kulikoni Dar live!parking at ur own risk!!!kweli?

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
8,305
13,265
Hakika kwa sasa ktk jiji la dsm kiwanja hiki cha starehe ndicho kimekuwa gumzo,kila kona,na nikutokana na buruduni live zinazokuwepo, ila kuna tatizo juu ya suala la parking, jana nilikuwa pale na jamaa yangu alikuwa na gari lake,tulipofika tukaonyeshwa sehemu ya parking na mlinzi,na sehemu yenyewe ni ile sehemu ya kati kati ya hifadhi ya barabara ya kilwa! Ndipo magari yana park!

Mlinzi akatuhakikishia kuwa ulinzi ni wa uhakika, bac tukaingia ndani,kwenye mida ya saa tano ucku tunaondoka tunakuta side mirror zote zimenyofolewa!

Tukamuita mlinzi na kumuuliza kulikoni,anajibu yeye haucki na ulinzi wa magari!,tukaenda kwa muhusika mwingine naye anajibu kuwa wao hawahusiki na ulinzi wa magari!ilikuwa zogo kwani jamaa ni mtata,ndio akaja mzee fulani naye ni muhusika pale,kidogo ana busara,akamuomba leo aende waangalie watamsaidiaje.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom