Kuku anaingia mwenyewe kwenye tenga...

Kakukuruka vyema,

Kaachiwa na kuonyeshwa tundu la kutokea, badala yake kajidanganya kwa kutamani mbegu chache zilizobakia kwenye tenga. Anarudi, anarushiwa mchele wa kutosha nje ya tenga hataki kutoka kisa mahindi kiduchu. Kwa kiburi kabisa anajaribu kuwadonoa hata wale ambao wangemsaidia, anawatishia... anang'ang'ania kukaa kwenye tenga!

Kwakuwa ni 'kuku wa kizungu' tumwache tusifunike tenga na 'kumshughulikia'?

Jamani Kuku anayezungumziwa hapa ni wananchi wa Igunga ambao kwa hiari yao walijikuta katika utawala(Tenga) wa CCM kwa miaka nenda rudi.Wamefunguliwa mlango wa tenga na kelele za ufisadi za Chadema zilizomtoa fisadi Rostam(Rostam ndiye mlango wa tenga) wamewekwa huru toka mikono ya CCM, cha ajabu wanaigunga hawataki kutoka kwa sababu tu ya woga wao ilhali nje(chadema) kuna manufaa endelevu ya kitaifa, huku wana igunga wakithubutu hata kuwa kuwadhihaki waliowafungulia mlango wa kutoka(Chadema)
Nawasilisha
 
Talking about JF Home of Great Thinkers.......
 
well we all know kwa nini sio kila mwana JF ni Great thinker...because tuko bize kufkiri avitu kama hivi:
tumblr_lkksfk9i6S1qh1fxmo1_500.jpg

Welcome back Brazameni
 
Kwa kurudi kwenye tenga kwa punje kidogo za mahindi kajikaanga mwenyewe, haitajiki hata mtoto wa jirani kusaidia kumkimbiza afungwe kamba mguuni!
 
kama shuleni kwetu Iyunga kuna jamaa alikuwa akiitwa Abuu Sabun. Jamaa alikuwa ni bangi, pombe na ukorofi for life. Alisoma Tambaza, lakini akahamishiwa shuleni kwetu ili kurejesha heshima na hadhi ya Tambaza. akahamia shuleni kwetu Iyunga...enzi hizo maarufu sana kwa kutesa form one kama magereza vile.

hahaha.......

ikawa kuna utaratibu wa wanafunzi kulazimishwa kutandika mashuka ya pinki vitandani. basi ikatokea siku tulikuwa tunafanya mitihani bana. Abuu Sabun yeye nadhani hata hakuwa na ratiba. alichokuwa anajua ni kwamba majira ya saa mbili watu wa Bweni la Shaaban Robert majira ya saa 2 watakuwa wanafanya mitihani.

kama kawa saa mbili ilivyokuwa inasogea, kila mtu akawa halahala anatandika shuka kuancha mandhari safi ya kitanda chake na chumba kwa ujumla.

tukaenda kupiga pepa....

Tuliporudi tu tukakuta Abuu Sabun kafanya mambo zake....kakomba mashuka yote lisisalie hata shuka moja.

Da kusoma boarding raha sana.

labda hii inaendana kidogo na hoja ya mtoa mada.

Kweli kitendawili kikiwa kigugumu, watu wanasimulia stori zao tu
 
Aaah Ndugu NasDaz, wa kwanza kusema kuwa huyu kuku ni bro. BEN MKAPA ilikuwa ni mimi,angalia michango ya mwanzo mwanzo kabisa kwenye thread hii!tuendelee kutegua fumbo la Invisible....

Ahaaa; na wewe nawe!!! kwanza swali la Invissible ilikuwa "Briefly and explain logically" na sio "mention or list!" lol, lakini sio mbaya Braza Invisible akinipa 10/10; wewe nitakugea 1/10!!!
 
Kakukuruka vyema,

Kaachiwa na kuonyeshwa tundu la kutokea, badala yake kajidanganya kwa kutamani mbegu chache zilizobakia kwenye tenga. Anarudi, anarushiwa mchele wa kutosha nje ya tenga hataki kutoka kisa mahindi kiduchu. Kwa kiburi kabisa anajaribu kuwadonoa hata wale ambao wangemsaidia, anawatishia... anang'ang'ania kukaa kwenye tenga!

Kwakuwa ni 'kuku wa kizungu' tumwache tusifunike tenga na 'kumshughulikia'?
Kumbe invisible mashairi nayo unayaweza!
 
When chicken is not poultry, tenga litaachia kamba zake halafu mabo yote hadharani, pwaaa!!!!
 
Good puzzle..
great thinkers wamepeleka tafsiri zaidi ya mbili zinazofit kwenye hii chemsha bongo.. lakini this time chemsha bongo inaakisi jamii halisi katika tukio la kweli na si la kufikirika kama zilivyo chemsha bongo za magazetini tulizo zowea.
 
tunamwogopa huyu kuku........................hata tunashindwa kumsema waziwazi.........a big shot..........but he is only too humane.....................
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom