Kukatika kwa umeme

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,466
9,028
Habari wana jf

Nimekuwepo Dar es Salaam na na-experience mgao wa umeme wa mara kwa mara. Hii imekuwa mitaani (residential places) lakini na mjini pia (katikati ya mji na Kariakoo) kuna ukatikaji usio rasmi. Hivi ninavyoandika umeme huku katikati ya mji hakuna na ilikuwa hivi kwa zaidi ya majuma mawili yaliyopita.

Sijamuona dada yetu Badra Masoud au Waziri Ngereja wakiongelea tatizo hili kwa siku hizi! Kama sikosei waziri na Tanesco waliwahi hapo nyuma kidogo kusema mgao ulikuwa umeisha (kama sio kupungua).

Kulikoni, mwenye taarifa na kinachoendelea naomba atujuze ili tuweze kupanga ratiba hizi za 'mateso'.

Inasikitisha!!!.
 
wakati mwingine ni matatizo ya kiufundi, nayo yako mengi kuliko mgawo unaotokana na kwisha kwa maji
 
Huku arusha_maeneo ya sakina hakuna umeme toka juzi usiku,...yaani ni tanesco ni full ujinga
 
Back
Top Bottom