kujivunia jinsia

Ndio tuone lugha yetu ya kiswahili ilivyongumu.... kujivunia ninakokuongelea mimi ni ile hali ya kufurahia,kuona fahari,kuridhika...( feel proud).

Yep, ndio vilevile nilivyokuwa namaanisha mimi..yaani kujiona uko juu..kuwa proud..kujiona flani ivi..kujiona matawi ..(=kujitapa, kwa sababu huwezi kujitapa kama hujioni au kujidhanii upo std ya juu..) etc..the same same.
 
kuna mantiki katika hili? Naona mmoja kasaini kuwa anashukuru Mungu kuwa mwanamke. mi nadhani ni ajali ya kibaiolojia tu kama ilivyo kwa imani ambayo ni matokeo ya kimazingira tu. umeshawahi kuwaza ungekuwa kinyume na jinsia uliyo nayo?

Sioni kama kuna ubaya kujivunia jinsia yako (kujikubali), hata kama ni ajali ya kibaolojia maana kuna baadhi ya watu hujikana kwa kubadili jinsia zao.
 
Accorading to sigmund freud, wanawake wanatamani kuwa na dhakari- ikimaanisha kuwa wanaume. Hata katika jamii zetu hii hali ipo. Mwanamke akivikwa uanaume hachukii, ila ni kinyume. Bado hii haimaanishi kuwa naitetea jinsia moja
 
Accorading to sigmund freud, wanawake wanatamani kuwa na dhakari- ikimaanisha kuwa wanaume. Hata katika jamii zetu hii hali ipo. Mwanamke akivikwa uanaume hachukii, ila ni kinyu
me. Bado hii haimaanishi kuwa naitetea jinsia moja

Wanawake wanaotamani kuwa wanaume wana kasoro. Vivyo hivyo wanaume (hata kama ni wachache kiasi gani) wanaotamani kuwa wanawake wana kasoro. Ni watu wasiojikubali walivyo. Ndo maana kutokana na kutokujibali unakuta watu hao wanafanya operesheni ili kuchukua jinsi ambayo Mungu hakuwapa.
 
Back
Top Bottom