kujivunia jinsia

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,848
2,669
kuna mantiki katika hili? Naona mmoja kasaini kuwa anashukuru Mungu kuwa mwanamke. mi nadhani ni ajali ya kibaiolojia tu kama ilivyo kwa imani ambayo ni matokeo ya kimazingira tu. umeshawahi kuwaza ungekuwa kinyume na jinsia uliyo nayo?
 
kwahiyo ww (nachukulia ww ni mwanaume)hua unatamani ungekua mwanamke???kama hujaridhika na ulivyo huwezi kujivunia....mpaka hapo unataka ulichokosa!!nenda China ukanunue kama wenzako!
 
Kujivunia jinsia ni sawa sawa na kuji vunia utaifa wako. Kusema namshukuru Mungu kwa kuwa jinsia fulani ni sawa na kusema ume ridhika na jinsi Mungu alivyo kuumba. Hakuna ubaya wowote, hata mimi naji vunia kuwa mwanaume.
 
I'm proud to be a woman. Ww Mziwanda hujivunii na huo ujinsia wako wa kuwa Female/male?
 
Huwezi ukajivunia kitu ambacho hujakifanyia kazi..simple logic points that way.
 
Unai fanyiaje kazi jinsia? sija kuelewa hapa?

Ni vizuri umeuliza .. Ninachosema ni kuwa simple logic inatudai tujivunie kitu ambacho umekitolea jasho au juhudi ya namna fulani. Mathalani mzazi anajivunia kuona mtoto wake amefaulu shuleni n.k. Huwezi ukajivunia kwa haki kitu ambacho hujakifanyia juhudi yeyote ile kufikia hali yake iliyopo.
 
Huwezi ukajivunia kitu ambacho hujakifanyia kazi..simple logic points that way.

mkuu umeongea pwent hapo! Kuna mmoja kaniambia niende china nikabadilishe jinsia (niwe dem). Kuwa jinsia uliyo nayo ni kwa neema tu. Jivunie ur achievements
 
Huwezi ukajivunia kitu ambacho hujakifanyia kazi..simple logic points that way.

usipojivunia ni kuwa unatamani kile ambacho hukupewa na utakuwa miserable kwa maana hutaweza kubadilisha.Ukibadilisha ndo utaonekana.........
Nadhani mtu mwenye moyo wa kujivunia kile alichonacho hata kama hakukifanya yeye anastahili pongezi.
 
Ume nena dada. Ni sawa na kujivunia kuwa Mtanzania. Hauku chagua kuzaliwa Mtanzania ume jikuta hivyo. Ila nita shangaa kweli kumsikia mtu hajivunii kuwa Mtanzania.
 
Nilishasema kuwa baadhi ya mambo ni kwa neema tu. Hayo kiasili tunayaacha. Wakati mwingine kujivunia jambo la asili ni kujipa moyo tu. Mwanaume aliyezaliwa na homoni nyingi ya kike atajivunia?
 
Wapo wanao jivunia. Ume sikia kitu kinaitwa gay pride Marekani?
 
usipojivunia ni kuwa unatamani kile ambacho hukupewa na utakuwa miserable kwa maana hutaweza kubadilisha.Ukibadilisha ndo utaonekana.........
Nadhani mtu mwenye moyo wa kujivunia kile alichonacho hata kama hakukifanya yeye anastahili pongezi.

Hiyo sentensi bold sijaelewa chanzo chake. Kwa hiyo unataka kusema kwamba mtu asipojivunia (kujitapa??) kuwa yeye ni mwanaume basi ina maana anatamani kuwa mwanamke, and vice versa? Na pia ina maana hajikubali alivyo?

Naona hapa kuna tatizo..
 
Last edited:
Ume nena dada. Ni sawa na kujivunia kuwa Mtanzania. Hauku chagua kuzaliwa Mtanzania ume jikuta hivyo. Ila nita shangaa kweli kumsikia mtu hajivunii kuwa Mtanzania.

Mimi binafsi sijivunii (sijipigii chapuo) utanzania. Siwakosoi wanaotaka kufanya hivyo kwa sababu huenda wanazo sababu zao kufanya hivyo, hata kama sio valid sina sababu ya kupigizana nao kelele. Kwa kifupi sioni kwa nini niringie utanzania au uanaume wangu. Sioni.
 
Nilishasema kuwa baadhi ya mambo ni kwa neema tu. Hayo kiasili tunayaacha. Wakati mwingine kujivunia jambo la asili ni kujipa moyo tu. Mwanaume aliyezaliwa na homoni nyingi ya kike atajivunia?

Kujivunia jinsia ni kujikubali, kujipokea ulivyo, tena kujipokea kwa kishindo. Ndo maana mtu anamshukuru Mungu. Anajua ni jambo alilopewa na Mungu bure. Kumbe lazima ku-appreciate hata yale mambo ambayo ni ya asili. Ni kutambua uuumbaji wake Mungu.
 
kuna mantiki katika hili? Naona mmoja kasaini kuwa anashukuru Mungu kuwa mwanamke. mi nadhani ni ajali ya kibaiolojia tu kama ilivyo kwa imani ambayo ni matokeo ya kimazingira tu. umeshawahi kuwaza ungekuwa kinyume na jinsia uliyo nayo?

'Kujivuna' na 'kushukuru' zina maana sawa?

Mtu anayejivunia jinsia yake anafanya nini hasa?(anadharau jinsia nyingine?)
 
kujivunia na kushukuru ni vitu viwili tofauti. jinsia, imani, uraia- hivyo ni vya kushukuru tu kwani tunavyo kwa neema. jivunie kufikisha post 10,000, kuwa na elimu bora, mali ulizo nazo. vile ambavyo umeweza kuvifanya kutokana na ulivyo. kujivunia jambo ni matunda ya ulivyo na si ulivyo. jivunie kile ambacho umeweza kufanya kama mwanaume/mwanamke
 
Mimi naona hakuna haja ya kujivunia jinsia. Na swala hili huwa linafanywa zaidi na wanawake ( samahamani kwa kusema huo ukweli), pale inapotokea kuna hali fulani ya mwanamke kuona au kuhisi amedharauliwa huwa anajivunia jinsia yake. Binadamu wote ni sawa na sidhani kati yetu kama kuna aliyewahi kuomba kuwa na jinsia aliyo nayo.
 
Hiyo sentensi bold sijaelewa chanzo chake. Kwa hiyo unataka kusema kwamba mtu asipojivunia (kujitapa??) kuwa yeye ni mwanaume basi ina maana anatamani kuwa mwanamke, and vice versa? Na pia ina maana hajikubali alivyo?

Naona hapa kuna tatizo..
Ndio tuone lugha yetu ya kiswahili ilivyongumu.... kujivunia ninakokuongelea mimi ni ile hali ya kufurahia,kuona fahari,kuridhika...( feel proud).
 
Back
Top Bottom