Huyu mwandishi anazungumzia kesi ya Zombe na wenzake kufanyika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu. Wakati kesi hii iko Mahakama Kuu na ilikuwa ikiendeshwa na Jaji Masati, manake kesi za mauaji hufanyika Mahakama Kuu, bali kwa kutajwa huanzia mahakama za chini. Hivi na wahariri wa habari nao hawana muda wa kupitia habari kabla ya kuchapishwa?. Soma habari:-
Zombe na wenzake kuanza kujitetea leo
Na James Magai
KESI ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva teksi wa Manzese, Dar es Salaam inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Dar es Salama, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe na askari wenzake 12, inaendelea leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kesi hiyo leo inaingia katika hatua ya pili, ambayo sasa itakuwa ni zamu ya watuhumiwa hao kuanza kujitetea dhidi ya tuhuma zinazowakabili.
Hatua hii ya pili ni muhimu na ngumu kwa washtakiwa kwa kuwa, watakuwa na kibarua cha kupangua hoja mbalimbali zilizotolewa dhidi yao na mashahidi wakati wakitoa ushahidi wao.
Lakini pia ni ndiyo hatua itakayotoa mwelekeo halisi wa kesi hiyo, iwapo wote ama baadhi yao watatiwa hatiani.
Pengine huu utakuwa uwanja mpana kwa Zombe, kuonyesha umahiri wake katika sheria, maana wakati wa ushahidi mara kwa mara alikuwa akiwaandikia mawakili wake ujumbe kwenye karatasi ama akiwaelekeza au kuwakumbushia maswali ya kuwauliza mashahidi au vifungu vya sheria
Kubwa zaidi katika hatua hii ni uwezekano wa washtakiwa kusalitiana au kuwakana wenzao. Hatua hii ni hatua ambayo kila mmoja anatakiwa kujiokoa mwenyewe.
Kutokana na hali hiyo, inaaminika kuwa huenda baadhi ya washtakiwa kusalitiana kunatokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, kutokana na baadhi ya mashahidi kuieleza mahakama kwamba, baadhi ya watuhumiwa walieleza ukweli jinsi mauaji hayo yalivyofanyika.
Miongoni mwa mashahidi hao ni pamoja na shahidi wa 36, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Sigine Mkumbi aliyekuwa kiongozi wa timu ya Jeshi la Polisi ya upelelezi wa mauaji hayo na shahidi wa 30, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emson Mmari, aliyekuwa mjumbe katika timu hiyo.
Mashahidi hao kwa nyakati tofauti waliieleza mahakama kuwa wakati wakifanya upelelezi juu ya tukio hilo, mshitakiwa wa 11, Rashid Lema na wa 12, Rajabu Bakari waliwaeleza wafanyabiashara hao kuwa waliawa katika Msitu wa Pande, ulioko Mbezi Luis nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mmari ambaye wakati wa mauaji hayo alikuwa akifanya kazi makao Makuu ya Jeshi la Polisi, aliieleza mahakama kuwa washtakiwa hao waliwaeleza kuwa wafanyabiashara hao walikuwa wakishushwa mmoja mmoja kwenye gari na kulazwa chini kifudifudi na kupigwa risasi.
Alisema wakati wa upelelezi alimhoji mshtakiwa wa 11, Koplo, Rashid Lema ambaye aliwaeleza ukweli wa jinsi na mahali maujai hayo yalikofanyika na kwamba, Machi 7 aliwapeleka eneo hilo ambapo walikuta damu ilikauka na kugandamana na udongo ambao waliupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kuthibitishwa kuwa ni ya binadamu.
Pia Mmari alisema Koplo Lema aliwaeleza aliyefanya mauaji hayo kuwa ni Koplo Saad Alawi ambaye hadi sasa hajakamatwa na kwamba, baadaye walipotakiwa kwenda kujieleza kwenye Tume ya Rais, Zombe aliwashinikiza waseme uongo na kuwaandikia maelezo kwenye vikaratasi jinsi ya kueleza.
Mbali na ushahidi huo wa Mmari na mashahidi wengine waliotoa uligusa watu wengi kutokana na kusisimua kiasi cha ndugu wa marehemu kutoa machozi, lakini shahidi aliyeacha gumzo ni shahidi namba 25, Shaban Said Manyanya.
Shahidi huyo aliwashangaza wasikilizaji baada ya kudai kuwa yeye ndiye aliyestahili kuuawa kwa sababu ndiye aliyepora pesa za Bidco ambazo watuhumiwa walidai ziliporwa na wafanyabiashara waliouawa.
Manyanya aliiambia mahakama kuwa aliumia sana aliposikia Zombe akitangaza kwenye luninga kwamba, wamewaua majambazi wanne Sinza kutokana na kupora fedha za Bidco kwa sababu hawakuwa na hatia hivyo walionewa kwani yeye na wenzake ndio waliopora pesa hizo.
Alidai kutokana na maumivu aliyoyapata ya kuuwa watu wasio na hatia aliamua kwenda kutoa maelezo yake katika Tume ya Rais ya kuchunguza mauaji hayo iliyoongozwa na Jaji Mussa Kipenka.
Hatua ya kwanza ya kesi hiyo ilianza kusikiliwa rasmi Mei 26, 2008 kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ilianza Mei 26 hadi Juni 12 na jumla ya mashahidi 29 walitoa ushahidi wao mahakamani hapo.
Awamu ya pili ilianza Septemba 2 hadi Septemba 6 mwaha huo huo na mashahidi watatu tu ndio walitoa ushahidi na kufanya idadi ya mashahidi kufikia 32.
Awamu ya tatu na ya mwisho katika kesi hiyo ilianza Septemba 22 hadi Septemba 26, upande wa mashtaka ulifunga ushahidi na jumla ya mashahidi 37, walikuwa wametoa ushahidi wao.
Katika kesi hiyo Zombe na wenzake wanatuhumiwa kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Wilaya ya Mahenge mkoani Morogoro ambao ni Sabinus Sabinus Chigumbi maarufu kama Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe Juma Ndugu, dereva teksi aliyelkuwa akifanya kazi katika kituo cha Manzese jijini Dar es Salaam.
Mbali na Zombe washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni SP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, F.5912 PC Noel Leonard, WP 4593 PC Jane Andrew, D6440, CP Moris Nyangelela, CPL Emmanuel Mabula, E6712 CPL Felix Cedrick, D8289 PC Michael Sonza, D 2300CPL Ebeneth Saro, D.9312D/C Rashid Lema, D4656 C/CPL Rajab Bakari na D.1367 D/CPL Festus Gwabisabi.
Source: Mwananchi Read News