Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 59,146
- 79,300
Wajameni kama ni wafuatiliaji wa mrengo wa haya magazeti mtagundua kubadilika kwa ghafla mtazamo wao kuhusu hali halisi ya Ufisadi katika CCM. Kulikoni? wadadisi wa mambo wanasema Matokeo ya kesi ya Dowans ndiyo inasababisha haya; katika kupumbaza Watanzania aka Wadanganyika magazeti haya yameanza hata kujinyooshea vidole yenyewe katika kile kinachoitwa kuchanganya watu katika agenda ya siku au wataalam wanaita (story/agenda of the day)! Ningependa kama wangejikita zaidi katika suala la Hukumu ya Dowans na sio janja iliyoratibiwa katika kupoteza mawazo ya Wadanganyika na fujo za uchaguzi wa Mameya zinaofanywa kinguvu kwa kutumia jeshi! Tunaona hata Lowassa anakaripiwa ilhali tunajua nguvu yake na uhusiano wake wa Dowans huu ni usanii tunachezewa kwa remote control sasa! Amkeni nani mmiliki wa Dowans?