Kujiandikisha Dar es Salaam

Pepe Rainer

Member
Jan 27, 2010
23
0
Tarehe 22-27 Machi, 2010 ni tarehe za kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kwa wakazi wote wa Dar es salaam, wote ambao umri unazidi miaka 18 twende tukajiandikishe.

Kitambulisho kikiwa kimehalibika maandishi kutoonekana vizuri,nenda ukajiandikishe upate kitambulisho kipya.

Kama ulijiandikisha na jina lako halikutokea katika orodha ya wapiga kura na hukuweza kupiga kura,nenda kajiandikishe upya jina lako liingie katika orodha ya wapiga kura.

Mwaka 2010 sio mwaka wa kukosea,kajiandikishe upate kitambulisho cha kukuwezesha kupiga kura,kutimiza haki yako ya kimsingi.Kura yako kwa maendeleo yako,kajiandikishe

TANZANIA BILA MAFISADI INAWEZEKANA, KAJIANDIKISHE!
 
Kuna wale waliouza vitambulisho vyao kwa pesa ndogo na doti za kanga kwa ajili ya njaa zao wakajikuta wanakosa huduma muhimu za kibenki na kijamii kwa miaka mitano mfululizo, hii ni nafasi yao ila wasiendekeze njaa, baadae itakua rahisi kupata kitambulisho cha uraia kama cha kupigia kura unacho.
 
Asante sana kwa kutukumbusha, maana mimi ni mmoja wa watu waliopoteza kitambulisho, niliibiwa mkoba na kadi ya kura ndani ikiwemo.

Asante sana Pepe Rainer
 
Kama kuna mtu anaelewa hili naomba anijulishe:

Mimi ni mkazi wa Dar, kadi yangu ya kupiga kura imepotea. Awali nilijiandikisha kituo cha Kimara Stop-over (wilaya ya Kinondoni), lakini sasa naishi Tabata (wilaya ya Ilala). Kwenda Kimara ku-renew ambako ndio kituo changu cha awali naona taabu kwa ajili ya foleni na muda mwingi utapotea. Je, naweza kujiandikisha hapa hapa Tabata?

Nikikumbuka mheshimiwa JK naye alihamia Msoga badala ya Chalinze alipopiga kura awali.
 
Watu walioajiliwa kufanya kazi ya kuandikisha wapiga kura mkoa wa DSM kwa ujumla ni very slow!! Wananchi wanatumia muda mwingi sana vituoni kujiandikasha, mfano rafiki yangu mmoja anaeishi Mbezi Beach kwa Sykes alikwenda kwenye kituo cha pale barabara mpya ya lami shuleni na kungoja kwa takribani saa NNE ndio akafanikiwa kupigwa picha na kupata kadi!! Something has to be done to speed up the exercise otherwise there might be a danger of some potential voters to just give up the registration exercise; which will be stupid anyway!.
 
Kama kuna mtu anaelewa hili naomba anijulishe:

Mimi ni mkazi wa Dar, kadi yangu ya kupiga kura imepotea. Awali nilijiandikisha kituo cha Kimara Stop-over (wilaya ya Kinondoni), lakini sasa naishi Tabata (wilaya ya Ilala). Kwenda Kimara ku-renew ambako ndio kituo changu cha awali naona taabu kwa ajili ya foleni na muda mwingi utapotea. Je, naweza kujiandikisha hapa hapa Tabata?

Nikikumbuka mheshimiwa JK naye alihamia Msoga badala ya Chalinze alipopiga kura awali.

MWENYE JIBU TAFADHALI - au nitwangie +255767266454
 
mimi tayari wenzangu nanyi kajiandikisheni

hongera sana Pengo kwa kufanikisha hilo.

watu wengi sana tumehama makazi katika kipindi hiki cha miaka 5 iliyopita, na ukizingatia nafasi za kutoroka kwa wafanyakazi wa sekta binafsi ni finyu basi taabu tupu ... nimeangalia kwa calendar 27th march (dealine) itakuwa ni Jmosi, hivyo unless uwahi sana vinginevyo ni kukesha kwenye foleni ... na kupoteza muda (kwenye foleni ndefu) hatimaye kukata tamaa na kukosa haki ya msingi ya kikatiba ... nadhani yatubidi tu kuiba mchana mmoja within these working days na kwenda kujiandika kabla ya jmosi coz nahisi patakuwa hapakaliki kwa hizo queue.

nina hamu sana ya kupiga kura ya kuwatosa mbunge 'bubu' wa jimbo langu na mgombania nafasi ya urais fulani hivi .......!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom