Kujivua gamba: Maoni yangu

COMPLICATOR2011

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
253
35
Ndugu zangu jana nimesikiliza kipindi cha JUNGU KUU cha TBC taifa, kilichonishangaza ni kusikia eti wananchi wa Igunga 11 wamezimia baada ya kusikia mbunge wao kaachia ngazi, sasa kali zaidi ilikuwa pale watoa maoni wote karibia 99% walikuwa wakimpongeza Mh. huyo kujiuzuru eti kafanya la maana, sasa mimi sijaelewa Rostamu kafanya uzuri gani kiasi cha kupongezwa? ILITAKIWA AENDE MAHAKAMANI KUKANA MASHITAKA YOTE NA SIO KUTUDANGANYA, CCM hapa msijisifu kwa lolote hamna kilichofanyika ni usanii mtupu. MWENYE MASIKIO NA ASIKIE.
 
Rostam ali-orchestrate vizuri sana toka press conference kule Igunga hadi tbc. Wa Igunga walipangwa na pia wachiangiaji wa tba nao walipangwa ili rostam aonekane anaungwa mkono na wengi. Siasa za bongo hizi
 
Kwa namna hii hakuna tunakoelekea, nasikia monduli nako ukitaka kupigwa mawe mseme vibaya lowasa hivyo hivyo na Bariadi
 
King maker!
siyo mchezo.....
 
Kwa namna hii hakuna tunakoelekea, nasikia monduli nako ukitaka kupigwa mawe mseme vibaya lowasa hivyo hivyo na Bariadi

Kwa taarifa yako sio munduli tu, hata bungeni na ndani ya kamati za chama ukitaka upigwe mseme vibaya Lowasa, ndiyo maana wakati anachangaia Hoja ya waziri mkuu alikuwa anashangiliwa mwanzo mwisho! Lowasa tuko nyuma yalo hakuna kujivua gamba wajivue magamba hao wanafiki wanaofanya siasa uchwara.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom