Kulikoni Mohamed Trans?

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,260
licha ya ajali nyingi kutokea hapa nchini hatujawahi kuona mmiliki wa kampuni anafuatiliwa kama ilivyo sasa kwa hii ya mohamed trans au ndio yupo katika hatua za mwisho kufilisiwa, jana jeshi la polisi lime kamata gari zake mbili kwa kosa ambalo halipo au ambalo linahusu zaidi TBS ambao ndio wanajua viwango gani vinafaa na ukiangalia gari kama hizo zipo nyingi sana barabarani na hazikamatwi, hii ikoje wana JF
 
kwani haya mabasi mmiliki wake ni nani? na je anauhusiano wowote au mchango kwenye siasa?
 
Unakumbuka juzi kati madereva wa mabus ya mikoani waligoma sababu dereva mwenzao wa Mohamed Trans alihukumiwa miaka 30 kwa kusababisha ajali?,may be kuna connection na hilo
 
Sina hakika lakini nasikia ni mwarabu wa huko shinyanga. kuna bosi mmoja anaitwa sudi sina hakika kama ndiye mmiliki au laa!
 
ni fitina za viongozi wetu tu kwenye ajali ya mohamed trans juzi huko tanga alifariki pia ndg ya Jk so ndo maana unaona trend ya hawa jamaa kufatiliwa ilianzia hapo .
 
Huyu Jamaa ni mwarabu anaishi pale Maganzo Shinyanga jirani na Mgodi wa Mwadui. Asili yake ni Idukilo kijiji kimoja kiko jirani na Mwadui pia. Huyu jamaa hajihusishi na siasa ila inawezekana kuna watu wanaotaka ambao wako connected na mafisadi (phantom) wanaweza kuwa wanaitumia Serikali ya CCM kumkandamiza huyu jamaa kwa sababu ya ugomvi wao
 
... kwa kosa ambalo halipo au ambalo linahusu zaidi TBS ambao ndio wanajua viwango gani vinafaa

Kosa gani hilo ndugu? Itakuwa vigumu kwa baadhi yetu kuanza kulaumu serikali, au kulaani mmiliki bila kujua hilo "kosa ambalo halipo." Tutang'amuaje kama kweli yapo vitabuni au anaonewa kama makosa yenyewe nayo yamekuwa siri?

Hoja yako ya TBS nayo ngumu kidogo kuikubali. Polisi akikushika na matairi ya mipira ya utomvu ya China huwezi kuwaambia "TBS ndio wanajua viwango, mi sijui." Watakusweka ndani.
 
Jamaa ni msukuma-mwarabu wa Idukilo na yeye ndiye aliyebaki baaday ya ndugu zake wawili kufariki hivi majuzi.Ni kijana mdogo hana amabo ya siasa.
 
Najua sana wanamuonea wivu wanamlazimisha sana aingie kwenye ufisadi wao awachangie pesa....yeye hataki mambo ya siasa wanamuandama kijana wa watu...na biashara zake......mbona magari yyote ya Tanga yana chesis za malori miaka na miaka wanamuandama yeye tu?????hata magari ya Mwanza kibao tuu.....wanamuonea Kombe anataka sifa hana lolote kazi ya TBS anaifanya yeye.......hana kazi ya kufanya????au ndio shule na ufisadi unamkimbiza...??
 
Mkuu,

To me kosa ni kosa, so it does not justfy kosa eti tu kwa sababu magari mengine au mabasi mengine yana makosa or weakness kama hizo za Mohamed Trans na hayajakamatwa! Ni jukumu langu na wewe kuwajulisha polisi kuwa kuna magari fulani na fulani yenye same problems na yakamatwe pia...sio kuquestion why kakamatwa huyu na sio yule, how can you know kama na hao wengine wameshaonekana machoni mwa polisi?
 
licha ya ajali nyingi kutokea hapa nchini hatujawahi kuona mmiliki wa kampuni anafuatiliwa kama ilivyo sasa kwa hii ya mohamed trans au ndio yupo katika hatua za mwisho kufilisiwa, jana jeshi la polisi lime kamata gari zake mbili kwa kosa ambalo halipo au ambalo linahusu zaidi TBS ambao ndio wanajua viwango gani vinafaa na ukiangalia gari kama hizo zipo nyingi sana barabarani na hazikamatwi, hii ikoje wana JF

Taja makosa hayo usitupe kitu ambacho ni black & white
 
Huyu Jamaa ni mwarabu anaishi pale Maganzo Shinyanga jirani na Mgodi wa Mwadui. Asili yake ni Idukilo kijiji kimoja kiko jirani na Mwadui pia. Huyu jamaa hajihusishi na siasa ila inawezekana kuna watu wanaotaka ambao wako connected na mafisadi (phantom) wanaweza kuwa wanaitumia Serikali ya CCM kumkandamiza huyu jamaa kwa sababu ya ugomvi wao

Jamani hamjui kwamba huyu bwana ameingilia route za watu?? Njia ya Nairobi-DSM na DSM - Mombasa ni njia za mabasi yanayo milikiwa na vigogo wa CCM.

Yeye alitakiwa akae njia ya MWZ-Nairobi na MWZ-DSM sasa kwa yeye kuanza route ya kaskazini kuja na kutoka Dar, itamgharimu sana.
 
licha ya ajali nyingi kutokea hapa nchini hatujawahi kuona mmiliki wa kampuni anafuatiliwa kama ilivyo sasa kwa hii ya mohamed trans au ndio yupo katika hatua za mwisho kufilisiwa, jana jeshi la polisi lime kamata gari zake mbili kwa kosa ambalo halipo au ambalo linahusu zaidi TBS ambao ndio wanajua viwango gani vinafaa na ukiangalia gari kama hizo zipo nyingi sana barabarani na hazikamatwi, hii ikoje wana JF

Hii ni dhulma kubwa
 
Najua sana wanamuonea wivu wanamlazimisha sana aingie kwenye ufisadi wao awachangie pesa....yeye hataki mambo ya siasa wanamuandama kijana wa watu...na biashara zake......mbona magari yyote ya Tanga yana chesis za malori miaka na miaka wanamuandama yeye tu?????hata magari ya Mwanza kibao tuu.....wanamuonea Kombe anataka sifa hana lolote kazi ya TBS anaifanya yeye.......hana kazi ya kufanya????au ndio shule na ufisadi unamkimbiza...??

Sasa jamani Kombe na elimu yake ya pale VETA atafanya nini? Nashukuru siku hizi anamuogopa Dk. Mwakyembe baada ya kutaka kumuongopea naye akaja juu, kwi kwi kwi.
 
Back
Top Bottom