Kukamatwa kwa Mbowe, jaji mkuu Chande anahusika?

Moja kwa moja, ujumbe unaopatikana ni DHARAU kwa MAHAKAMA ama anataka umaarufu kupitia vyombo vya SHERIA. Hivyo Hakimu hana makosa, mkono wa sheria umechukua MKONDO wake. Watz tuchape kazi tusiingie katika mtego wa CDM na MBOWE ambao wanataka kujipatia UJIKO kupitia MAHAKAMANI na POLISI. Maandamano endelevu wamegundua hayana mvuto badala yake wanataka MISIFA kwa kuifanya MHIMILI mmojawapo wa DOLA uonekane hauna USAFI mbele ya wananchi.

KWA KUWA AMELIKOROGA, INABIDI ALINYWE SI VINGINEVYO!!!!

Ah wapi... own goal- ccm that is!

Ni mufilisi wa strategy ndio anaweza kufanya blunder kama hii ya kwenda kumkamata Mbowe. Sasa hivi the entire nation hata hawakumbuki bunge la bajeti linaanza kesho! macho na masikio yote yameelekezwa Arusha!

Mama Spika naye kaingia mitini. hajasema chochote, but again not surprise there, bibi hajui sheria yule, so, she can hardly figure out what is going on - legally.

Tukutane kesho Arusha - CHADEMA twanga kote kote.
 
Ni jambo la kushangaza kwa wana CDM kulalama na kuitupia lawama CCM kuwa imetia mkono kukamatwa kwa Mwenyekiti wao ambaye ni mbunge Hai, Mheshimiwa Freeman Mbowe. Haingii akilini kwa watu walio makini kutotenganisha mipaka ya kazi kati ya MAHAKAMA, POLISI na CCM. Mbowe ni mjuaji wa ufanyaji kazi na taratibu za vyombo vya sheria na dola vya nchini mwetu, tena amezungukwa na jopo la wanasheria na mawakili wanaoshinda katika viunga vya mahakama kila kukicha HIVYO ni wajuzi wa masuala ya mahakama yanavyoendeshwa.

Ni jukumu la kila mshitakiwa aliye katika dhamana kuweka kumbukumbu ya siku ya kesi, tena mheshimiwa ana kitu cha ziada kwani katika kesi yao wapo washitakiwa wengi ambao haipiti siku pasipo kuwasiliana. Pia katika kesi yao wana wakili ambaye kwa mujibu wa kazi zake ni lazima aweke kumbukumbu ya tarehe za kesi zinazohusu wateja wake. Mshitakiwa kama Mbowe ambaye ni mtunga sheria na anaetetewa na wakili, katika hali ya kawaida, hataeleweka machoni mwa jamii kuwa ameshindwa kutokea MAHAKAMANI zaidi ya mara moja pasipo kutoa sababu za maandishi kwa Mahakama husika kupitia mwakilishi wake ama WAKILI.

Moja kwa moja, ujumbe unaopatikana ni DHARAU kwa MAHAKAMA ama anataka umaarufu kupitia vyombo vya SHERIA. Hivyo Hakimu hana makosa, mkono wa sheria umechukua MKONDO wake. Watz tuchape kazi tusiingie katika mtego wa CDM na MBOWE ambao wanataka kujipatia UJIKO kupitia MAHAKAMANI na POLISI. Maandamano endelevu wamegundua hayana mvuto badala yake wanataka MISIFA kwa kuifanya MHIMILI mmojawapo wa DOLA uonekane hauna USAFI mbele ya wananchi.

KWA KUWA AMELIKOROGA, INABIDI ALINYWE SI VINGINEVYO!!!!

Sina uhakika kama wewe binafsi unaelewa sheria, lakini hata hivyo hoja yako inanifanya nikuelewe kuwa na wewe umeleta ujuaji wa sheria hasa kwenye suala la mipaka ya kazi ya polisi na mahakama. Lakini naomba unieleweshe kuhusu yafuatayo:

1. Kuhusu suala la kutoa taarifa mahakamani ambayo Mh. Mbowe ameitoa kuwa ratiba shughuli za bunge zitamzuia kuhudhuria mahakamani. Je, hakimu anakana kupewa taarifa hiyo? na taarifa hiyo kama ilitolewa haikubaliki kisheria?
2. Unadhani kuwa Mh. Mbowe alishindwa kuhudhuria mahakamani kutokana kutokuweka kumbukumbu za tarehe za kesi na hivyo kusahau? Au unataka kutupotosha?
3. Unaelewa nini kuhusu suala la kinga ya Bunge?Hilo ni suala ambalo Mh. Mbowe amekuwa akililalamikia hasa alipoongea na waandishi wa habari tarehe 3/06/2011. Kinga hiyo ya bunge linazuia mahakama kutoa amri kumkamata mbunge anapokuwa katika shuguli za bunge. Pia kupitia wakili Tundu Lissu siku hiyo ya tarehe 3/06/2011 alifafanua maana ya shughuli za bunge na maeneo ya bunge na pia suala spika kuombwa ruhusa kuhusu suala la kumkamata au kumhoji mbunge kama ilivyofanyika kwa wabunge wa CCM. Je hilo unalichukuliaje?
4. Kwanini hujatoa ufafanuzi wa kisheria kabla ya kukimbilia kwenye hoja ya Mh. Mbowe kutokuwa juu ya sheria. Hoja yako haikueleza chochote kisheria juu suala hilo bali umeenda moja kwa moja kwenye hitimisho. Huoni hiyo ni kasoro kubwa katika hoja yako hasa kwa sababu jambo lenyewe linahusu sheria?
 
Jamani hivi mnapata faida gani katika uzushi? Una maana gani unaposema WABUNGE WOTE WA CDM? Niko hapa na Mh. Mbunge wa BIHARAMULO (CDM) Dr. Mbassah tumemaliza kusali ibada ya misa takatifu na 2napata lunch sa hii. Au ye c mbunge kupitia cdm?
 
Ni jambo la kushangaza kwa wana CDM kulalama na kuitupia lawama CCM kuwa imetia mkono kukamatwa kwa Mwenyekiti wao ambaye ni mbunge Hai, Mheshimiwa Freeman Mbowe. Haingii akilini kwa watu walio makini kutotenganisha mipaka ya kazi kati ya MAHAKAMA, POLISI na CCM. Mbowe ni mjuaji wa ufanyaji kazi na taratibu za vyombo vya sheria na dola vya nchini mwetu, tena amezungukwa na jopo la wanasheria na mawakili wanaoshinda katika viunga vya mahakama kila kukicha HIVYO ni wajuzi wa masuala ya mahakama yanavyoendeshwa.

Ni jukumu la kila mshitakiwa aliye katika dhamana kuweka kumbukumbu ya siku ya kesi, tena mheshimiwa ana kitu cha ziada kwani katika kesi yao wapo washitakiwa wengi ambao haipiti siku pasipo kuwasiliana. Pia katika kesi yao wana wakili ambaye kwa mujibu wa kazi zake ni lazima aweke kumbukumbu ya tarehe za kesi zinazohusu wateja wake. Mshitakiwa kama Mbowe ambaye ni mtunga sheria na anaetetewa na wakili, katika hali ya kawaida, hataeleweka machoni mwa jamii kuwa ameshindwa kutokea MAHAKAMANI zaidi ya mara moja pasipo kutoa sababu za maandishi kwa Mahakama husika kupitia mwakilishi wake ama WAKILI.

Moja kwa moja, ujumbe unaopatikana ni DHARAU kwa MAHAKAMA ama anataka umaarufu kupitia vyombo vya SHERIA. Hivyo Hakimu hana makosa, mkono wa sheria umechukua MKONDO wake. Watz tuchape kazi tusiingie katika mtego wa CDM na MBOWE ambao wanataka kujipatia UJIKO kupitia MAHAKAMANI na POLISI. Maandamano endelevu wamegundua hayana mvuto badala yake wanataka MISIFA kwa kuifanya MHIMILI mmojawapo wa DOLA uonekane hauna USAFI mbele ya wananchi.

KWA KUWA AMELIKOROGA, INABIDI ALINYWE SI VINGINEVYO!!!!

Andika ujumbe Kama hizi buku kumi kwa wajinga wenzio
 
SHERIA KUFUATA MKONDO WAKE!!!! Katika nchi hii? Hebu temeni mate chini jamani, msiwe mnaleta vitu ambavyo havipo katika utawala wa JK. Sheria ingekuwa inafuata mkondo wake -- saa hizi akina Rostam, Chenge na wengineo wangekuwa lupango wanatumikia vifungo vya makumi ya mvua!!! Eti sheria inafuata mkondo wake! Shit a 100 times!!!!

Ndugu Mafilili -- tukubaliane kitu kimoja: Sheria inafuata mkondo wake iwapo wakosaji watakuwa ni kutoka vyama vya upinzani, au kama ni wa CCM, basi ni wale dagaa, au isiyowataka!

Unataka mifano? Loo nitakutajia hadi majogoo ya alfajiri ya kesho. Wengine wanisaidie kutoa mifano.

Hawa CDM wanataka kuliweka hilo hadharani -- undumila kuwili wa polisi wa CCM na vyombo vyake vya sheria.

Kuna mtoa mada mmoja humu ndani jana alisema haioni picha ya kiongozi yoyote wa magamba (wale wa magwanda ya kijani) akiteremshwa jukwaani na kukamatwa na na polisi kwa kuzidisha muda wa kuhutubia mkutano. Hivi kuna uonngo katika hili?
 
Kwa jinsi hali ya mambo ilivyobadilika ghafla, kuna uwezekano mkubwa sana huyu mheshimiwa akaenda jela miezi 3 kwa kosa la kuidharau mahakama. Pia kwa kesi ya awali ya maandamano bila kibali dhamana yake itafutwa, na maombi ya dhamana kusikilizwa upya. Hii inalenga kuonyesha umma kuwa mahakama sio chombo cha kuchezea, na kwamba nchi yetu inaheshimu utawala wa sheria. CDM wajiandae kisaikolojia kwa kitakachotokea mahakamani Arusha kesho alasiri.

Hakuna jambo linalomshtua yeyote kati ya hayo unayoota. Afadhali ungeota kuwa nchi hii itaingia katika machafuko na ndoto ya namna hiyo ingeliesaidia labda wenye hekima wanaweza kutookoa tusiingie huku. Kwa aina ya ndoto zako unazoota hakika Tanzania itaangamia pamoja na wewe.
 
Mwandishi anahitaji maombezi. Keshasahau kuwa kuna mihimili mitatu ya DOLA na sina hakika kama anafahamu maana ya DOLA.
============

Sikubaliki

Nimesoma hiyo makala, nadhani mwandishi haitaji maombezi bali pongezi.
Anachosema mwandishi ni kuonyesha wasiwasi wetu pale Jaji Mkuu anapokuwa Mkuu wa mhimili wa mahakama, na hapo hapo kwa mazingira akaonekana ni sehemu ya "executive" branch ya dola. Sasa hiyo executive ndiyo anaiita "serikali".
Dola ni muungano wa mihimili yote mitatu.
 
Salama wakuu,najua kuna thread nyingi sana zinazohusu kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe. Freeman Aikael Mbowe,MB/KUB.Naomba mods waiache hii japo kwa masaa mawili ijadiliwe kisha iunganishwe na thread nyingine mama.....

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari juzi na ile ya Mnadhimu mkuu wa kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe. Tundu Lissu,MB ilielezwa kwamba Mhe Mbowe hatajisalimisha Polisi kama alivyotakiwa afanye,lakini jana tunaelezwa kwamba Mhe. Mbowe amejisalimisha na kukamatwa....Swali ni je,ina maana Mhe. Lissu alikuwa anampotosha Mhe. Mbowe?,natatizilka kidogo hapa.....

Hebu angalia Habari hii ya Gazeti la Tanzania Daima la jana;

Mbowe agoma kuipigia magoti mahakama

na Bakari Kimwanga

MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amekataa kujisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iliyoamuru akamatwe kwa kosa la kutotii amri ya kufika mahakamani hapo.

Bila kumung’unya maneno, Mbowe alisisitiza kutojisalimisha akisema, “Ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nikiwa nimepiga magoti!”

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, alisema walishatoa ombi mbele ya Hakimu Mkazi Charles Magesa la kuruhusiwa kushiriki vikao vya kamati ya Bunge kwa mujibu wa nafasi zao, ambalo lilikubaliwa na mahakama hiyo.

Alisema katika ombi hilo, waliomba dhamana yao iendelee wakiwa nje jambo ambalo pia mahakama hiyo ililiridhia, hivyo kuwa na uhuru wa kushiriki vikao vya kamati ya Bunge la bajeti litakaloanza Juni 7, mwaka huu.

Alisema kutokana na maombi hayo, mahakama iliamuru wabunge wote waendelee na majukumu yao ikiwemo kushiriki vikao vya kamati za Bunge lakini baada ya siku chache alishangaa kusikia anatakiwa kukamatwa.

“Siwezi kuzuia hali hii, najua kuna jambo vyombo vya usalama vinataka kufanya ikiwemo kuwadhoofisha wabunge wa vyama vya upinzani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea bajeti ya nchi.

“Kwa nafasi yangu ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni ni mjumbe wa Kamati ya Fedha ya Bunge, na ninasimamia serikali kivuli katika kuandaa maoni ya kambi ya upinzani, sasa kama wao wanaona wana haki ya kunikamata wafanye hivyo, lakini ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nikiwa nimepiga magoti… sitafanya hivyo kama wanavyotaka hata kidogo,” alisisitiza Mbowe.

Alisema yeye na chama chake hawawezi kukaidi amri ya mahakama ila kinachotakiwa ni mahakama yenyewe kutanguliza busara kuliko kutanguliza utashi na shinikizo la kisiasa kutoka kwa watawala.

Hivyo, alisema kilichofanyika dhidi yake na watu waliomdhamini ni udhalilishaji hasa kwa nafasi yake kama Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu, alisema kambi yao imepokea kwa mshtuko, masikitiko na mshangao mkubwa taarifa za Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha kutoa amri ya kumkamata Mbowe.

Alisema kiongozi wao hakuhudhuria mahakamani mara mbili kwa kuwa alikuwa akihudhuria vikao vya kamati mbalimbali za Bunge vilivyoanza Mei 23 mwaka huu.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na amri ya kumkamata Mheshimiwa Mbowe kwa vile inakiuka moja kwa moja sheria, mila na desturi za miaka mingi zinazohusu kinga, haki na mamlaka ya Bunge na ambazo ni msingi mkuu wa demokrasia yetu ya kibunge.

“Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatambua na kulinda uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge
.

“Uhuru huu wa Kikatiba umetiliwa mkazo katika vifungu vya 5, 6 na 11 vya Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge ya mwaka 1988 vinavyokataza mbunge kukamatwa au kupewa amri ya kuhudhuria mahakamani wakati akiwa ndani ya eneo la Bunge au wakati Bunge limekutana bila kuwepo kwa kibali cha Spika,” alisema Lissu ambaye ni mwanasheria kitaaluma.

Alisema maneno ‘eneo la Bunge’ yametafsiriwa na kifungu cha pili cha sheria hiyo kumaanisha “ukumbi ambao hutumiwa kwa vikao vya Bunge, pamoja na ofisi, vyumba, vibambaza, maeneo ya wageni, bustani na maeneo mengine yaliyowekwa kwa ajili ya matumizi au malazi ya wajumbe, maafisa au wageni wa Bunge pamoja na njia zinazounganisha maeneo hayo na maeneo mengine yanayoweza kutangazwa na Spika kuwa ndani ya maeneo ya Bunge
.

Alisema kwa maana hiyo, mbunge anapokuwa anahudhuria vikao vya Bunge au kamati zake au anapokuwa mahali pengine popote kwa kuitikia wito wa kuhudhuria vikao hivyo vya Bunge hawezi akakamatwa ili kutekeleza amri ya mahakama au ya chombo kingine chochote nje ya Bunge.

Akigusia kile alichokiita ‘upendeleo’, Lissu alisema inashangaza kuona wabunge wa upinzani wakikamatwa na polisi bila kuomba kibali kwa Spika, lakini wanapotaka kuwakamata wabunge wa CCM hufanya hivyo.

Alisema wabunge wa kambi ya upinzani waliokamatwa kinyume cha sheria ni Freeman Mbowe (Hai), Godbless Lema (Arusha Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Meshack Opulukwa (Meatu), Ester Matiko (Viti Maalum CHADEMA) Felimon Ndesamburo (Moshi Mjini), Joseph Selasini (Rombo) na Madgalena Sakaya (Viti Maalum CUF).

Akitoa ushahidi wa vibali vinavyoombwa pindi polisi inapotaka kuwakamata wabunge wa CCM, alionyesha barua ya mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Mwanza SP B.M. Wakulyamba kwenda kwa Katibu wa Bunge, ambayo ilimwomba ruksa ya kumhoji Mbunge Dk. Titus Kamani (Busega, CCM) kuhusiana na njama za kutaka kumuua aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Dk. Raphael Chegeni.

Kutokana na hali hiyo alisema hakuna mbunge hata mmoja wa CHADEMA au chama kingine cha upinzani ambaye kwa taarifa zao amewahi kuombewa kibali cha kukamatwa na polisi kama inavyoonekana kwa wabunge wa CCM.

Alisisitiza kuwa hali hiyo inadhihirihisha upendeleo wa wazi wa Jeshi la Polisi kwa wabunge wa CCM na uonevu kwa wapinzani.

“Tutapinga kwa nguvu zetu zote kitendo chochote cha kumtishia au kumkamata kiongozi wa kambi ya upinzani,” alisema.

Alisema wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha inatoa amri ya kumkamata Mbowe, kiongozi huyo tayari analindwa na kinga ya Bunge.

“Mbowe ataendelea kulindwa na kinga hiyo kwa kipindi chote cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano pamoja na muda muafaka na wa kutosha kama unavyotambuliwa katika mila na desturi za Mabunge ya Jumuiya ya Madola hadi baada ya kwisha mkutano huo,” alisema mnadhimu huyo.

Na hii hapa chini ya Gazeti la leo la Mwananchi;

Mbowe, Zitto mbaroni

Saturday, 04 June 2011 22:08

Waandishi Wetu
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe jana alitiwa mbaroni na Jeshi la Polisi baada ya kujisalimisha katika kituo Kikuu cha jijini Dar es Salaam.Katika hatua nyingine, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, jana alikamatwa na polisi mjini Singida kwa kosa la kuzidisha muda wa kuhutubia mkutano wa hadhara.Habari zilizopatikana kutoka Singida na kuthibitishwa na Zitto mwenyewe, zinaeleza kuwa polisi walimkamata jana jioni kwa madai kuwa alihutubia mkutano wa hadhara mpaka zaidi ya saa 12:00. Muda wa mwisho kisheria kuhutubia mkutano wa hadhara ni saa 12:00 jioni."Mpaka sasa bado nipo polisi wanaendelea kunihoji," alisema Zitto kwa kifupi.

Hadi tunakwenda mitamboni, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alikuwa bado ameshikiliwa katika Kituo cha Polisi mjini Singida.Kukamatwa kwa Mbowe kunafuatia amri ya mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuamuru akamatwe popote alipo na kufikishwa mahakamani kwa kutotii amri ya kufika mahakamani katika kesi yake.

Juni 2 mwaka huu, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa, alikubaliana na hoja ya wakili upande wa Serikali kuitaka mahakama kutoa amri ya kukamatwa kwa Mbowe kwa sababu ya kutotii amri ya kufika kortini au kumtuma mdhamini wake.Alisema sababu iliyotolewa mahakamani hapo kwamba mshtakiwa huyo ni mbunge na yupo kwenye vikao vya Kamati za Bunge haina uzito kwa kuwa hiyo ni moja ya shughuli zake kama ilivyo shughuli nyingine kwa watumishi wa Serikali.

Hakimu Magesa akitoa agizo hilo alisema kuwa inachokumbuka ni kwamba mahakama hiyo ilipokea maelezo ya kuwa washtakiwa hawatahudhuria mahakamani hapo Mei 27, mwaka huu na kwa sababu ya kuwapo vikao vya kamati za Bunge iliagiza wafike wadhamini wao kesi inapotajwa. Ndiyo maana Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, alimpeleka mdhamini.Katika kesi hiyo iliyopangwa kuendelea kusikilizwa kesho, Mbowe na wenzake wanashtakiwa kwa kosa la kufanya kusanyiko lisilo halali Januari 5, mwaka huu jijini Arusha.

Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwanasheria wa chama hicho, Mabere Marando alithibitisha jana kukamatwa kwa Mbowe saa 9:00 alasiri kutokana na amri ya mahakama."Ni kweli amekamatwa saa moja iliyopita kwa sababu ni amri ya mahakama na chama hakiwezi kumwombea dhamana itabidi apelekwe Arusha," alisema Marando.

Pamoja na Marando kuthibitisha kukamatwa kwa Mbowe, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema halina taarifa zozote za kukamatwa kwa mwenyekiti huyo.Jeshi hilo limesema halina taarifa zozote juu ya mwenyekiti huyo kujisalimisha katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam. Mei 27, mwaka huu, mahakama hiyo ilitoa hati ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani hapo kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na Mwenyekiti wake, Mbowe.

Pamoja na viongozi hao, mahakama hiyo pia iliamuru wabunge wawili wa chama hicho, Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini) na Godbless Lema (Arusha Mjini) wakamatwe na kufikishwa mahakamani baada ya kushindwa kuhudhuria mara kadhaa . Lakini, viongozi hao waliwasiliana na mahakama hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi wa suala hilo hakupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita bila ya kupokelewa.
Awali asubuhi, akizungumza na gazeti hili ofisini kwake, Kamanda Shilogile alisema kuwa hana taarifa zozote za Mbowe kukamatwa au kujisalimisha katika kituo hicho.

“Sina taarifa zozote kuhusiana na kukamatwa kwa Mwenyekiti cha Chadema. Taarifa hizi ndiyo nazisikia kwenu waandishi wa habari. Mimi wala uongozi wangu hauna taarifa hizo,”alisema Shilogile na kuongeza;
“Angekuwa amekamatwa au amekuja kujisalimisha mkoa wangu ndiyo ungekuwa wa kwanza kupata taarifa hizo, labda mtafute Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kama ana taarifa hiyo anaweza kukwambia.”Kova alipotafutwa kwa njia ya simu alisema yuko Zanzibar na kwamba hana taarifa zozote za kukamatwa kwa Mbowe.

Marando, Tundu Lissu
Mapema asubuhi Marando na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu walionekana wakiingia katika Ofisi ya Mpelelezi wa Mkoa wa Ilala (RCO), Diwan Nyanda.Alipoulizwa ujio wake katika ofisi hizo, Marando alisema kuwa alikwenda katika ofisi hizo kwa shughuli zake binafsi na kwamba hana taarifa za kukamatwa kwa Mbowe.

Akizungumza na Mwananchi Alhamisi wiki hii baada kutolewa amri ya kukamatwa kwake, Mbowe alisema anatarajia kutoa tamko kuhusu suala hilo Ijumaa jijini Dar es Salaam.“Nitatoa tamko kesho, lakini nasikitishwa na tafsiri hii ya Mahakama kwamba mimi nimekaidi amri ya kufika katika vikao vya mahakama...,” alisema Mbowe

Mnyika
Katika hatua nyingine Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) amesema chama hicho kitaandika barua rasmi katika Ofisi za Bunge kueleza jinsi wabunge wa vyama vya upinzani wanavyokamatwa bila kufuata kanuni na taratibu, wakati wana kinga ya kibunge inayowazuia kukamatwa bila kibali.

Alisema mpaka sasa wabunge wa upinzani ambao wamewahi kukamatwa bila kuombwa kwa kibali chochote kutoka kwa Spika wa Bunge ni pamoja na Godbless Lema (Arusha Mjini), Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini), Joseph Selasini (Rombo), Meshack Opulukwa (Meatu)

Wengine ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Esther Matiko (Viti Maalumu-Chadema) na Magdalena Sakaya (Viti Maalumu-CUF) ambaye mpaka sasa yuko mahabusu mkoani Tabora huku kesi yake inatarajiwa kutajwa Juni 6 mwaka huu.

Imeandikwa na Hadija Jumnne, Fidelis Butahe na Edward Qorro

Swali: Ilikuwaje Mhe. Mbowe akabadili maamuzi yake ya kujisalimisha ilihali analindwa na kinga, haki na mamlaka ya Bunge(kwa mujibu wa Mhe. Tundu Lissu,MB)

Hivi kanuni na taratibu zinasemaje kuhusiana na kinga ya wabunge kukamatwa na Polisi/Vyombo vya sheria...Mipaka ya kanuni hii ikoje?.....Naomba waelewa wanijuze hili...

Bala.
 
Msingi wa yote ni DHARAU kwa mahakama wala haina uhusiano na vikao vya bunge. Usitoke nje ya reli, MBOWE AMEDHARAU MAHAKAMA KWA KUTOTOA TAARIFA SIKU ZA KESI

Una uhakika na hicho unachosema? Taarifa ilitolewa kabla ya siku hiyo ya kesi. wewe unazungumzia taarifa gani?
 
Leo ni siku ya kihisitoria hapa Tanzania, hasa jijini DSM.

LENGO NI KUPINGA UGANDAMIZAJI WA DEMOKRASIA NA UONEVU DHIDI YA WATETEZI WA WANYONGE.

KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI NA NAIBU WAKE KUKAMATWA NA KUSHIKILIWA SIKU CHACHE KABLA YA KIKAO CHA BAJETI NI DALILI ZA WIZI UNAOTARAJIWA KUFANYWA NA WAKUBWA BUNGENI.

================
UPDATES katika picha:

lipumba-ndani.jpg

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Lipumba akifika katika kituo cha polisi kati kwa nia ya kumdhamini Mbowe
bango-mojawapo.jpg

Bango mojawapo lililokuwa limeshikiliwa na wafuasi wa CHADEMA lililonaswa na Polisi maeneo ya Magomeni
a.jpg

Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akihojiwa na mwandishi wa shirika la habari BBC - Central Police
CDM-polisi.jpg

Polisi wakiwa na bendera na mabango waliyokamata eneo la Magomeni (Travatine Hotel)
washawasha.jpg

Gari maalum la kikosi cha kutuliza ghasia likiwa limeegeshwa tayari (Central Police) kusubiri amri ya kamanda wa polisi kuwatawanya wafuasi wa Chadema
walokamatwa.jpg

Hali ilikuwa hivi maeneo ya Magomeni
central-ulinzi.jpg

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU wakiwa wameimarisha ulinzi katika kituo cha polisi kati ambako anashikiliwa Mbowe.
CDM-followers-1.jpg

Wafuasi wa CHADEMA wakiondolewa Central Police

Hali Magomeni ilikuwa kama inavyoonekana chini:
maandamano-dar-1.jpg

polisi-dar.jpg

polisi-dar2.jpg

polisi-1.jpg

alokamatwa.jpg

Mtuhumiwa mmojawapo aliyekamatwa akihojiwa
machozi-mabomu.jpg

islam-machozi.jpg

Maji yaligeuka bidhaa muhimu kupunguza makali ya mabomu
 
SHERIA KUFUATA MKONDO WAKE!!!! Katika nchi hii? Hebu temeni mate chini jamani, msiwe mnaleta vitu ambavyo havipo katika utawala wa JK. Sheria ingekuwa inafuata mkondo wake -- saa hizi akina Rostam, Chenge na wengineo wangekuwa lupango wanatumikia vifungo vya makumi ya mvua!!! Eti sheria inafuata mkondo wake! Shit a 100 times!!!!

Ndugu Mafilili -- tukubaliane kitu kimoja: Sheria inafuata mkondo wake iwapo wakosaji watakuwa ni kutoka vyama vya upinzani, au kama ni wa CCM, basi ni wale dagaa, au isiyowataka!

Unataka mifano? Loo nitakutajia hadi majogoo ya alfajiri ya kesho. Wengine wanisaidie kutoa mifano.

Hawa CDM wanataka kuliweka hilo hadharani -- undumila kuwili wa polisi wa CCM na vyombo vyake vya sheria.

Kuna mtoa mada mmoja humu ndani jana alisema haioni picha ya kiongozi yoyote wa magamba (wale wa magwanda ya kijani) akiteremshwa jukwaani na kukamatwa na na polisi kwa kuzidisha muda wa kuhutubia mkutano. Hivi kuna uonngo katika hili?

Ntakusaidia mfano mmoja: Nchi hii kuna kundi la watu hutoa roho za wenzao kwa kuwapiga risasi lakini hawaguswi. Wanaoguswa na kutiwa misukosuko ni wengine. Rudi nyuma kuanzia 1998 (Membe Chai), 2001 (Pemba), 2011 (Arusha). Hakuna kosa kubwa la jinai kama kumuuwa mtu, lakini hapa Tanzania siyo kosa kabisa iwapo ni polisi wakifanya hivyo -- na ndiyo maana nchi hii haiwezi kutulia kamwe.

Huko Misri yule dikteta Mubarak sasa anashitakiwa kwa kuuwa waandamanaji wasio na silaha -- kama vile Pemba na Arusha. JK anaichezea sana nchi hii! I warn him.
 
Bala

regardless on how you analyse this, sheria nchi hii zipo valuvalu kwasbabu zilikua za chama kimoja, tukaweka viraka weee hadi sasa matak0 yetu yapo wazi.

Mbowe hayupo juu ya sheria na kamwe hatakiwi kuwa juu ya sheria and that is what CDM is fighting for, to prevent people who abuse the law... Tatizo pia mbowe analindwa na sheria hiyohiyo kama kiongozi wa upinzani

WHAT WE SAW LAST WEEK HADI JANA NI UPUUZI WA SYSTEM YETU KUJUA NANI YUPO WAPI NA ANAFANYA NINI KIASI CHA KUISHIA KUKANGANYANA WENYEWE.... haikua na haja ya kuhangaika na mbowe wakati kuna ofisi za bunge na mahakama na bunge zingemaliza haya mambo bila promo

my personal view... Magesa hana makosa, mbowe hana makosa... poor communication na intelligence (intended or unintended) ndio tatizo, but i would also blame lawyer wa mbowe sana tu!!

UPUMBAVU WA MFUMO WETU UNATUTESA SANA....
 
Cdm tunawaamini mtatafakari na kujipanga jinsi ya kuhandle hili - we have no doubt on your wisdom, mitego no mingi hapa nchini hila zao ni wazi

go go cdm
 
Hatuna haja ya kuitana wapumbavu..etc...tujadili hoja zenye tija na weledi, si matusi.

Nawasilisha.[/QUOTE]

umenena vyema..tunaitaji watu kama wewe hapa jf..
 
Back
Top Bottom