Kulikoni Mzee wetu Aboud Jumbe

Hii kali ya kufungia mwaka 2010, viagra na kahawa! Uongo mwengine hauna hata mwelekeo jamani.

kama muungwana alivyosema huko juu mkuu, usipende kusema ni uogo tu kwa sababu hujakipenda kilichoandikwa, we toa sababu kuonyesha ni the other way around vinginevyo unataka kuleta ubishani usio na tija! kwani kutumia viagra kwa mtu mzima kama yule ni ajabu? alikufa gen.sani abacha kwa viagra tena sio kwa mkewe kwa hooker wa kirusi itakua yeye bana! mda aliotangazwa kafa ni mida flan ya ndio kwanza watu wanaenda kulala na pia hadi anaenda kulala alikua mzima kabisaaaaa!
 
Julius alikula kiapo cha kuilinda Katiba ya JMT. Na Jumbe pia. Kumbuka Jumbe ndiye alikuwa kinara wa kuunganisha ASP na TANU kuanzisha CCM. Alikuwa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM. Hivyo Jumbe alipoanzisha hatua za kuuvunja Muungano kinyemela ilibidi aadhibiwe. Tunataka Rais anayesimamia na kulinda Katiba ya nchi kwa dhati na si kuuona Muungano unachezewa halafu anachukulia mambo kirahisi.
 
Hii kali ya kufungia mwaka 2010, viagra na kahawa! Uongo mwengine hauna hata mwelekeo jamani.

Mkuu hapo hakuna uongo. Kumbuka kuwa Kahawa inasababisha mapigo ya moyo kuwa juu, hii ni kweli na haipingiki. Halafu tena viagra ni kiboko kwa mapigo ya moyo, ndiyo maana unashauriwa kabisa uzingatie kipimo kwa kuzingatia umri, uzito, magonjwa hatarishi kama kisukari, blood preasure, etc. Sasa basi kwa umri wa mzee wetu yule marehemu halafu uchanganye kahawa na viagra kwa hakika ni umauti. Siamini kama mjumbe aliyesema hili atakuwa ametunga. Kumbuka kile kifo, hakikusemewa sana!!! Hukujiuliza kwa nini?

Kuhusu Mzee Jumbe hicho ndicho kifungo chake cha maisha ndani ya makazi yake. Alijengewa nyumba ile na serikali na kutengwa kabisa na wazanzibari ili kukata mawasiliano. His movements and actions are subject to watchdogs!! Hivi jamani watoto wake wako wapi?
 
Muulizeni Ibrahim Jumbe aliyesoma chuo cha maji ubungo mwanae anayefanya kazi katika meli ziendazo Dar-Zanzibar atawapeni full story.
 
Mkuu hapo hakuna uongo. Kumbuka kuwa Kahawa inasababisha mapigo ya moyo kuwa juu, hii ni kweli na haipingiki. Halafu tena viagra ni kiboko kwa mapigo ya moyo, ndiyo maana unashauriwa kabisa uzingatie kipimo kwa kuzingatia umri, uzito, magonjwa hatarishi kama kisukari, blood preasure, etc. Sasa basi kwa umri wa mzee wetu yule marehemu halafu uchanganye kahawa na viagra kwa hakika ni umauti. Siamini kama mjumbe aliyesema hili atakuwa ametunga. Kumbuka kile kifo, hakikusemewa sana!!! Hukujiuliza kwa nini?

Kuhusu Mzee Jumbe hicho ndicho kifungo chake cha maisha ndani ya makazi yake. Alijengewa nyumba ile na serikali na kutengwa kabisa na wazanzibari ili kukata mawasiliano. His movements and actions are subject to watchdogs!! Hivi jamani watoto wake wako wapi?

hata kwangu hii ya viagra na kahawa imekuja kama habari mpya.........:)

mzee jumbe keshakuwa mzee sana hata kutoka nje mpaka iwe lazima tu. wanawe watu wazima wako zenji wana vyeo vyeo serikalini, na hapo mji mwema anakaa na watoto wake wengine na wajukuu.
 
Hivi, Karume alipoamua kupindua utawala wa Sultani alitoa fursa gani kwa Wazanzibari kujadilia na kutoa radhi yao?

Watu wanapotosha historia ya mapinduzi ya Zanzibar!! Aliyeongoza mapinduzi huko Zenj mwaka 1964 ni mganda aliyejulikana kwa jina la Field Marshall John Okello!! Wazanzibari hawataki kumtukuza huyu bwana kwani wanadhani atawapunguzia sifa wakina Natepe!!
 
Watu wanapotosha historia ya mapinduzi ya Zanzibar!! Aliyeongoza mapinduzi huko Zenj mwaka 1964 ni mganda aliyejulikana kwa jina la Field Marshall John Okello!! Wazanzibari hawataki kumtukuza huyu bwana kwani wanadhani atawapunguzia sifa wakina Natepe!!
Hilo nalo nenooo!
 
FOR THOSE WHO DONT KNOW.
Komandoo na Hamad ndio waliokuwa waaminifu wa Mwalimu Komandoo msimamizi wa Unguja na Hamad Pemba.
ABoud Jumbe alisalitiwa na Wazanzibari ndio matokeo yake alipolazimishwa kwa mtutu wa Bunduki kulazimishwa kujiuzulu na laipogoma Pilot wake wa Ndege alitekwa nyara na usalama wa Taifa na Kurudishwa ZNZ , Mzee Jumbe akawa hana la Kufanya baada ya kuzungukwa na Usalama wa Taifa na silaha kama kuna VITA, kwani alikua makali sana na Mwalimu alihofia Aboud Jumbe alivyokua mkali akifika ZNZ atawatangazia Wazanzibari Muungano basi.
Aboud Jumbe for 90 days alikatiwa Simu baada ya kuambiwa na Usalama wa Taifa kuambiwa hana Ruhusa kurudi ZNZ kwa usalama wake, na hapo ndio Hamad alpotumwa Pemba kucheki hal iya Hewa na Salmin kuangalia kisiwa cha Unguja na kumpa report nyerere kumuambia hali iko Shuari mapinduzi yaendelee , matoeko ya mapinduzi haya wazee wa ASP wali fight back na kumngoa Hamad na Kundi lake ndani ya CCM ndio maneno ya Nyerere kila siku aliwambia watanzania kuwa upinzani wa Kweli utatoka ndani ya CCM kwani baada ya Hamad na kundi lake kutoka walihakikisha wanaimaliza CCM ZNZ na walifanikiwa kwa hilo. chaguzi tatu zilizofanyika ZNZ ccm imenguka ila usalama wa Taifa ndio wanafanya kazi ya kuilinda CCM.
 
Ninaishi just nyumba ya tano kutoka kwa JUMBE huku mjimwema.
Mzee wa watu hajui kama yupo au la maana
haoni, hasikii vizuri, na kumbukumbu hana hata moja. pia anaumwa kihodari kweli kweli shughuli imesalia moja tu kumtoa nje aote jua na kumrudisha ndani kwa kumbeba. tena siku hizi ulinzi umepunguzwa kwa asilimia 80. yaani unaweza kukatisha kwake utokee beach.

Kuhusu familia, watoto wake wenye akili ni wale aliowapata akiwa bado rais zenji. alipofika huku alikuwa mzee wa shughuli-fimbo alioa wake vijana-moto ambapo alipata watoto shombeshombe ambao nadhani walianza kula unga wakiwa ktk matumbo ya mama zao. Mitoto yote ni vurugu tupu na bangi mtu.

Kuhusu political scenario yake imepotea kama jiwe katika kilindi.
 
Natamani nikisome kitabu chake cha 'Partnership' ingawa sijui kinapatikana wapi!!

Ukisoma michango ya watu hapo juu....utagundua vitu vifuatavyo,
1. je muungano wa Tanganyika na Zanzibar bado unahitajika na wananchi wa pande zote mbili?

2. Mfumo uliopo wa serikali mbili unakidhi matwakwa ya pande zote mbili?

3. Unafiki wa wanasiasa hasa wa Zanzibar?

Hivi mikataba na makubaliano ya awali ya muungano yako wapi?

Sitoshangaa kusikia kuwa pengine hata Mh. Rais JK hajawahi kuyaona makubaliano hayo......ila kwa sababu ameukuta muungano inabidi akomae nao tu! Nakumbuka Mh. Mkapa aliwahi kutamka kuwa kamwe hasingeruhusu muungano uvunjikie mikononi mwake!!
 
Kosa kuu la Jumbe lilikuwa kujaribu kuvunja muungano na kuunda serikali tatu. Alituhumiwa kwa makosa sita. Makosa hayo yalisomwa na Kawawa kama ajenda toka kamati kuu ya CCM kwenye mkutano wa NEC.

1. Kuna watu ndani ya serikali ya Zanzibar ambao wanavumisha uvumi kwamba zoezi la kubadili katiba ya muungano lilikuwa na maana ya kuimeza Zanzibar na wazanzibar wameanza kuamini katika uwongo huo.

2. Baraza la mapinduzi Zanzibar lilikuwa linapinga chama kushika hatamu kitu ambacho ni kinyume na katiba ya CCM

3. Kuna watu karibu na serikali ya Zanzibar walikuwa wanapinga waziwazi muungano na kudharau misingi ambayo ilitumika kuanzisha muungano huo. Wanadai Tanzania ina serikali tatu na wameandaa file la kupeleka case mahakamani. hapo ndio ile hesabu ya nyerere eti 1+1=3, wajinga sana hawa watu.

4. Vitendo vya wasaliti hawa vimeleta wasiwasi ndani na nje ya nchi yetu.

5. Ni wazi hali kama hiyo inahatarisha usalama wa taifa.

6. Kulikuwa na uvumi kwamba wakati wa sherehe za miaka 20 ya mapinduzi ya Zanzibar, watu wa usalama walitishiwa. Japo hali ilitulizwa lakini kuchafuka kwa hali ya kisiasa kumeendelea.


Waliopigilia misumari hasa alikuwa Hamad. Pamoja na Jumbe kupangua point moja baada ya nyingine lakini Mwalimu akapigilia misumari zaidi.

Jumbe aliwaambia wajumbe kwamba tuhuma dhidi yake ni kubwa mno na kama wajumbe wanaziamini au wanahisi kunaweza kuwa na ukweli basi wamsaidie kwa kumvua madaraka yote waliyompatia.

Alitia huruma mzee wa watu aliposema I say this with a clear conscience, without arrogance or humilation, or anger or joy.

Ilikuwa kama ile ya Asulubiwe Yesu. Wajumbe wa NEC wakaitikia asulubiwe. Baada ya Nyerere kumwomba ajiuzulu, akatangaza kwenye mkutano kwamba anajiuzulu. Kawawa na Sokoine wakamfuata Jumbe nje ya ukumbi kwamba aandike barua za kujiuzulu lakini yeye akaandika kujiuzulu vyeo vya muungano tu ambavyo ni makamu wa rais na makamu wa CCM na aksema vile vya Zanzibar ataenda kuandika barua baada ya kufika Zanzibar. Ikabidi Nyerere aitwe na akamwambia Jumbe asiende Zanzibar na ana uhuru wa kwenda popote Tanzania bara na aandike barua zote hapo hapo.

Jumbe akajitetea kwamba kule Zanzibar ana wake zake na anataka kwenda kuwaona, akaambiwa hakuna. Alivyofika airport akakuta ndege yake haipo tena na akachukuliwa na ndege ya muungano. Kufika Dar hakukuwa na hata viongozi wa kumpokea zaidi ya usalama wa taifa kibao. Akachukuliwa na kupelekwa kwake Mji Mwema ambako alikuta simu zake zote zimekatwa mpaka akashindwa kuwasiliana na wake zake Zanzibar.

Baada ya siku moja na nafikiri baada ya mabishano sana wakamruhusu kwenda Zanzibar kuwaona wake zake chini ya ulinzi mkali na kisha wakamrudisha bara siku iliyofuata ambako ndio anaishi muda wote.

Hamad akaogopa kwamba baraza la mapinduzi kule Zanzibar lingemchagua Seif Bakari kumbadili Jumbe. Ikabidi amshauri Nyerere kwamba mabadiliko yafanywe na NEC na Nyerere akakubali ingawaje kikatiba NEC ilikuwa haina uwezo wa kumchagua kaimu rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi. Lakini baada ya haya yaliyompata Jumbe nani angebisha? Ikabidi mzee Kombo aitwe toka alikokuwa na yeye ndiye aliwashauri wamteue Mwinyi.


Jumbe hawezi kumsahau Hamad kwa kumsaliti.

Siku hizi serikali imemrudishia mafau yake na kuna siku niliwahi kumwona airport Heathrow akiwa na toto dogo dogo huku yeye hata kuona haoni. Alikuwa anatoka kutibiwa UK.
 
Aboud Jumbe Mwinyi alikuwa Rais wa pili wa Zanzibar toka mwaka 1972 hadi mwaka 1982 alipotimuliwa na CCM baada ya kuchafuka kwa hali ya hewa.Nasikia siku hizi anaishi mji mwema kigamboni Dar es Salaam akisubiri siku zake ziishe hapa dunia.

Jumbe aliondolewa kuwa rais wa Zanzibar January 1984 kwenye kikao cha dharura cha NEC kule Dodoma. Hakutimuliwa mwaka 1982.
 
Hivi, Karume alipoamua kupindua utawala wa Sultani alitoa fursa gani kwa Wazanzibari kujadilia na kutoa radhi yao?

Historia ya kweli ya mapinduzi ya Zanzibar inaonyesha kuwa John Okelo ( mganda) na wanaharakati vijana wengi wao kutoka bara km akina mfaranyaki ndio walioshiriki mapinduzi hayo....baada ya kufanikiwa ilibidi wamtafute mzawa wa hapo ili wampe uongozi na kwa sababu hiyo ilibidi watumie matangazo ya radio kusaka Karume alipojificha ili aje atwae madaraka....ni mbinu za nyerere zilizo msaidia karume kumtosa Okello kwa kumdanganya kuwa anaitwa Dar ili kupongezwa na nyerere kwa ushujaa wake..lakini alipowasili uwanja wa ndege dar alikamatwa na kusafirishwa hadi Uganda.
 
okello,wakat wa utawala wa idi amin alisema "now we have two field marshalls here" akimaanisha yeye na idi amin ndio FM. Huo ndio ulikuwa mwisho wake kuonekana duniani,makachero wa idd amin walimtupa mto nile na crocodiles wakamalizia
 
Nilikuwa sijui kama nyerere alikuwa dikteta kiasi hiki. yaani alikuwa analotaka ndo linalokuwa. Hii ni aibu kwa mtawala ambaye kila kukicha anasifiwa. Alietaka awe rais ndo aliekuwa. Hakupenda kupingwa wala mtu kuwa na mawazo mbadala. Hii ni hatari kwani akiwa hata na maoni ambayo hayana tija kama ya muungano hamna wakumshauri. we do not need a leaders of such kind. KULIKUWA NA UBAYA GANI WA KUACHIA HOJA KAMA ILIKUWAPO KWA MFANO HII YA MUUNGANO KUJADILIWA NA KUWA NA RADHI YA JAMII ZOTE HUSIKA? AU KWENYE HUO MUUNGANO KUNA SIRI GANI? KWA NINI HAKUTAKA KUJADILIWA? MATOKEO YAKE NAONA WATU WANAMKEJELI TU MZEE JUMBE. SISHANGAI HUENDA HUYU MZEE ALIKUWA SAHIHI. This is a century shame!

Mkuu, waweza kuwa sahihi lakini nina mawazo tofauti kidogo,
Nadhani katika uongozi huwezi tenda kutokana na matakwa ya watu wote, ukizingatia mawazo na uwezo pambanua wa watu hutofautiana, fikiri kama Nyerere asingefany aaliyoyafanya na matokeo ya Mzee Jumbe, Je hali ingekuwaje?

Naamini hata katika uongozi, hakuna pure democracy bali akili ya kiongozi mzuri hupembuwa wapi demokrasi itumike and wapi NGuvu itumike.

Nawasilisha
 
kama muungwana alivyosema huko juu mkuu, usipende kusema ni uogo tu kwa sababu hujakipenda kilichoandikwa, we toa sababu kuonyesha ni the other way around vinginevyo unataka kuleta ubishani usio na tija! kwani kutumia viagra kwa mtu mzima kama yule ni ajabu? alikufa gen.sani abacha kwa viagra tena sio kwa mkewe kwa hooker wa kirusi itakua yeye bana! mda aliotangazwa kafa ni mida flan ya ndio kwanza watu wanaenda kulala na pia hadi anaenda kulala alikua mzima kabisaaaaa!

Gen Sani Abacha hakufa kwa viagra ndugu ila kwa Apple lililokuwa limechomwa poison injection na hakuwa hoocker wa kirusi ila ni four hookers from India
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom