Kukataa mitumba tukiwa ndani ya mitumba

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
umevaa jeans la mtumba; used. Unaendesha gari 'used'. Na hata hii post unaisoma kwa kutumia laptop 'used'. Iweje sasa upinge serikali kununua vitu 'used?'
 
Unaoa au kuolewa na mtu "used". Lakini vitu vingine angalau tuepuke kununua "used" pale inapowezekana. Kwanini tununue ndege au meli used? Nafikiri ni vyombo vinavyohitaji umakini sana katika manunuzi kwa sababu vinahusisha maisha ya watu wengi. Afadhali kidogo gari used likiwa limechoka linaweza kugoma kuwaka kuliko meli inayozama au ndege inayoanguka.
 
Used ya serikali ya magamba itakuwa balaa, ikiwa sasa hivi tu sheria haijapita kuna vitu used kibao mfano x-ray, madawa n.k imagine sheria ikipita watatuletea matakataka kibao kutoka ughaibuni na kutengeza ni sawa na kununua kipya.
 
Tatizo kubwa ni kuwa kila mtu amekuwa mjanja, kiwango cha kuaminiana kimeshuka sana. MPs kimsingi sidhani kama wanakataa used ila wana hofu ya watendaji kupiga dili za nguvu, ili wanaliogopa kuliko hata usalama wenyewe.
Uchumi wetu mdogo sana hatuwezi kukwepa used things.
Hata hao precisionair n.k wanatumia ndege used, ATCL naye aruhusiwe anunue used, ila issue ni uaminifu wa watendaji ambao pengine ni mimi na wewe linapokuja suala la kununua used maana bei zake ni maelewano.
 
umevaa jeans la mtumba; used. Unaendesha gari 'used'. Na hata hii post unaisoma kwa kutumia laptop 'used'. Iweje sasa upinge serikali kununua vitu 'used?'

acha porojo!sisi ndio walipa kodi na hatutaki kodi zetu zitumike kununua vitu used.ni upuuzi kulinganisha serikali na mtu mmoja.ni ujuha kukaa bungeni kutumia muda na rasimali zetu kutunga sheria inayoruhusu ununuzi wa mitumba.kama tatizo ni fedha basi tuongeze makusanyo ya kodi za madini.
 
Hii itatoa mwanya kwa mafisadi kukomba kodi zetu. Pia vitu hivi 'chakavu' vitamaliza pesa zetu kwa matengenezo ya mara kwa mara.watanzania tuamke nafuu ni gharama
 
Hii nchi ccm imeshawashinda, tangu nchi yetu ipate uhuru huyu ndio kiongozi wa kwanza kufanya maamuzi ya kuangamiza taifa.
 
Kwa ninavyowaelewa hawa wataalam wetu wa kubandua, usikute hii sheria inatungwa kwa makusudi kukiwa tayari kuna mtumba marehemu kabisa uko pending kununuliwa na wao tayari wameshajipangia cha kwao. Kuliko kununua ndege used, bora tusiwe nazo kabisa kwani hata tulipohoji kwa nini ATCL inakwenda kwa ruzuku badala ya kuchangia pato sbb ilikuwa kuwa ni gharama kubwa za ukarabati wa vinega vyetu vikuu kuu, sasa iweje leo tukanunue ndege used? Yaani watu wazima na familia zao mishipa ya makoo imewatoka kushabikia ubadhirifu. Yanaandaa mazingira ya kuiba tu hayana lolote!

Huyo mwenye kuiuza anaiuza kwa sababu gani jamani mbona tunagoma kutumia akili zetu!!!! Hii ndio sababu sasa tunaambiwa tuoane bila kuzingatia jinsia, sababu tumeshaonekana tunaingilika.

Hapo zamani: 'NAJIVUNIA' KUWA MTANZANIA

Leo hii: 'NAVUMILIA' KUWA MTANZANIA
 
Hii sheria naona ni nzuri ila ianze kwa awamu:
Awamu ya kwanza: magari ya mawaziri, spika, naibu spika, wabunge, makatibu wakuu, wakurugenzi, RC, DC, DED, IGP, RPC, wayanunue pale autorec au carjunction halafu baada ya miaka mitano tufanye tathmini. Ikilipa tuingie awamu ya pili..... lakini kuanza na meli na treni ambazo waheshimiwa hawatazipanda...HAPANA!!!
 
mna dharura gani na hvy vitu chakavu, ndege ni anasa pandeni mabasi km sisi. Acheni kulazimisha maji yapande mlima.
 
mna dharura gani na hvy vitu chakavu, ndege ni anasa pandeni mabasi km sisi km hamtaki pandeni UNGO. Acheni kulazimisha maji yapande mlima.
 
Back
Top Bottom