Kulikoni star tv siku hizo hawarushi bunge live?

mchaichai

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
648
76
Star tv ilikuwa na imeendelea kuwa tv ya kurusha mambo ya kitaifa live lakini cku za hivi karibunu naona kama imejitoa kabisa kurusha habari za bunge...ni sababu za kibiashara au kisiasa anayejua kisa na mkasa atujuze...Tv zingine tunajua cyo huru kwani wenye nazo wanauma na kupuliza sitaki hata kujua sana habari zake...Tbc waipatikani kila mahali cc tulitegemea zaidi star tv
 
ah ah walizidisha maswala ya M4C...sasa serikali ikawabania kurenew mkataba na kuwapa mlimani tv
 
Na ni radio gani inayorusha matangazo ya bunge live ,kwa mie dreve tax ingenifaa sana
 
wakubwa may be washachakachua..kulikua kuna kampango ka kuvibania vyombo vya habari vya sahara communications kwa sababu vimechangia kwa kiasi kikubwa kuporomosha umaarufu wa ccm kanda ya ziwa..huezi jua maybe kampango kashaanza kutekelezwa
 
Wana JF naomba mnisaidie bunge limeanza hakuna tv inayoonyesha live kama zamani kulikoni? Tunahitaji democracy ya kweli na transparency kwa wa tz wote. Je kama kuna mabadiliko nijulisheni mbona kimyakimya kama ndiyo hivyo 2015 mchakato majimboni kipindi kitakwepo kweli? Maana kinatusaidia kujua uwezo wa wagombea majimboni hata kama haushiriki mikutano au tupeleke hoja binafsi? Au linahitaji katiba mpya? Kama wanazuia kwa masilahi ya nani? Nawasilisha.
 
Hiyo ndo ccm bana wamewanyima!
Ee Mungu saidia ccm iendelee kufa! Wanatuwekea kupitia tbc ccm yao isiyoeleweka! Wanaona star tv inafika mno mbali, wao wanaona watu wengi wataona jinsi wabunge wa ccm wasivyojua kitu. Eti wamewapa mlimani ambao wanaishia hapo magomeni!!
 
Yamkini Dialo kaona hakuna dili tena na ubunge kaukosa vipi wengine wauze sura kwenye tv yake, au ni system ata work si unajua Tv zinavyoiumbua thithi em
 
Star TV ilikosea kuwaonesha akina ****** wakiuchapa usingizi (wakitafakari) kwa hiyo wamekula Ban kimyakimya!!
 
Hizo zote ni tetesi ila wenye taarifa kamili kuhusu startv kutoonyesha bunge ni nini atujuze as grt thinkers.
 
Back
Top Bottom