibwege hasa
 
Kuna tuhuma kuwa Wajumbe walio hudhuria kikao hicho walikuwa mamluki yaani hawakuwa halali, wasemaje kuhusu hili?
 
Mhe. Machali kuna taarifa kwamba uliwahi kuugua kichaa, ukiwa na umri kati ya miaka saba hadi kumi, na jinsi unavyoongea hapo tunathibitisha maneno hayo, je kuna ukweli juu ya tuhuma hizo?
 
Ikiwa dhahiri kiongozi wetu mkuu wa chama anaonekana kuwa ktk mlengo si wa kimageuzi, na kupitia nguvu yake chamani kumvua uanachama wake.

Je, kauli ya Mbatia lazima avuliwe gamba ni kosa linaloweza kumfukuza? Ikiwa kauli kama hizi ni kauli tulizozizoea kwa vyama vingine vya siasa, je hii NCCR-Mageuzi ni kwa maslahi ya taifa au ya kundi fulani linaonesha wazi mnamtumkia mwenyekiti? Issue sio mwenyekiti kushindwa ubunge ila kuonesha si mwanamageuzi wa ukweli.
 
Machali umekaririwa mara kadhaa kwenye vyombo vya habari ukidai kwamba kama Mbatia angevuliwa uenyekiti basi ulikuwa tayari kuhama chama. Pia umekaririwa mara kadhaa ukidai kwamba huwezi kubaki ndani ya NCCR Mageuzi endapo Kafulila angefanikiwa kuwa mwenyekiti wa chama.

Je, upo NCCR Mageuzi kwa sababu ya Mbatia ama kwa sababu ya sera na itikadi zake?

Je, kutokuwa tayari kuongozwa na Kafulila ni dalili za majivuno, ni dharau ama kutokujua unachokifanya?

Je, kuvuliwa uanachama kwa Kafulila ni katika jitihada za kuona kwamba nafasi ya uenyekiti wa Mbatia inalindwa kwa gharama zozote?

Je, hakukuwa na adhabu nyingine ya kumpa Kafulila zaidi ya kumvua uanachama?
 
Mh Machali

1. Kwa maono yako mwenyewe unadhani kufukuzwa kwa Kafulilia na wenzake ndo mwarobaini wa migogoro katika NCCR?

2. Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikimhusisha mh zito katika mgogoro uliyopelekea kufukuzwa kwa Kafulila na wenzake, unalisemaje hili?
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom