Kulikoni TBC haiendeshi vipindi juu ya mswada wa katiba mpya kama itv, star tv!

JOB SEEKER

Senior Member
Aug 1, 2011
145
33
Wana JF,Nimekuwa nikifuatilia vipindi mbalimbali juu ya mswada wa katiba mpya katika television vinavyowakutanisha makundi mbalimbali ya jamii kama vijana,wazee,wanawake ,watoto wenye umri na taaluma tofauti wenye kutoa michango iliyobeba mawazo na mitazamo tofauti yenye nia na lengo la kujenga mswada wa katiba mpya.Lakini sijawahi kuona vipindi kama hivyo juu ya mswada wa katiba mpya vikionyeshwa na television ya taifa (TBC), ni kwanini ? na kwa mamlaka ya nani wana fanya hivyo? Hichi ndicho chombo kinacho wafikia watanzania wengi kwa ujumla na kwa wakati mwafaka, Je ! tujiulize swala la mswada wa katiba mpya halina maslahi kwao kama vipindi vya miaka 50 ya uhuru!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kwanini wenzao kama ITV,STAR TV, wanaweza kukidhi maslahi ya watanzania lakini wao washindwe, Je !! maslahi ya taifa yana maslahi gani na maana ipi kwao??? Job Seeker.

 
hehehehehe mleta uzi umesahau tena kuwa tbc ni gamba ++
kuliko waonyeshe habari za midahalo ambayo wanauhakika
inapingana na sirikali bora wamuonyeshe king majuto
 
wamelewa madaraka ,,vyombo kama hivi inabidi visifungamane na siasa kabisa viwe free bila hivyo kutakuwa hakuna la maana zaidi ya blah blah
 
Ni kwanini TV channels za bongo zinaboa?????? Hakuna mwenye afadhali yaani zote hovyo, Kisiasa na maslahi ya nchi ITV inaongoza.
 
Back
Top Bottom