Kulikoni Tanzania Daima online?

Mlalahoi

JF-Expert Member
Aug 31, 2006
2,182
883
Pengine post hii hapa si mahala pake.If so,inaweza kuhamishiwa kunakostahili.Kwa sie tulio mbali na nyumbani,machapisho ya magazeti yetu katika mtandao ndio tegemeo letu kubwa (of course,JF ni tegemeo kubwa zaidi).Hata hivyo,vyombo vya habari vingi vya TZ vimekuwa vikitupuuza wasomaji wao wa mtandaoni hasa katika ku-update habari kwenye tovuti zao.

Tanzania Daima walikuwa wakijitahidi sana ku-update habari kwenye tovuti yao. Lakini hali imebadilika katika siku za hivi karibuni.Habari zilizowekwa Ijumaa iliyopita hazijabadilishwa hadi leo.Kama kuna matatizo ya kiufundi ni vema webmaster akaweka tangazo pale.Maana kwa sasa freemedia.co.tz haina tofauti sana na newhabari.com.Bora wenzao wa Uhuru walioamua kupotea kabisa hewani.

Nategemea kuna members wenzetu hapa JF ambao kwa namna moja au nyingine wanaweza kuwaamsha Freemedia.Tatizo kubwa linalotawala mentality ya wamiliki wa vyombo vya habari huko nyumbani ni kwamba online versions za magazeti ni sawa na kuuza gazeti bure.
 
Hasa juzi Jumamosi nilisikitika mno mkuu,kukosa safu ya Maswali magumu ya Ansbert Ngurumo na makala za akina Pascal Mayega.samsom Mwigamba,padri karugendo,Ndimbwaga,Mobin,Mwanakijiji,mpayukaji, na wenineo kama akina Irene Mark.Duh,nilisikitika mno.
 
Au kuna ufisadi unafanyika kutunyima habari?
 
Back
Top Bottom