Kujivua gamba hakusadifu maudhui

mwana wa africa

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
548
128
Nimejaribu kutafuta maana na tafsiri sahii ya usemi "kujivua gamba" . Neno gamba kwa maana pana ni kama nyumba au kitu mfano wa container lkinachotumika kuhifadhia kitu/vitu fulani; kwa msingi huo kilio cha watanzania wengi cha kutaka mabadiliko ya kweli kwa wanaoitakia mema nchi hii hakitapata muarobaini . Hivyo basi tusitegemee mabadiliko yoyote kwa sababu, nyoka anapojivua gamba ni ishara ya kukua na kutengeneza gamba kubwa zaidi.
 
AJIRA ZA KUTEUANA SERIKALINI: KWA NINI WATU TUENDELEE KURUHUSU MFUMO WA KUTEUANA KIITIKADI ZA KISIASA ILHALI MALIPO YA GHARAMA ZA UENDESHAJI SERIKALI WATU TUKAZIBEBE KITAIFA ZAIDI KWA KILA MMOJA WETU???????????


Picha+no+3.JPG

Tanzania kweli viongozi wetu ni watu wa ajabu saaana tu; iweje bado tunaendeleza MAGAMBA YA MFUMO WA CHAMA KIMOJA KUTEUANA TU TEUANA KI-KADA WA CHAMA na kunyima Watanzania wengine fursa za kushindania nafasi mbalimbali kama vile ya Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, makatibu wakuu na kadhali????

Matokeo ya kuteuana hivi hujenga sana chuki kitaifa maana hata ajira za chini nazo zinakuja kutolewa na mtazamo huo huo wa ki-Chama kwa kulingana na kada aliyeteuliwa awali anavyopendezewa kudumisha uwepo wa chama chake kila sehemu ya kazi.

Kama kweli CCM kimeamua kujivua gamba; hili la ajira za Watanzania kutolewa ki-upendeleo kichama ikome mara moja na tupitishe sheria bungeni kwamba hakuna tena kuteuana.

Hebu fikiria tu kwamba tangu nyumba 10 ni CCM, kata, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Mabalozi, Wkurugenzi - hivi ndivyo kweli Rasilmali za taifa ziwe zikigawiwa kiasi kwamba siku TLP pia kikishika madaraka basi Watanzania wengine tujihesabu tu kwamba hatuna chetu kweli???

Kama kweli tulihiari sisi wenyewe kwenye azimio la Zanzibar kufuata mfumo wa soko huria na basi tukalizingatie kila mahali hata kwenye ajira zetu serikalini. Hili ni jambo ambalo watu tunalinyamazia lakini hasa ndio chimbuko la watu kukichukia zaidi CCM. Ajira ni za Watanzania wote kwa pamoja, malipo yao ni kodi za wote ila ugawaji mkate wa taifa

Hivi hawakuwaona wachapakazi hawa kama vile Marin Hassan Marin, Elia Elias au yule Dada fulani hivi ka-Odhiambo vile??? Jaama eeehhh, haya mambo ya kuteua teua katika karne ya 21 tuache mara moja.

Kama watu tumeamua kufuata mfumo wa soko huria amba kunahitajika kuonekana uchache zaidi wa serikali katika maisha yetu, basi hata ya ajira serikalini nazo ziende ki-ushindani watu watume maombi na mashirika huru yawapembue mpaka kupatikane hata Mheshimiwa Ali Salleh wa BBC Zanzibar bila kumtazama itikadi yake. Uteuzi kila kona ya nchi ni utamaduni wa serikali inayofuata mfumo wa kikiritimba ambapo kila kitu hunyesha kama mvua kutoka kwa watawala tu.

Pindi tunapofanya hivyo (kuzingatia mfumo wa soko huria katika kila tutendalo) hapo ndipo Tanzania inapokua yetu sote. Hii mambo ya kutengeana vyeo ndio inayolea uvivu kazini, kutukuzwa kwa watawala na hatimaye kudidimiza maendeleo ya nchi. Ushindani unatija zake nyingi sana tu.

Hebu tufikirie sana hili.
 
Ajira za namna hii ni kuhakikisha unfriendly habari zinachujwa, na kwamba ahakikishe kamwe hakuna mchakato majimboni!
 
Nimejaribu kutafuta maana na tafsiri sahii ya usemi "kujivua gamba" . Neno gamba kwa maana pana ni kama nyumba au kitu mfano wa container lkinachotumika kuhifadhia kitu/vitu fulani; kwa msingi huo kilio cha watanzania wengi cha kutaka mabadiliko ya kweli kwa wanaoitakia mema nchi hii hakitapata muarobaini . Hivyo basi tusitegemee mabadiliko yoyote kwa sababu, nyoka anapojivua gamba ni ishara ya kukua na kutengeneza gamba kubwa zaidi.
Unajivuaje gamba wakati sumu imeenea mwilli mzima? hapo labda kikombe cha babu tu
 
Back
Top Bottom