Kulikoni Singida hakuna mwakilishi baraza la mawaziri?

Naheshimu sana mawazo yako lakini unapaswa kuheshimu watu wengine pia kabla hujatoa mawazoyako, unaposema singida hawana ushawiashi wa kuingia kakatika siasa umetumia kigezo gani hebu fafanua tafadhali,

paul: kuna wasomi wengi singida mbona hawajitokezi kugombea nafasi za siasa? na hao wachache wanaojitokeza mbona basi hawapati? fanya utafiti uone watu waliojitokeza wasomi 2005 lakini wakshindwa? tatizo ni nini?

kufanya uchaguzi kila mara hilo sio sababu kuwa na ushawishi , kinachotakiwa je wanachangua right person ? angalia kwa mtazamo huo wala mimi sina nia mbaya na watu singida



Right person what, do u mean? Nilikua sijui kama wabunge wa singida sio right person
 
Nilipata fursa ya kumuuliza mh. JK kwa nini mkoa wa Singida hauna mwakilishi kwenye baraza lake la mawaziri? zaidi ya John chiligati na ambaye siyo mzawa wa mkoa wa Singida? jibu: "we bana vipi? wabunge wengi wa singida elimu yao ni kidato cha nne unategemea mtu kama huyo umpe uwaziri afanye nini ?"

Hivi mtu mwenye elimu ya kidato cha nne hawezi kuongoza wizara kwa sababu ya kiwango chake cha elimu?

Jibu: HAWEZI
simple and clear! It requires a certain level of the ability to manage and also the know how! Unless uwe na experience kibao ya ku-manage watu na multiple tasks...ambazo kwa mtu wa kidato cha nne ni shughuli.
 
Nilipata fursa ya kumuuliza mh. JK kwa nini mkoa wa Singida hauna mwakilishi kwenye baraza lake la mawaziri? zaidi ya John chiligati na ambaye siyo mzawa wa mkoa wa Singida? jibu: "we bana vipi? wabunge wengi wa singida elimu yao ni kidato cha nne unategemea mtu kama huyo umpe uwaziri afanye nini ?"

Hivi mtu mwenye elimu ya kidato cha nne hawezi kuongoza wizara kwa sababu ya kiwango chake cha elimu?

Mohammed Dewji graduate,chiligati graduate,Nyalandu Masters,martha mlata nadhani atakua amemaliza masomo uk shahada ya kwanza,

Sio jibu sahihi hili! Lakini ume-prove Rais kadanganya! au yupo mis-informed? Sasa sijui kipi bora..hahaha
 
Sio jibu sahihi hili! Lakini ume-prove Rais kadanganya! au yupo mis-informed? Sasa sijui kipi bora..hahaha



Nafikiri mtoa mada alikua anatania hii thread ilitakiwa iende kwenye jokes. hata hivyo nilikua najaribu kumonyesha wapo graduate.lakini je mikoa yote imetoa mawaziri hadi aulize singida ambayo inaye waziri tayari.au alitaka kuonyesha wabunge wa singida sio wasomi
 
Hii mada imekaa kibaguzi usimwone kwenye jukwaa lingine aanze kuuliza singida kuna wabunge wangapi waisilamu , mara udsm kuna wanafunzi wangapi toka singida
 
Hii mada haina tija. Tukifika hatua ya kuchagua/kuteuwa viongozi au kukataa viongozi eti tu kwa misingi ya kabila, jimbo, mkoa au kanda ambayo mtu anatoka ni kufilisika kimawazo na kuitakia nchi balaa la ukabila na umajimbo kama Kenya. Whether kuna waziri au hakuna waziri anayetoka mkoa wa Singida ni irrelevant. Nyerere alituasa sana kwenye jambo hili.
 
Nilipata fursa ya kumuuliza mh. JK kwa nini mkoa wa Singida hauna mwakilishi kwenye baraza lake la mawaziri?

Mkuu...kwani siku hizi uwaziri ni kama ubunge kwamba kila mkoa lazima utoe waziri(mawaziri) au kuna majimbo ya uwaziri?

tufahamishe mkuu...inawezekana tupo mijini humu lakini hatujui kinachoendelea.....
 
Jamaaa katupuuza sana sisi watu wa Singida! Yaani umasikini kwetu ni kitu cha kwaida! Haya ndugu umeamua kuusemea ovyo mkoa wetu, kwa hoja isiyo na maana kabisa. Naipenda Singida kama niipendavyo Tanzania.............Natamani Tundu Lissu achukue form kugombea ubunge Singida Kusini....ninaahidi kurudi nyumbani kumpigia campaign na kura pia.
 
Back
Top Bottom