Kujipendelea Muhimu

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844
...jamani mara moja moja kujipendelea muhimu. Hizi Romantic Retreats zinasaidia kupunguza usongo wa mawazo kwa wanandoa. Hakuna cha kusema '...Ooh, mambo ya wazungu hayo!'...Picha zote hizi ni Sehemu zilizopo Tanzania.

images

images

Kwa wale wenzangu na mie ambao tukishanuniwa ndio 'hakieleweki mpaka anunuliwe khanga,' si vibaya tukajitutumua na kum-surprise mother house na bonge la week end 'Romantic' retreats kama hizi angalau mara moja kwa mwaka jamani...

566655.jpg

...au sio wazee wenzangu? ...mamsapu wetu deserve to be treated like Queens.

luxury-safari-accommodation-tanzania.jpg

Haipendezi eti mkishaoana , outings zinabakia zile mkihudhuria harusi (tena kwakuwa mlichangishwa!,) au Family Day za makazini!...
Na nyie kina dada na kina mama, msizubae jamani. Nyumba ndogo wanawapiga bao, Ohoo...shauri zenu!
 
Mwee umfanyie hivi wife si ataanza kukulalamikia huko huko ohoo sijui mbona unachezea hela baba watoto si tungetumia kumalizia kibanda haha hahhah
Viva nyumba ndogo sie tunajua kutumia tuuuu:glasses-nerdy::glasses-nerdy::becky:
msinishambulie jamani:madgrin:
 
Hahahahah lol! MR zipo sana hizo! We Baba nanihii lakini huku sikufuja hela? Kile kibanda tutamaliza lini? Hii hela tunayotumia hapa ni sawa na mifuko mingapi ya saruji!?.....Kujirusha mwiko mpaka kibanda kiishe!!!
 
Ingawaje umeongea kimzaha lakin kuna hoja fulani hapa . . . . :whistle:
Lakin Mbu kasema angalau MARA MOJA KWA MWAKA
Nadhani kama pesa inayotumika inatosha kumalizia kibanda hata Baba watoto nae ataliona tu, hawezi kuchezea pesa.
Lakin FURAHA YA WANANDOA ndio muhimu zaid kuliko kumalizia kibanda
Hata mjenge Kasri ya Kifalme, kama hamna furaha ktk ndoa yenu NI KAZI BURE
 
Mwee umfanyie hivi wife si ataanza kukulalamikia huko huko ohoo sijui mbona unachezea hela baba watoto si tungetumia kumalizia kibanda haha hahhah
Viva nyumba ndogo sie tunajua kutumia tuuuu:glasses-nerdy::glasses-nerdy::becky:
msinishambulie jamani:madgrin:
Hii ni kweli kabisa inatokea sana...:becky::becky::becky:
 
Sikujui nikupe nini Mbu,post yako ni nzuri sana,tena sana ngoja nimtafute muhusika naye ajisomee.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
...jamani mara moja moja kujipendelea muhimu. Hizi Romantic Retreats zinasaidia kupunguza usongo wa mawazo kwa wanandoa. Hakuna cha kusema '...Ooh, mambo ya wazungu hayo!'...Picha zote hizi ni Sehemu zilizopo Tanzania.

images

images

Kwa wale wenzangu na mie ambao tukishanuniwa ndio 'hakieleweki mpaka anunuliwe khanga,' si vibaya tukajitutumua na kum-surprise mother house na bonge la week end 'Romantic' retreats kama hizi angalau mara moja kwa mwaka jamani...

566655.jpg

...au sio wazee wenzangu? ...mamsapu wetu deserve to be treated like Queens.

luxury-safari-accommodation-tanzania.jpg

Haipendezi eti mkishaoana , outings zinabakia zile mkihudhuria harusi (tena kwakuwa mlichangishwa!,) au Family Day za makazini!...
Na nyie kina dada na kina mama, msizubae jamani. Nyumba ndogo wanawapiga bao, Ohoo...shauri zenu!

Noted and saved for future use.:violin:
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Yeah, we all want to do this for our wives/husbands, to re-kindle our love
But, truly, an innocent Tanzanian salary man/woman can afford this luxury?
I doubt, may be, after saving for a life time!!
Cheers!
 
Mwee umfanyie hivi wife si ataanza kukulalamikia huko huko ohoo sijui mbona unachezea hela baba watoto si tungetumia kumalizia kibanda haha hahhah
Viva nyumba ndogo sie tunajua kutumia tuuuu:glasses-nerdy::glasses-nerdy::becky:
msinishambulie jamani:madgrin:

...ha ha ha, Maria Roza Mke wa aina hiyo atakuwa hasharifiki japo uliyosema ni kweli tupu!
aahhh, kwenye ndoa hizi...unampata Mke yeye kazi yake kukukatisha tamaa tu! No wonder wanaume wengi
wanajiamulia kujirusha 'Outings' iwe Mango Garden, au hata Dubai na nyumba ndogo

Nice one. Umenichekesha asb asb!

Hahahahah lol! MR zipo sana hizo! We Baba nanihii lakini huku sikufuja hela? Kile kibanda tutamaliza lini? Hii hela tunayotumia hapa ni sawa na mifuko mingapi ya saruji!?.....Kujirusha mwiko mpaka kibanda kiishe!!!

Mzee Mzima MR hajakosea kabisa, zipo sana hizo kwenye ndoa. Maisha haya!
Halafu usipojitutumua utasikia lawama, "Ohhh....mwanaume mbahili weee!...angalia Bwana Kijiko anavyo mstarehesha na kusafiri Mkewe!"
 
Mbu aksante kwa Remainder nzuri kama hii. Duh kama unamfanyia hayo umpendae mbona namwonea wivu!

Ngoja na mimi nitafute wa kumshika mkono nimlete aje asome hapa kama alivyofanya chauro.

MR umenichekesha sanawanawake wengine tunajifanyaga tuna uchungu na maendeleo kuliko wanaume na cha ajabu ni kuwa hatuzipigii kelele zile zinazotumbuliwa karibu kila siku Baba Chanja kwenye viti virefu akizungusha rounds za bia, konyagi, value, JDs; rounds za nyama choma na mafuta ya gari maana viti vingine huwa vinafuatwa mpaka nje ya mji!

Mbu aksante
 
Wewe una mtritigi? kwa kweli mambo kama haya yanaongeza sana mapenzi basi tu hatujagundua, i wish ......
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
<font face="Lucida Sans Unicode"><font color="sienna">Mwee umfanyie hivi wife si ataanza kukulalamikia huko huko ohoo sijui mbona unachezea hela baba watoto si tungetumia kumalizia kibanda haha hahhah<br />
Viva nyumba ndogo sie tunajua kutumia tuuuu

msinishambulie jamani

hahaha sikutarajia kucheka leo
 
Mwee umfanyie hivi wife si ataanza kukulalamikia huko huko ohoo sijui mbona unachezea hela baba watoto si tungetumia kumalizia kibanda haha hahhah
Viva nyumba ndogo sie tunajua kutumia tuuuu:glasses-nerdy::glasses-nerdy::becky:
msinishambulie jamani:madgrin:

Wajua mai dia MR wanawake wengi wako very considerate na sio kama hawapendi kustarehe. Hebu ona hii.....labda mume wake ni mfanyakazi wa serikali na ukweli kipato sio kikubwa kivile na wanawatoto wanaosoma msondo ngoma shule ya msingi na wao wenyewe wamepanga mahali. Mara mume anakuja na hili la kujiliwaza mahali...........unadhani mama ataliafiki kirahisi........hapana cos mama anafikiria watoto watakula nini, michango ya upe na ujenzi mashuleni, nyumba ndio hivyo tena ya kupanga na mama mwenye nyumba kila siku maneno ya mafumbo kwa mama na watoto wake......... hapo chochote kitakacho patikana kwa baba lazima mama afikirie kwanza kupata kibanda chake na wtoto na hayo mengine baadae.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom