Kuku wa kisasa wanakuzwa kwa ARVs

Mar 9, 2010
9
0
Kuna rafiki yangu amenitumia email hii ambayo imenishtua kiasi fulani. Wanajamii forum hebu tuichunguze na kuijadili kuona kama ina ukweli wowote.

"Habari ndio hiyo, uamuzi ni wako

Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi wa kitabibu, baadhi ya kuku wa kufugwa
wanaoingia sokoni wamekuzwa kwa kutumia ‘utundu’ wenye hatari wa baadhi ya
wafugaji wasio waaminifu kwa kulisha mifugo hiyo dawa za ARV ambazo
huwafanya kuku hao kuonekana wakubwa na wanene kwa muda mfupi.

Uchunguzi huo unakwenda mbele zaidi na kubainisha kwamba, tabia za dawa
hizo ambazo ni kujenga mwili na kuimarisha kinga ya magonjwa kwa
mwathirika wa Virusi vya Ukimwi, ndiyo inayompata mlaji wa kuku hao.

Inadaiwa kuwa, kuku hao wanapokula chakula kilichochanganywa na dawa hizo,
huweza kutumia siku kumi na mbili hadi kumi na nne kutoka kuwa vifaranga
hadi utayari wa kuingizwa kwenye soko la walaji.

Ili kukamilisha uchunguzi huo, Amani lilituma makachero wake maeneo ya
Kibamba, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo ndipo kwenye viwanda vya
kuzalisha kuku wa ‘sampuli’ hiyo.

Kwa mujibu wa kijana mmoja ‘profesheno’ wa kutunza kuku katika moja ya
nyumba maarufu kwa uzalishaji maeneo hayo, ambaye hakutaka jina lake
lichorwe kwenye ‘pepa’ hii, alikiri kuwepo kwa ishu hiyo, lakini
alibainisha kuwa hajui bosi wake anapochukulia vidonge hivyo vya ARV’S.

MADHARA:
Kwa mujibu wa Daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbi ambaye aliomba
hifadhi ya jina lake, mtu anayependa kula kuku waliokuzwa kwa kutumia ARV
na yeye huanza kunenepa kupita kawaida, lakini uzito unaweza kuwa tofauti
na unene ‘boya’.

Mtabibu huyo aliongeza kuwa, watoto wengi wanaozaliwa siku hizo ambao
wazazi wao wamekuwa watumiaji wazuri wa kuku, hukua haraka kiasi kwamba,
mtoto wa miaka 18 huonekana kama ana miaka 27.

Aidha, alidai kuwa, wengi ambao kuku hao wamekuwa chakula chao kikuu,
hufika mahali wanakuwa ‘legelege’ katika utendaji wa kazi wa kila siku
tofauti na zamani huku sehemu kubwa ya chakula hicho ikiangamiza ‘pati’ ya
subira na uvumilivu na mlaji kuwa na hasira.

Dalili nyingine ni mtu kuhisi muda wake wa kuchoka unakuwa mfupi
akilinganisha na zamani na wakati mwingine hali ya kuhisi kusinzia
humtawala hata kama anafanya kazi"

Department of Agricultural Engineering,
P.O. Box 3003,
Morogoro
TANZANIA
 
Mimi sikuiami the first day nilipoiona.

Inadaiwa kuwa, kuku hao wanapokula chakula kilichochanganywa na dawa hizo,
huweza kutumia siku kumi na mbili hadi kumi na nne kutoka kuwa vifaranga
hadi utayari wa kuingizwa kwenye soko la walaji.

Hii kali siku 12 unakula kuku?

MADHARA:
Kwa mujibu wa Daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbi ambaye aliomba
hifadhi ya jina lake, mtu anayependa kula kuku waliokuzwa kwa kutumia ARV
na yeye huanza kunenepa kupita kawaida, lakini uzito unaweza kuwa tofauti
na unene ‘boya'.

Mtabibu huyo aliongeza kuwa, watoto wengi wanaozaliwa siku hizo ambao
wazazi wao wamekuwa watumiaji wazuri wa kuku, hukua haraka kiasi kwamba,
mtoto wa miaka 18 huonekana kama ana miaka 27.
 
dada Judy naona umejilipua mzima mzima na jina lako! teh teh teh eh!

Department of Agricultural Engineering,
P.O. Box 3003,
Morogoro
TANZANIA

Join Date: Tue Mar 2010
Posts: 5
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
 
Back
Top Bottom