Wakuu mi nna ka account kangu kwenye benki ya makabwela, NMB. Nakumbuka miezi ka minne hivi iliyopita nilikuwa nna sh alfu 40 , na nilikuwa nimepoteza kadi so nikaenda ndani kwenye counter nikadraw pesa yote(40) halafu ndani ka ya dakika tano baada ya kupewa pesa nikafikiri hawa watakuwa hawaja update database zao. Nikachukua simu yangu ya mkononi nikabofya kupitia NMB Mobile nikafanikiwa kununua vocha za sh 40. Nikajua watanipigia au ntakuta na negative elfu 40 waki upadate system au tu watakata nikiweka pesa. La tofauti na matarajio yangu kuna pesa niliwekewa baada kama ya mwezi na hawajakata chochote mpaka sasa? Swali langu je hii ina madhara gani kisheria za kibiashara incase naongeza ongeza kakiwango na kuzitoa kila mara kwa kamchezo haka? Ukizingatia hatuna mkataba wa kukopeshwa pesa kutoka kwenye hizi akaunti za kawaida?