Kukatika kwa umeme uwanja wa taifa; wizara yaomba radhi

Viongozi wetu kwa sababu za kipumbavu na uzembe wanaongoza duaniani.

Sasa kama mnajua generator halina uwezo wa kuwasha umeme hapo uwanjani kwanini mlinunua? Au mmezuga kuweka hapo la bei rahisi hili hela iliotolewa kwa ajili ya generator lenye uwezo mtie ndani?

Tamaa inatumaliza wa afrika.
 
mpuuzi tu huyu manager, ngoja wakachunguze kama wanaochunguza wako makini watagundua makubwa zaidi ya hili.

Issue kubwa hapa lazima itakuwa ni mafuta tu. Nadhani ndo deal lao kubwa. Wakifatilia watakuta magenerator huwa yanakunywa wese kila siku tena full tank. Hapo ndo wizara na huyu manager sasa hivi mmkojo unawawasha.
 
Jana Waziri Nchimbi aliunda tume ya watu wanne ili kutafuta kile kilichoelezwa "sababu ya kukatika umeme uwanja wa taifa juzi". Kwa mtazamo wangu mi naona hii ni kuwahadaa watanzania. Hapa hakuna jingine bali ni uzembe wa hali ya juu wa wahusika wa uwanja wa taifa (Hapa siilaumu Tanesco maana hao washashindikana).

Umeme ulikatika sawa, standby generator zipo na zilipaswa kuwaka punde tu baada ya umeme kukatika, hali haikuwa hivyo. Tuanze kuwasaka wachawi wetu kuanzia hapo. Yaani tuanze na meneja wa uwanja wa taifa hadi kufikia kwa yule anayehusika na jenereta na ufundi umeme hapo uwanjani. Tujenge utamaduni wa kuwajibika na kuwajibishana na sio kuunda matume yanayotafuna mamilioni ya POSHO mwisho wa siku blah blah.
 
Asema yeye alikuwepo, substation ya kurasini, umeme ulipokatika walitegemea genereta ya U/taifa itawashwa lakin haikuwashwa lakin ameahd kulifanyia kazi suala hlo.
 
Bi Jenister Mhagama nae kazima swali la zitto la serikari kutowambia ukwel khs swala la mgao wa umeme na kwanin waziri na naibu wake wasijiuzuru?
 
natarajia wahusika wawajibishwe the same way walivyomuajibisha Kaijage wakati cd ya wimbo wa Taifa ilivyokataa kupiga
 
Wengi tumeshuhudia au kusikia kuwa umeme ulikatika ndani ya uwanja wakati zoezi la zawadi likiendelea baada ya mechi ya fainali ya Kombe la Kagame.

Magazeti ya leo yametoa taarifa za wadau kumbwa radhi kwa tukio lile. Serikali, Tanesco na TFF wameomba radhi.

Swali langu:

Hivi ni kweli uwanja ule uliojengwa hivi karibuni kwa fedha nyingi hauna "standby generator?"

Je kama zipo mbona hazikuwashwa?

Kama hazipo walitegemea nini wakati mara kadhaa tumeona mpira ukichezwa usiku.

Hivi hizi mechi za usiku huwa zinachezwa kwa kutegemea umeme wa Tanesco Pekee?

Kwa Tanzania leo Tanesco is a GIANT on Death bed. Kuwa na facility kama ile ambayo inachukuwa watu wengi kama vile tena nyakati za usiku kwa kutegemea Tanesco ni kucheza na usalama wa watu na mali zao.

Hebu menejimenti ya uwanja itupe ufafanuzi.
 
Majibu mepesi kwa swali zito..hawa mawaziri(Hasa Malima) wanajiona kama wako kwenye mradi wa familia kwa tabia na mienendo yao. Hivi hiki kichwa wenzangu kinaweza kutatua matatizo tulionayo? Du ngoja nikanunue mshumaa mkubwa kama mwenge maana hapa hakuna umeme labda mpaka Hilary Clinton arudi na kutukuta bado tuko gizani.
 
Mbona sasa hajajibu chochote? utumbo mtupu tunatiwa aibu na wapu.. wachache
 
@Mkeshaji, ni vizuri tukapata taarifa za uhakika nn kilichotokea maana yawezekana jenereta likawepo na likawaka na CHANGEOVER ikashindwa kurespond, au breaker ikaTRIPPLE etc. unajua kwny mambo ya kiufundi huwezi kukurupuka au kutumia siasa. If we can get technical report from technicians now w'll be in good position to comment
 
Tanzania acheni siasa za kuleana. Mpaka sasa hakuna aliyewajibika? nashangaaaaa sana?

Haya yetu macho
 
Hii nchi bwana....watu wamekalia upuuzi tu na ukichukulia vyeo vyenyewe wanapeana kishikaji na kindugu basi ndio hakuna wa kuwajibika..kila linalofanyika poa tu
 
Asema yeye alikuwepo, substation ya kurasini, umeme ulipokatika walitegemea genereta ya U/taifa itawashwa lakin haikuwashwa lakin ameahd kulifanyia kazi suala hlo.

Eti wameunda TUME ya watu 4 kuchunguza utakuta wametumia milioni 100 ambazo zingeweza kununua jenereta kubwa la kusambaza umeme uwanjani pale
 
mpuuzi tu huyu manager, ngoja wakachunguze kama wanaochunguza wako makini watagundua makubwa zaidi ya hili.

Issue kubwa hapa lazima itakuwa ni mafuta tu. Nadhani ndo deal lao kubwa. Wakifatilia watakuta magenerator huwa yanakunywa wese kila siku tena full tank. Hapo ndo wizara na huyu manager sasa hivi mmkojo unawawasha.
mtindo ndio huohuo! hata kwenye ma-STK!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom