Kukatia maji JWTZ tuone fahari au wazimu?

Jeshi ambalo linawapiga wanaolipa kodi kwa kuwepo kwao hatulitaki. Jeshi lisilokuwa na nidhamu hatulitaki.

Hii ni tabia ambayo imejitokeza kwa muda mrefu na inaendelea. Yuko wapi waziri atueleze sababu za wanajeshi kuchukua hatua hii mikononi mwao. JWTZ sio Polisi? Kulikoni?
 
Rev Kishoka naona kwenye hii issue umechemsha ile mbaya,nadhani unataka DAWASCO ife na mji mzima ukose maji labda utafikiria tena unachotetea.

Koba,

Yanayochemka ni maji, mimi si kibubujika!

Mimi nimesema busara itumike kwa suala hili la jeshi na bili ya maji au hata kama ni ya umeme. Sijahahi kusema Jeshi lisilipe deni. Mimi nilikuwa wa kwanza kuuliza kwa nini Dawasco hawakwenda kwa Waziri wao na kumuambia kuwa Jeshi linakataa kulipia maji na ndipo Mwandosya aende kuongea na Hussein Mwinyi kutatua tatizo!

Rudia kusoma maoni yangu!
 
Koba,

Yanayochemka ni maji, mimi si kibubujika!

Mimi nimesema busara itumike kwa suala hili la jeshi na bili ya maji au hata kama ni ya umeme. Sijahahi kusema Jeshi lisilipe deni. Mimi nilikuwa wa kwanza kuuliza kwa nini Dawasco hawakwenda kwa Waziri wao na kumuambia kuwa Jeshi linakataa kulipia maji na ndipo Mwandosya aende kuongea na Hussein Mwinyi kutatua tatizo!

Rudia kusoma maoni yangu!

bogus!!! ama kweli wewe ni kishoka.........for the record, jwtz in dawasco eyez are just costumers like anybody and everybody in the city. what you advocate here ni uswahili and its NOT, I will repeat, its NOT how business and/or companies are supposed to be running.
ati "wangemwona waziri kisha waziri huyo aende kwa waziri mwenzake ili wajadiliane," siandiki mengi....lakini ifikirie hiyo statement ktk quotes, kisha jiulize kwanini koba kakuita wewe ni "boiler."!!!
 
bogus!!! ama kweli wewe ni kishoka.........for the record, jwtz in dawasco eyez are just costumers like anybody and everybody in the city. what you advocate here ni uswahili and its NOT, I will repeat, its NOT how business and/or companies are supposed to be running.
ati "wangemwona waziri kisha waziri huyo aende kwa waziri mwenzake ili wajadiliane," siandiki mengi....lakini ifikirie hiyo statement ktk quotes, kisha jiulize kwanini koba kakuita wewe ni "boiler."!!!

YNiM, sorry to burst your bubble, hivyo ndivyo walivyofanywa, na bili haijalipwa bado na maji yamerudishwa. Sometimes biashara inaenda kwa mapatano.. you don't treat your best customers like crap!
 
Mkuu, sina ubavu wa kumsemea Mzee Mwanakijiji. Tatizo la kuingiza uhasama wa binafsi kwenye mada, mtatuboa wengine. Yeye kujiona Genius/Nyerere wa JF kunahusiana nini na mada hii?

With all due respect, nyinyi ndio hamna mtazamo wa kibiashara. Haya mambo ya kutishana, kukatiana huduma yote ni mazao ya monopolies zilizotokana na siasa yetu. Umesikia wapi ambako mteja mkubwa anatendewa hivi? Wameshindwa hata kwenda kuonana nao na kulitatua tatizo? Kwa wenzetu mabepari, mteja ni mfalme. Mteja mkubwa ndiyo basi. Kama nilivyosema, kibishara, kukata huduma ni hatua ya mwisho. Sasa hawa wafanyabiashara walifanya jitihada gani za kuwasiliana na mteja zaidi ya barua? Mteja anayetumia maji ya karibu bilioni moja ni wa kumlea na si kumdhalilisha. Ndio biashara na si siasa. Biashara unayozungumzia ni ya daladala.

halafu maneno hayo ndio ya mpenda amani na wenzake kwenye JF?? haya kaka, mie nazungumzia biashara ya daladala.........Tanzania yenu!!!!! endelea na kibarua chako cha msemaji wa "mfalme" MKJJ.

najitoa ktk mjadala huu...........obligado!!
 
halafu maneno hayo ndio ya mpenda amani na wenzake kwenye JF?? haya kaka, mie nazungumzia biashara ya daladala.........Tanzania yenu!!!!! endelea na kibarua chako cha msemaji wa "mfalme" MKJJ.

najitoa ktk mjadala huu...........obligado!!

Samahani kama nimekuudhi! Haikuwa nia yangu. Nimetumia mfano wa daladala kuonyesha utofauti wa 'scale'.
 
halafu maneno hayo ndio ya mpenda amani na wenzake kwenye JF?? haya kaka, mie nazungumzia biashara ya daladala.........Tanzania yenu!!!!! endelea na kibarua chako cha msemaji wa "mfalme" MKJJ.

najitoa ktk mjadala huu...........obligado!!

YNiS, don't put yourself down, simamia hoja zako, hapa haogopwi mtu au kupendelewa, nadhani nimejaribu kutoa hili somo mara nyingi.. go ahead mpinge unayejisikia kumpinga usinyanyue mikono kusalimu amri namna hiyo; vinginevyo mafisadi watashinda!! Kama amekushinda kwa hoja kubali ndio uungwana and move on.. !!
 
ninyi mna-point na sisi pia tuna point.......nadhani wote tupo sahihi!! cha msingi hapa ni kwamba wahusika "hopefully" wataona mawazo yetu na kuyafanyia kazi. chochote kibaya ktk sakata hili inshallah, hakitajirudia tena!!!

Fundi,
mie na mkjj tumeshawahi kuwa upande mmoja wa debate mara kadha(mfano issue ya miss TZ mhindi). tumeshapingana sana(mfano mjadala huu, wa nyerere na kambona n.k)....bottomline bado tunaendelea kuheshimiana!!!!. lau kama ukihisi memberz wanakorogana "ndonya" mkuu wangu, usichukue side, bali jaribu kuwa fair mediator, otherwise your accountability will have a BIG question mark!!!!

its all good, no sweats!!.
 
Fundi,
mie na mkjj tumeshawahi kuwa upande mmoja wa debate mara kadha(mfano issue ya miss TZ mhindi). tumeshapingana sana(mfano mjadala huu, wa nyerere na kambona n.k)....bottomline bado tunaendelea kuheshimiana!!!!. lau kama ukihisi memberz wanakorogana "ndonya" mkuu wangu, usichukue side, bali jaribu kuwa fair mediator, otherwise your accountability will have a BIG question mark!!!!

its all good, no sweats!!.

Kumbe ndiyo zenu wakuu! Kama ulivyosema, it is all good. Respect!
 
Unajua when i heard this kasheshe kuna kitu nilikumbuka...

Miaka hiyoooo wakati nasoma Shule Ya jeshi, unajua bwana this Guy Wanawa Jeshi sio kwamba ni Ubabe au wazimu hayo ni matokeo ya malezi na principal zilizopo huko kwao.. Unajua let see the fact here .. sasa wewe unaenda kukatia maji chombo kinachokulinda wewe na mali zako na hata kazi yako, Una akili kweli wewe ?

Imefika wakati Serikali ibebe mzigo wake Mbuzi wa bwana Herri na shamba la bwana Herri wacha wale.

Serikali Msikimbie Majukumu Yenu ni Hivi Lipieni hawa wajamaa From Umeme Maji na Usafiri Pia, kwani mkiwapatia huduma hizo kwa ufasaha kabisa basi hata Maadili yao yatakua mema kwa jamii kwani itawaheshimu kwa kujua wao ndio wanawalipia kupitia kodi zao.

Hao Dawasco Tanesco waende wakadai kwa baba yao Gorvment, wameweza kulipa madeni hea na mikataba ya kicheating cheating leo mshindwe kulipa huduma za watoto wenu.

Msituzungushe zungushe, Nijukumu la serikari kulipia kama hawalipi then ni hujuma tu, but kama ni Hoja basi najibu wazimu ule ule hamna kukata maji, nyie dawasco limbikizeni kodi afu mnakata juu kwa juu.

Wakija wale watoto wenzenu wa TRA na nyinyi pandisheni wazimu.

Unafiki mtupu hapa wanajua nini chakufanya basi tu na Serikali isipo kuwa makini kesho yake mtasikia Tanesco nao wametandikwa, Ebo hawa wanarinda nchi ............
 
Kampuni ikiingia ICU kwa kushindwa kujiendesha tutalalamika?

Mkuu Icadon,

Ni vigumu sana kwa DAWASCO kuingia ICU kama itafanya biashara vizuri na wateja wakubwa kama taasisi ya jeshi.

Biashara yoyote kubwa, hata kama ya maji, inatakiwa iwe na utaratibu wa kukopesha wateja kwenye biashara hii inaitwa credit facilities. Ni vigumu kuwapata wateja wa fedha taslimu kila siku, otherwise kimizania taasisi za fedha kama benki zingeshindwa kufanya kazi, kwa kuwa wakopaji wasingekuwapo (tafadhali zingatia hapa). Kukopesha au kukopa si dhambi, bali ni utaratibu wa kuhuisha biashara.

Hata makampuni makubwa kama ya magari, ndege nk nayo huwa yanawakopesha wateja bidhaa zao na suala la ICU huwa halipo. Scania Tanzania, kwa mfano, wanawakopesha wateja wao magari hapa kwa kuwa wanatambua hilo. Biashara bila mikopo haiwezekani, labda iwe ya bidhaa ndogo ndogo sana.

Kwa kesi ya Dawasco na Jeshi, mteja alikuwa ameshalipa sh milioni 690, kati ya bilioni 1.2 ambazo zilitolewa kwenye bajeti ya maji na serikali. Zilizobaki zikalipwa kwenye taasisi za maji mikoani, kwa mujibu wa taarifa ya jeshi. Kwa hali hii, ni wazi kuwa jeshi lime exhaust fedha yote.

Hata kama suppliers wangetaka kukata maji, wangeheshimu unyeti wa taasisi yenyewe, ukizingatia kuwa ndiyo yenye dhamana ya kulinda mipaka ya nchi masaa 24 kwa kutumia rasilmali zetu zilizopo, maji yakiwemo. Wangefanya mawasiliano kuhakikisha kuwa deni linalipwa, na maji hayakatwi. Naamini hili lingewezekana, maana limewezekana pia hata sasa baada ya maji kukatwa.

Kwa kazijamii, jeshi pia linasaidia katika huduma za afya na elimu (naona wengi wetu hili hatulithamini, tunafika mahali tunakejeli kwani jeshi lina kazi gani!)Jeshi ilibaki kidogo sana liifunge hospitali ya Lugalo kwa kukosa maji wakati wa mzozo huu.

Najua wengi hatuna picha ya nchi ikiwa vitani inakuwaje. Ni vigumu kuona umuhimu wa ulinzi hadi nchi inapokuwa imevamiwa, na jeshi linakwenda vitani. Lakini pia haliwezi kuonekana liko kazini (vitani) wakati wa amani. Umuhimu wa kuwa na silaha, angalau mkuki au panga chumbani kwako utauona pale tu wanapokuvamia vibaka na mapanga, unapotumia zana hizo kujiokoa.

DAWASCO wanaweza kuingia ICU wakiwakatia maji wateja wakubwa kumi tu kama jeshi, ambapo nao wataamua kuchimba visima vyao au kuweka mitambo yao mtoni kuvuta maji.

Wanajeshi walipowapiga raia ni kitendo cha kinyama pia, hakistahili kupongezwa.

Jeshi ni la wananchi na linalelewa na serikali, na halifanyi biashara ya kuweza kujiendesha lenyewe. DAWSACO ni taasisi ya umma huo huo wa waTanzania, na ni ya kibiashara. Si kweli kwamba wamefikia mahali pa kilikatia jeshi maji kwa kuwa ni wadaiwa. Kuna sababu zaidi ya hizo, na nadhani tutazijua hivi karibuni.
 
kuna wakati yule mtu aliyegundua DNA aliwahi kusema maneno hapa watu wakamsakama kuwa ni mbaguzi,wakati mwingine mie naungana naye kabisa. Tumetumia Miliion 500 kwenye sherehe za miaka 46 ya uhuru eti kuyafanya maadhimisho hayo kuwa ya kihistoria,huu ni wenda wazimu. Halafu leo watu wanatunisha misuli kwanini tunakatiwa maji sisi watu wa taasisi nyeti? huu ni ukichaa mwingine,hakuna aliyejuu ya sheria,huduma inayotolewa lazima ilipiwe na kila mtu,ukisema mimi mjeshi lazima nilipiwe na sisi madaktari tukidai haki zetu tutafika wapi. Kila mtu atimize wajibu wake

You are right! Dr. Watson alikuwa sahihi kabisa! Basi tu wanadamu tuna hulka ya kutopenda kuambiwa ukweli hasa ule unaouma. Kadri ninavyopambanua mambo yanavyokwenda shaghala bhagala kwenye nchi zetu za Kiafrika, najikuta namuunga mkono Dr. Watson kwa usemi wake kwamba amefanya utafiti na kugundua kwamba watu weupe wana akili zaidi kuliko watu weusi. Kama isingekuwa kweli, basi angalau kungekuwa na nchi kadhaa za Afrika zinazo ongozwa na weusi ambazo zingekuwa zimeendelea.

Mbaya zaidi, Tanzania ni miongoni mwa nchi za Kiafrika ambazo watu wake na viongozi wao wana mawazo mgando.
 
JWTZ wasikatiwe maji hata wakidaiwa- Mwandosya

2008-04-04 08:37:52
Na Joseph Mwendapole


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, ameagiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lisikatiwe maji hata kama linadaiwa.

Aliyasema hayo jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Matembwe (CCM), Bw. Kheri Khatib Ameir, aliyetaka kujua sakata la Jeshi hilo na Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco) limeishia wapi.

Waziri Mwandosya aliulizwa maswali na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Maji na Mifugo mara baada ya kuwasomea taarifa ya utekelezaji wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo na umwagiliaji.

Alisema Jeshi ni sehemu nyeti hivyo utaratibu wa kudai madeni unapaswa kufanywa kwa umakini wa hali ya juu tofauti na ilivyofanya Dawasco hivi karibuni.

``Sio sahihi na si busara kuwakatia maji JWTZ, tuko hapa tulipo kwa ajili yao na nisingependa tuanze kukorofishana nao,`` alisema Waziri Mwandosya.

Alisema kauli yake hiyo hainaanishi kuwa JWTZ hawapaswi kulipa bili ya maji ila utafutwe utaratibu mzuri wa kudai deni badala ya kukata huduma hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Bw. Alex Kaaya ni mmoja wa watu waliohudhuria mkutano huo.

Mbunge wa Bukene (CCM), Bi. Teddy Kaselabantu, alishauri uwekwe utaratibu mzuri wa kuvuna maji na yatumike kwa umwagiliaji badala ya kutegemea mvua.

Alishauri kamati hiyo itembelee nchi kama Misri ili wakajionee namna nchi hizo zilivyopiga hatua katika kilimo cha umwagiliaji kwa kuvuna maji.

Alisema mwaka 1984, aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Sokoine, aliahidi kujenga Bwawa kubwa la maji jimboni humo lakini ahadi hiyo bado haijatekelezwa.

``Naomba tutekelezewe ahadi hiyo kama sehemu ya kumuenzi na kumbukumbu ya Sokoine atakapotimiza miaka 25 ya kufa kwake,`` alisema.

Mbunge wa Kinondoni, Bw. Idd Azzan, alisema tatizo la maji limekuwa sehemu ya maisha ya wakazi wa Jiji la Dare s Salaam na aliomba kujua mikakati ya Wizara hiyo kukabiliana nalo.

Alisema hata vioski vilivyowekwa na Dawasco havitoi maji na kwamba anajisikia aibu anapozomewa na wapiga kura wake kwani yeye ndiye aliyekwenda kuvizindua.

``Wapiga kura wangu wananiona nafanya utapeli kwani vioski vingi havina maji na pia naomba kujua huu mradi unaosimamiwa na wachina hapa Dar es Salaam utakamilika lini na kama maji yatapatikana au la ili tupate cha kuwaeleza wananchi,``alisema Bw. Azzan.

Mbunge wa Ubungo, Bw. Charles Keenja, alisema inashangaza kuona matenki makubwa ya maji maeneo ya Kimara lakini wakazi wa maeneo hayo hawapati maji.

Bw. Keenja ambaye alikuwa Waziri wa Kilimo na Chakula katika Serikali ya Awamu ya Tatu, alisema serikali inatabia ya kutegemea wahisani hata kwa mambo ambayo yako ndani ya uwezo wake.

Alisema inashangaza kuona watanzania kila siku wanalilia maji wakati mvua zikinyesha wanayaacha bila kuyavuna.

Mbunge wa Mafia, Bw. Abdulkarim Shah Bulji, alishauri miji mikubwa itengewe fedha kwa ajili ya kujenga matenki makubwa ya kuhifadhia maji.

Aliitaka serikali pia ijifunze namna ya kurejereza maji taka kuwa maji safi kama inavyofanywa na nchi mbalimbali duniani.

Aliitaka Dawasco nayo ipeleke wataalamu wao nje kujifunza namna nchi hizo zinavyotoa huduma hiyo kwa ufanisi licha ya kuwa na vyanzo vichache vya maji.

My Take:

Uamuzi wa kukatia maji JWTZ ulikuwa ni uamuzi wa mtu asiyefikiri ambaye alikuwa anajaribu kutunisha misuli yake. Finally, somebody agrees.. JF tunamkoma nyani giledi mchana kweupeee..
 
Si bora watangaze maji bure kwa JWTZ ieleweke! Kwa mtaji huu hilo shirika litajiendesha vipi kibiashara?
 
Hivi Mheshimiwa amesema kuwa wasikatiwe maji hata kama wanadaiwa au taratibu na busara itumike katika kudai malipo kutoka kwao? Hiyo statement yao ya kuwa tuko hapa tulipo kutokana na wao sikuielewa maana hatukupata uhuru kwa mtutu wa bunduki. Au alikuwa ana maana gani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom